KLABU ya Al Ahli ya Saudi
Arabia imethibitisha na kuweka wazi kuwa imemteua Vitor Pereira kuwa kocha mpya wa klabu
hiyo baada kocha huyo kuondoka Porto mwishoni mwa msimu huu. Pereira
ameifundisha Porto kwa kipindi cha misimu miwili baada ya kuchukua
nafasi ya Andre Villas-Boas Juni mwaka 2011 na kuisadia klabu hiyo
kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu nchini Ureno. Katika taarifa
iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo, Pereira mwenye umri wa miaka
44 atajiunga rasmi na klabu hiyo Juni 27 kabla ya kuiandaa timu kwa
ajili ya msimu ujao siku mbili baadae. Pia zimekuwepo taarifa kuwa
atatua katika klabu hiyo na wasaidizi wake wa watatu kutoka Ureno kwa
ajili ya kuimarisha benchi lake la ufundi.
Monday, June 10, 2013
MMOJA APOTEZA MAISHA KATIKAMICHUANO YA LANGALANGA YA CANADIAN.
MASHINDANO ya langalanga ya Canadian Grand Prix jana yalimalizika kwa Majonzi makubwa baada ya mmoja wa wafanyakazi mwenye umri wa miaka 38 kufariki baada ya kukanyagwa na winji. Ajali hiyo ilitokea wakati gari la dereva Esteban Gutierrez wa timu ya Sauber lilipokuwa likiondolewa barabara za Montreal baada ya kupata ajali.
Mashuhuda
wanasema wakati winji hilo likijaribu kuliondoa gari hilo ndipo
mfanyakazi huyo aliangusha radio yake na wakati akiiokota ndipo
alipokanyagwa kwasababu dereva wa winji hakumuona. Katika
ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter Gutierrez alituma salamu
zake za rambirambi kwa familia ya mfanyakazi huyo kwa kumpoteza mtu wao
karibu. Mbali na
Gutierrez madereva wengine waliotoa rambirambi zao ni pamoja na
Sebastian Vettel wa Red Bull aliyeshinda mbio hizo pamoja na Fernando
Alonso wa Ferrari aliyeshika nafasi ya pili. Hilo
ni tukio la pili kutokea katika mashindano hayo kwani mwaka jana katika
michuano ya Grand Prix ya Italia mfanyakazi wa kujitolea wa zimamoto
Paolo Ghislimberti alifariki kutoka na amejraha aliyopata kichwani na
kifuani baada ya kupigwa na tairi lililochomoka kutoka katika gari la
Heinz-Harald Frentzen wa timu ya Jordan.TAIFA STAR YATUA NCHINI IKITOKEA NCHINI MORROCO.
TIMU
ya taifa ya Tanzania,
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imewasili nchini leo asubuhi.
Taifa stars ilikuwa Morocco kucheza na wenyeji wao
ambapo katika mchezo huo taifa star imefungwa bao 2-1 katika mechi ya Kundi C
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Stars ambayo bado inashika nafasi ya pili katika kundi hilo
ikiwa na pointi sita imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere.
Aidha katika kundi c kinara wa kundi hilo ni Ivory Coast yenye point kumi ambayo
itacheza mchezo wa marudiano na Taifa Star wikiendi ijayo katika uwanja wa
taifa jijini Dar es salaam.
Hata hivyo kwa upande wa kundi hilo nafasi ya tatu
inashikiliwa na Morocco yenye point tano huku nafasi ya mwisho ikishiliwa na
Gambia yenye point moja.
KUNDI C
Pos
|
Team
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
Pts
|
1
|
Ivory Coast
|
4
|
3
|
1
|
0
|
10
|
2
|
8
|
10
|
2
|
Tanzania
|
4
|
2
|
0
|
2
|
6
|
6
|
0
|
6
|
3
|
Morocco
|
4
|
1
|
2
|
1
|
6
|
7
|
-1
|
5
|
4
|
Gambia
|
4
|
0
|
1
|
3
|
2
|
9
|
-7
|
1
|
Subscribe to:
Posts (Atom)

