Wednesday, May 15, 2013

FRANK LAMPARD BADO NIPO NIPO SANA CHELSEA SAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA.

KIUNGO mkongwe wa timu ya taifa england na klabu ya Chelsea, Frank Lampard amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja utakaomuweka Stamford Bridge kwa msimu mmoja zaidi. Nyota huyo ambaye ana rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi Chelsea mustakabali wake umekuwa gumzo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita lakini sasa ameamua kubakia hapo kwa msimu mwingine. Lampard ambaye mkataba wake wa zamani ulikuwa umalizike mwishoni mwa msimu huu alikuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia katika Ligi Kuu nchini Marekani kwenye klabu ya Los Angeles Galaxy kabla Chelsea hawajampatia mkataba huo mpya wa miezi 12. Mashabiki wa soka wa Chelsea wamekuwa wakipeperusha mabango katka mechi za timu hiyo wakitaka nyota huyo aliyefunga mabao 203 na kuipita rekodi ya Bobby Tambling aendelee kuwepo hapo. Lampard anatarajiwa kuwa nahodha wa kikosi cha Chelsea ambacho kitajitupa uwanjani baadae kucheza na Benfica ya Ureno katika fainali ya michuano ya Europa League jijini Amsterdam.

    FRANK LAMPARD KATIKA KATIKA HARAKARI ZA SOKA DUNIANI

Jina :Frank Lampard
Urefu
1.83 m (6 ft 0 in)
Playing position
[Midfielder]
TIMU YA SASA
Current club
                       TIMU YA UKUBWA
Miaka
Timu
Apps
(Gls)
1994–2001
148
(24)
2001-
363
(125)
Timu ya Taifa ya Kandanda
1999
90
(23)

FIFA YAONYA MAOFISA WA JIJI LA SAO PAULO KUHUSU KUPOTEZA HAKI YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2014

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeonya maofisa wa jiji la Sao Paulo kwamba wanaweza kupoteza haki ya kuandaa baadhi ya mechi za Kombe la Dunia 2014 kwasababu ya kuchelewa kukamilika kwa uwanja. Tishio hilo limeleta hasira kwa wamiliki wa kiwanja cha Corinthians ambao wamedai kuwa FIFA wanaweza kuwanyima haki hiyo kama wakitaka lakini hawawezi kufanya kazi chini shinikizo. Katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke amesema shirikisho hilo haliwezi kukubali kitu chochote ambacho kitapelekea uwanja huo ambao utachezwa mechi sita ikiwemo ile ya ufunguzi, kushindwa kufikia tarehe ya mwisho waliyowekewa. Mafundi tayari wameonya kuwa uwanja huo hautarajiwa kuwa tayari mpaka mwishoni mwa Februari mwakani. Valcke amesema kuanzia sasa mpaka hapo tiketi zitakapoanza kuuzwa wana uwezo wa kubadilisha mechi hizo katika viwanja vingine vilivyo tayari, hivyo wanasubiri mpaka Agosti mosi ili kuangalia uwezekano wa kubadilisha viwanja.

FAINALI EUROPA LIGI- LEO JUMATANO CHELSEANI VS BENFICA DIMBANI


Katika mechi ya kukata na shoka kesho jumatano mei 15 ni fainali ya europa ligi  kati ya chelsea wakitinga katika jijini  la amsterdam huko uholanzi  kukipiga  benfica  ya ureno huku chelsea ikiwazakuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kabisa kuweza kutwaa ubingwa wa uefa championz ligi na europa ligi mfululizo.
endapo chelsea wataibuka na ushindi basi itakuwa klabu ya nne barani uaya kuweza kutwaa makombe yote makubwa wakifuatiwa na juventus ,afc ajax na fc bayen munich ambazo zimeshawahi kushinda kombe la washindi mwaka 1970-71 na 1997-98.
FAINALI:EUROPA LIGI 
REKODI KWA TIMU HIZI"
Benfica

