Kocha wa Real madrid Jose Mourinho pamoja na nyota wa
klabu hiyo Cristiano Ronaldo wamefungiwa mechi mbili za michuano ya Kombe la Mfalme baada ya kutolewa
nje katika fainali dhidi ya Atletico Madrid. Mourinho
mwenye umri wa miaka 50 alitolewa nje baada ya kumshambulia mwamuzi kwa
maamuzi aliyotoa adhabu ambayo hataweza kuitumikia baada ya kutangaza
kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu. Ronaldo
mwenye umri wa miaka 28 alipewa kadi nyekundu baada kukutwa na hatia ya
kumpiga teke la uso kwa makusudi mchezaji wa Atletico, Gabi. Wote wawili Ronaldo na Mourinho watakuwepo katika michezo miwili ya mwisho ya ligi ya Madrid.
Thursday, May 23, 2013
TIMU YA TAIFA YA CAMEROON YAPATA KOCHA MPYA.
Timu ya taifa ya Cameroon imefanikiwa kupata kocha mpya Volker
Finke kuwa kocha mkuu wa timu hiyo huku kibarua chake cha kwanza Mjerumani huyo ni kuhakikisha timu hiyo inafuzu michuano ya
Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Finke
anachukua nafasi ya kocha wa muda wa timu hiyo Jean-Paul Akono ambaye
aliwekwa hapo kuziba nafasi ya Denis Lavagne Septemba mwaka jana baada
ya Mfaransa huyo kushindwa kuisaidia timu hiyo kufuzu michuano ya
Mataifa ya Afrika 2012 na 2013. Kocha
huyo mwenye umri wa miaka 65 aliwahi kuifundisha klabu ya SC Freiburg
kuanzia mwak 1991 mpaka 2007 na atakuwa anafundisha kikosi cha timu ya
taifa kwa mara ya kwanza baada ya kutemwa na timu ya Urawa Red Diamonds
ya Japan na timu ya Cologne ya nchini kwake. Katika
mechi za kufuzu Kombe la Dunia, Cameroon wako kileleni mwa kundi I
wakiwa na alama sita katika mechi tatu walizocheza wakifuatiwa na Libya
wenye alama tano, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC alama nne na Togo
alama moja. Kazi
yake ya kwanza Finke itakuwa ni kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya
nchi hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ukraine utakaochezwa jijini
Kiev Juni 2 mwaka huu kabla ya kuhamishia nguvu zao katika mechi za
kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Togo Juni 9, DRC Juni 16 na Libya
Septemba 6 mwaka huu
CLUB YA SANTOS YAKATAA OFA YA PILI YA BARCA
MAKAMU wa rais wa klabu
ya Santos ya Brazil, Odilio Rodrigues amedai kwamba wamekataa ofa ya klabu
ya Barcelona ya Hispania kutaka kumsajili mshambuliaji wao nyota Neymar
kwa mara ya pili. Katika
siku za hivi karibuni Barcelona ndiyo pekee wameonyesha nia ya kumhitaji
mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil na kuripoti kuwa walitaka
kuwapa Santos euro milioni 20 ili waweze kumiliki haki za mchezaji huyo
kwa asilimia 55. Wakati
mahasimu wao nao Real madrid wakiongeza mbio ya kumfukuzia mshambuliaji huyo,
Barcelona walitoa kiasi hicho ili waweze kumaliza suala hilo lakini
Rodrigues amesisitiza kuwa hawana haraka ya kumuuza Neymar kwa kiasi
kidogo kuliko wanachotaka. Rodrigues
alithibitisha kuwa ni kweli walipata ofa ya Barcelona kwa mara ya pili
lakini waliikataa kwasababu hawakufikia kiwango walichokuwa
wakikihitaji. Neymar
katika siku karibu ameweka wazi nia yake ya kubakia Santos mpaka baada
ya michuano ya Kombe la Dunia 2014, ingawa uhamisho wa kwenda barani
Ulaya katika kipindi hiki cha usajili unaonekana kama unaweza kuwepo.FA CHADAI KUWA CARROL AJITOA TIMU YA TAIFA KUTOKANA NA MAJERUHI.
CHAMA cha Soka nchini Uingereza {FA} kimedai kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa nchi hiyo, Andy Carroll amejitoa katika timu ya taifa kutokana na kuwa majeruhi. Carroll mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya kisigino baada ya kocha wa timu ya taifa Roy Hodgson kumuita katika kikosi chake ambacho kitacheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki kati ya Ireland Mei 29 na Brazil Juni 2 katika Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro. Mshambuliaji huyo wa Liverpool amekuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya West Ham United msimu uliopita huku vyombo vya habari nchini Uingereza vikiripoti kuwa klabu hiyo imekubali kumchukua moja kwa moja kwa ada ya paundi milioni 15. Carroll anaungana na nahodha wa Liverpool Steven Gerrard na kiungo wa Arsenal Jack Wilshere kukosa mechi hizo za kujipima nguvu kabla ya mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Moldova na Ukraine Septemba mwaka huu.KOCHA WA LIVERPOOL RODGERS HANA MPANGO WA KUMUUZA SUAREZ.
BOSI wa majogoo wa jiji la londo Liverpool Brendan Rodgers amesema hana mpango wa kumuuza mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Luis Suarez. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay alikosa mechi nne za Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kufungiwa mechi 10 kwa kumng’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic lakini alimaliza katika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu nchini Uingereza akiwa na mabao 23. Liverpool haijafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya toka mwaka 2009 lakini pamoja na vilabu vikubwa kummezea mate Suarez, kocha huyo ana imani kwamba ataweza kumbakisha mchezaji huyo kwa msimu ujao. Rodgers amesema kwasasa wanajipanga kutengeneza kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao na Suarez ni sehemu ya kikosi hicho ingawa amekiri kwamba zipo baadhi ya klabu kubwa zinazomtaka.
GARCIA AMUOMBA RADHI MCHEZAJI NAMBA MOJA TIGER WOODS
MCHEZAJI machachali wa mchezo wa gofu, Sergio Garcia ameomba radhi kwa kauli yake ambayo inaweza kuonekana kama ya kibaguzi kwenda kwa nyota wa mchezo huo anayeshika namba moja kwa ubora Tiger Woods. Garcia mwenye umri wa miaka 33 aliulizwa kama ataweza kula chakula cha jioni na Woods ili kuzungumzia tofauti zao za hivi karibuni na mchezaji huyo kutania kuwa atamuandalia kuku wa kukaanga nyota huyo. Kuku wa kukaanga ni chakula kinachohusishwa na watu weusi huko Marekani haswa wale wanaotoka kusini mwa nchi hiyo. Garcia aliomba radhi kwa kauli hiyo kama imeeleweka vibaya akidai kuwa hakumaanisha chochote kuhusu ubaguzi wa rangi kwa nyota huyo ambao ambaye asili yake ni mweusi.
MURRAY AJITOA MICHUANO YA WAZI UFARANSA:
MCHEZAJI nyota maarufu wa tenisi kutoka Uingereza Andy Murray amejitoa katika michuano ya wazi ya Ufaransa kutokana na maumivu ya mgongo yaliyopelekea kushindwa kuendelea kucheza katika michuano ya wazi ya Italia. Murray ambaye anashika namba mbili katika orodha za ubora Duniani kwa upande wa wanaume amejitoa katika michuano hiyo baada ya kushauriwa na madaktari wake na anatarajia kurejea tena uwanjani katika michuano ya Wimbledon katikati ya mwezi ujao. Nyota huyo ambaye ni bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani amesema umekuwa ni uamuzi mgumu kufanya kwani huwa anapenda kucheza jijini Paris lakini imekuwa nje ya uwezo wake kwasababu ya ushauri wa kiafya aliopewa. Murray aliwaomba radhi waandaaji wa michuano hiyo na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumtumia ujumbe wa kumuunga mkono na sasa kazi kubwa aliyokuwa nayo ni kuhakikisha anapona na kurejea haraka uwanjani.
Subscribe to:
Posts (Atom)