1989/90 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa 1-0 na  AC Milan
1987/88 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa Penati 6-5 na PSV Eindhoven (Sare 0-0)
1982/83 UEFA Cup: Walifungwa Jumla Bao 2-1 kwa Mechi 2 na  RSC Anderlecht 
1967/68 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa 4-1 na Manchester United
1964/65 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa 1-0 na FC Internazionale Milano
1962/63 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa 2-1 na AC Milan
1961/62 Klabu Bingwa Ulaya: Washindi 5-3 na Real Madrid CF
1960/61 Klabu Bingwa Ulaya: Washindi 3-2 na FC Barcelona
Chelsea:
2011/12 UEFA Champions League: Washindi Penati 4-3 na Bayern Münich (1-1)
2007/08 UEFA Champions League: Walifungwa 6-5 na Man United FC (Sare 1-1)
1997/98 Kombe la Washindi: Washindi 1-0 na VfB Stuttgart
1970/71 Kombe la Washindi: Washindi 2-1 na Real Madrid (sare 1-1)
Timu hizi mbili zote zimetinga Fainali hii baada ya kutolewa katika hatua za
 Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, na hatimaye kushiriki EUROPA LIG.
EUROPA LIGI-WAFUNGAJI BORA:
-8 Libor Koza [Lazio]
-7 Edinson Cavabi [Napoli]
-6 Oscar Cardozo [Benfica]
-6 Rodrigo Palacio [Inter Milan]
-5 Fernando Torres [Chelsea]
Chelsea na benfica zilikutana kwa mara ya kwanza kwenye Mashindano ya Klabu Barani Ulaya 
Mwaka jana kwenye Robo Fainali ya UCL na Chelsea, chini ya Meneja Roberto Di Matteo,
iliifunga Benfica nje ndani, 1-0 huko Lisbon na 2-1 Stamford Bridge, wakiwa njiani kulitwaa Kombe hilo.
Kwa Benfica, hii itakuwa Fainali yao ya 9 Barani Ulaya na kwa Chelsea ni ya 5 lakini Chelsea wameshinda Fainali hizo 3 na Benfica 2 huku Benfica wakiwa wapo kwenye wimbi la kufungwa katika Fainali 6 tangu washinde ile ya Klabu Bingwa Ulaya Mwaka 1962 ila hii ni Fainali yao ya kwanza baada ya Miaka 23.
DONDOO ZA MAKOCHA WOTE WAWILI.


-Akiwa Liverpool, Rafael Benitez wa Chelsea alisimamia Mechi 4 dhidi ya Benfica 
na kushinda 1 tu na kufungwa 3.
-Katika Mechi za UEFA, Bernitez amesimamia Mechi 138 na Jorge Jesus wa Benfica 
Mechi 74 Baada ya kutwaa Taji hili na Valencia Mwaka 2003/04,
Benitez anaweza kuwa Kocha wa Pili, baada ya Giovanni Trapattoni ambae ameshinda mara 3,
kulitwaa na Klabu mbili tofauti Wengine waliotwaa mara mbili ni Luis Molowny akiwa
(Real Madrid, 1985 na 1986) na Juande Ramos (Sevilla FC, 2006 na 2007).

Tuesday, May 14, 2013

AL AHLY KUUMANA USO KWA USO NA USO NA MAHASIMU WAO MISRI ZAMALEK

Katika Jijini Cairo, Misri  hii leo Droo ya hatua ya Makundi ya Mashindano ya CAF ya CHAMPIONZ 
LIGI imechukua nafasi na Mabingwa Watetezi Al Ahly wataanza utetezi wa Taji lao kwa kucheza Ugenini na wenzao Mahasimu wao wakubwa wa huko Misri Zamalek ambao wamepangwa pamoja kwenye Kundi A.
Hii ni mara ya pili kwa Miaka miwili mfululizo kwa
 Miambahiyo ya Misri kupangwa Kundi moja kwenye
michuano hii na safari hii wako pamoja na Orlando
 Pirates ya SouthAfrica na Timu mpya kwenye
 Mashindano haya ACLeopards ya Congo ambayo
 Mwaka jana ilitwaa Kombe la Shirikisho.
aidha Kundi B lina Timu za Esperance ya Tunisia, ambayo ndio ilitolewa Fainali na
 Al Ahly kwenye michuano hii Mwaka jana, na nyingine ni Coton Sport ya Cameroo
n, Sewe Sport ya Ivory Coast na Recreativo de Libolo of Angola, ambao ndio
 waliwatupa nje ya michuano hii waliokuwa Mabingwa wa Tanzania, Simba SC.
hata hivyo Mechi za Makundi zitachezwa kwa Mtindo wa Ligi wa Nyumban
i na Ugenini na Washindi wawili wa juu wa kila Kundi watasonga Nusu Fainali.
Mechi za Makundi zitachezwa kuanzia Julai hadi Septemba huku Nusu Fainali
ikitarajiwa kuwa Oktoba.
DROO:
KUNDI A
Al Ahly  (Egypt)
AC Leopards (Congo)
Orlando Pirates (South Africa)
Zamalek (Egypt)
KUNDI B
Esperance (Tunisia)
Coton Sport (Cameroon)
Recreativo de Libolo (Angola)
Sewe Sport (Ivory Coast)
HABARI HII YA CHINI TULIITOA MEI 7
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: DROO RAUNDI YA MCHUJO YAFANYWA"
DROO YA RAUNDI YA MCHUJO:
TP Mazembe (DRC) v Liga Muculmana (Mozambique)
St George (Ethopia) v ENPPI (Egypt)
Stade Malien (Mali) v Lydia Academic (Burundi)
Enugu Rangers (Nigeria) v CS Sfaxien (Tunisia)
FUS Rabat (Morocco) v FAR Rabat (Morocco)
CA Bizertin (Tunisia) v Ismaily (Egypt)
Entente Setif (Algeria) v US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia (Algeria) v Etoile Sahel (Tunisia)
-MECHI KUCHEZWA Mei 17-19 na Marudiano Mei 31-Jun1 2
-FAHAMU: WASHINDI 8 WA RAUNDI HII WATAINGIZWA KWENYE
 DROO KUPANGA MAKUNDI MAWILI YA TIMU 4 KILA MOJA.

VICENTE ASEMEA NEYMAR HUENDA AKAELEKEA BAYEN MUNICH

OFISA wa zamani wa klabu ya Santos ya Brazil, Vicente Cascione amedai kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Neymar ataondoka kwenda klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani katika kipindi cha majira ya kiangazi kuungana na kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola. Barcelona ndio wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kupata saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye amepanga kwenda Catalunya baada ya michuano ya Kombe la Shirikisho kuzungumzia uhamisho wake wakati Real Madrid nao wakimnyatia kimya kimya nyendo zake. Hata hivyo, Cascione amesisitiza kuwa Neymar atakwenda kucheza katika Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bundesliga kwani tayari taratibu za uhamisho kwenda Allianz Arena umeshakamilika. Ofisa huyo aliandika katika blog yake kuwa amezinasa taarifa hizo akiwa wa kwanza kwamba Neymar tayari ameshamwaga wino Bayern hivyo hatakwenda Hispania kama inavyodhaniwa na wengi.

BLATTER ASEMA AS ROMA WALIYOPEWA ADHABU NDOGO KWA UBAGUZI.


RAIS wa Shirikisho ka Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ameponda adhabu ya faini ya kiasi cha euro 50,000 waliyopewa klabu ya AS Roma ya Italia kwa tabia za kibaguzi walizoonyesha mashabiki wake akidai kuwa ni ndogo na haikubaliki. Blatter amesema atazungumza na Shirikisho la Soka la Italia ambalo amedai kuwa hawakufanya uchunguzi wa kutusha kuhusiana na tukio hilo la lililotokea Jumapili iliyopita katika katika mchezo kati ya AC Milan na Roma kwenye Uwanja wa San Siro. Blatter aliuambia mtandao wa FIFA kuwa ameshangazwa na kushindwa kuelewa kwanini kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka la nchi hiyo itoe maamuzi wa kuwatoza faini Roma kwa kipindi kifupi namna hiyo bila kuchunguza tukio kwa undani. Amesema kiwango walichotozwa Roma ni kidogo sana ukilinganisha ukubwa wa tatizo lenyewe ndio maana anataka kuzungumza na shirikisho hilo kuwatahadharisha kuwa njia waliyotumia sio sahihi kama wanataka kutokomeza tatizo hilo.

MFAHAMU KWA UZURI ROBERTO MANCIN KATIKA HARAKATI ZA SOKA DUNIA

Roberto Mancini
Roberto Mancini 008.jpg
Taarifa kuhusu yeye
Full nameRoberto Mancini
Date of birth27 November 1964 (age 48)
Place of birthIesi, Italy
Height1.79 m (5 ft 10 12 in)
Playing positionAttacking midfielder/Second striker
Timu alizocheza
mwakaTimumechi (Goli)
1981–1982Bologna30(9)
1982–1997Sampdoria424(132)
1997–2001Lazio87(15)
2001Leicester City (loan)4(0)
Total545(156)
Timu ya taifa
1982–1986Italy U2126(9)
1984–1994Italy36(4)
Timu maneja
2001–2002Fiorentina
2002–2004Lazio
2004–2008Internazionale
2009–2013Manchester City


MATAJI ALIOTWAA NA TIMU HIZI

Sampdoria
Serie A (1): 1990-1991
Coppa Italia (4): 1984-85, 1987-88, 1988-89, 1993-94
Supercoppa Italiana (1): 1991
Kombe la UEFA Cup Winners '(1): 1989-1990

Lazio
Serie A (1): 1999-2000
Coppa Italia (2): 1997-98, 1999-2000
Supercoppa Italiana (1): 1998
Kombe la UEFA Cup Winners '(1): 1998-1999
UEFA Super Cup (1): 1999

TIMU MANEJA
Fiorentina
Coppa Italia (1): 2000-01
Lazio
Coppa Italia (1): 2003-04

Internazionale
Serie A (3): 2005-06, 2006-07, 2007-08
Coppa Italia (2): 2004-05, 2005-06
Supercoppa Italiana (2): 2005, 2006

Manchester City
Ligi Kuu (1): 2011-12
Kombe la FA (1): 2010-11
FA Community Shield (1): 2012

TUZO NA MAFANIKIO
Guerin d'Oro (2): 1987-88, 1990-91
Serie Mchezaji wa Mwaka (1): 1996-1997
Italia Mchezaji wa Mwaka (1): 1996-1997
Albo Panchina d'Oro (1): 2007-08
Ligi Kuu ya Meneja wa Mwezi (2): Desemba 2010, [95] Oktoba 2011