Monday, August 12, 2013

TOURE YAYA ATWAA UCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA ASILIMIA 32%

YaYa Toure kiungo mahiri wa kimataifa wa Ivory Coast  na club ya man city ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo katika msimu wa 2012-2013 baada ya kupata asilimia 32 ya kura zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo na watumiaji wa mtandao. Toure mwenye umri wa miaka 30 anayecheza katika klabu ya Manchester City anafuatia na mshambuliaji nyota wan chi hiyo Didier Drogba aliyepata asilimia 24 wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Bony Wilfried aliyepata asilimia 17. Wengine ni Aroune Kone ambaye amejiunga na timu ya Everton akitokea Wigan mwezi uliopita pamoja na Gervino aliyejiunga na AS Roma akitokea Arsenal ambao wote kwa pamoja wamepata asilimia 15 ya kura zilizopigwa. Hiyo inakuwa mara ya tatu Toure kushinda tuzo hiyo mara nyingine ikiwa mwaka 2008 na 2009.

LIVERPOOL YAIKINGIA KIFUA BARCA KUHUSU AGGER

Wakala wa beki mahiri wa club ya Liverpool, Daniel Agger amesema kuwa Liverpool imeitupilia mbali ofa iliyotumwa na Barcelona kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo. Barcelona imekuwa ikihusishwa na kutaka kusajili mabeki kadhaa wa Ligi Kuu nchini Uingereza ambapo tayari walishatoa kitita cha euro milioni 25 kwa ajili ya beki wa Chelsea David Luiz. Chelsea waliweka wazi kuwa mabingwa wa soka nchini Hispania wanapoteza muda wao na sasa wakala wa Agger aitwaye Per Steffensen naye amebainisha kuwa Liverpool tayari wamepiga chini ofa hiyo. Wakala huyo amesema mteja wake bado ana mkataba wa miaka mitatu na Liverpool hivyo ni juu ya makubaliano ya klabu hizo mbili kuhusu ada ya uhamisho.

MAKOCHA 32 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA COPA COCA-COLA

Makocha 32 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanashiriki kozi ya Copa Coca-Cola inayoanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA).

Kozi hiyo itakayomalizika Agosti 17 mwaka huu itafunguliwa saa 3 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre na washiriki wote tayari wameshawasili Dar es Salaam. Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo kutoka Mauritius.


Washiriki wa kozi hiyo ni Ahazi Ibrahim Kasegese (Mbeya), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Asuri Msakamali (Simiyu), Bakari Khamis Kilambo (Kaskazini Pemba), Chacha Sambulo (Mara), Charles Rwezaura (Kagera), Daniel Sambala (Njombe), Dudu Haruni (Iringa) na Emmanuel Kapurata (Rukwa).


Faki Makame Haji (Kaskazini Unguja), Fatawi Khamis Sheha (Kusini Pemba), Hamisi Omary Mabo (Kigoma), Hussein Maulid (Morogoro), Issa Lugaza (Kilimanjaro), James Gaspar (Shinyanga), James Wambura (Arusha), Jomo Jackson Puccey (Lindi), Joseph Sihaba (Dodoma), Kelvin Haule (Ruvuma) na Kessy Juma Abdallah (Tanga).


Kessy Mziray (Mwanza), Menswi Mchwampaka (Kinondoni), Mohamed Abdallah Kweka (Singida), Nurdin Gogola (Temeke),  Pius Kamande (Rukwa), Ramadhan Abrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Ramadhan Salum Mnyoti (Manyara), Raphael Ngeleja (Geita), Samuel Edgar Maokola (Ilala), Shaweji Nawanda (Mtwara) na Vuai Abdul Haji (Kusini Unguja).


Fainali za U15 Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa zitafanyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

 SEMINA YA MAKAMISHNA YAANZA DAR, MWANZA
Semina kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa  waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa 2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza.


Mafunzo hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam wakati kituo cha Mwanza kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.


Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.


Kituo cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.


Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.


Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Friday, July 26, 2013

BAYERN VS DORTMUND JUMAMOSI

Club ya Bayern Munich na Borussia Dortmund zinataraji kushuka dimba siku Jumamosi katika Mechi ya fungua pazi Msimu mpya kugombea

German Super Cup haya yakiwa kama Marudiano ya Fainali ya Mwezi Mei Uwanjani Wembley ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Bayern walishinda Bao 2-1 na kuweka historia ya kuwa Klabu ya kwanza Nchini Germany kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa Germany, Kombe la Germany na Ubingwa wa Ulaya.
Hata hivyo, Dortmund wamesema wao hawasaki kisasi pale Beki wao anaechezea Germany, Mats Hummels, aliposema: “Hii si kisasi cha Wembley! Ni mtihani mzuri kuonyesha Msimu huu tukoje!”
Kawaida German Super Cup hugombewa na Bingwa na yule Mshindi wa Kombe la Germany lakini kwa vile vyote vilichukuliwa na Bayern Msimu uliopita, Mshindi wa Pili wa Bundesliga, ambae ni Borussia Dortmund aliemaliza Pointi 25 nyuma, ndie atacheza na Bayern Munich.
Sura Mpya
Kila Timu, Bayern Munich na Borussia Dortmund, zitaingia kwenye Mechi hii na sura mpya huku Bayern ikiwa na Kocha mpya Pep Guardiola aliembadili Jupp Heynckes, Thiago Alcantara wa Spain akiwa Bayern kutoka Barcelona na Mario Gotze akiwa pia Bayern kutoka Dortmund.
Dortmund pia wanao wapya ambao ni Viungo Pierre-Emerick Aubameyeng toka St Etienne na Henrikh Mkhitaryan kutoka Shakhtar Donetsk lakini wote hawa wapya huenda wasicheze kutokana na kuwa na maumivu.
Tayari Tiketi zote, 80,654 za Westfalenstadion, kama ilivyo maarufu Signal Iduna Park, zimeshauzwa na Mechi hii itatangazwa Nchi 195 Duniani.

Thursday, July 25, 2013

MESSI AKIRI KUWA MATATIZO YA KIAFYA YA VILANOVA YAMEMUATHIRI

Mshambuliaji nyota wa Club ya Barcelona na timu ya taifa ya argentina,Lionel Messi amekiri kuwa matatizo ya kiafya ya Tito Vilanova yamekuwa pigo kubwa kwao lakini ana uhakika kuwa timu hiyo itafanikiwa kupita katika kipindi hicho kigumu cha kuondoka kwa kocha huyo. Vilanova alitangaza kujiuzulu wiki iliyopita ili aweze kuendelea na matibabu yake ya saratani na Barcelona ikamteua kocha wa zamani wa Newell Old Boys, Gerardo Martino kuchukua nafasi yake. Messi amesema wamesikitishwa kwa kilichotokea kwa Vilanova lakini kikosi chao bado kipo imara na wataendelea kusonga mbele kwa heshima yake. Messi ambaye alicheza dakika 45 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bayern Munich jana ambao walichapwa kwa mabao 2-0, amesema kwasasa yuko fiti na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua msimu uliopita yamekwisha.

HIGUAIN NA PEPE REINA WOTE WAJIUNGA NA CLUB YA NAPOILI YA ITALY

Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Argentina, Gonzalo Higuain na golikipa wa kimataifa wa Hispania Pepe Reina wanakaribia kukamilisha uhamisho wao wa kwenda Napoli baada ya kufaulu vipimo vya afya. Rais wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kimajii wa twitter kuwa wachezaji hao wawili walifaulu vipimo vyao na wanatarajiwa kujiunga na wenzao muda wowote.  
 
Higuain ambaye alikuwa akimendewa na klabu za Arsenal na Juventus, ameripotiwa kuigharimu Napoli euro milioni 37 wakati Reina yeye amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea Liverpool. Mwishoni mwa wiki iliyopita Napoli ilimuuza mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uruguay Edinson Cavani kwenda Paris Saint Germain kwa uhamisho ulioweka rekodi wa euro milioni 64.

RODGERS ADAI OFA WALITOA ARSENAL HAILINGANI NA THAMANI YA MCHEZAJI HUYO

KOCHA wa Club ya Liverpool Brendan Rodgers amedai kuwa ofa waliyotoa Arsenal hailingani na thamani aliyonayo mshambuliaji wake Luis Suarez. Liverpool imekataa ofa iliyovunja rekodi ya klabu hiyo ya paundi milioni 40 lakini Suarez anaonekana anataka kuzungumza na timu hiyo yenye maskani yake jijini London. Rodgers amesema kama Arsenal wanamtaka mchezaji huyo wanatakiwa watoe dau ambalo litalingana na thamani yake.  
Kwa maana hiyo Arsenal itatakiwa kuongeza dau zaidi baada ya ofa zake mbili kukataliwa na klabu hiyo. Suarez alionekana kwa mara ya kwanza uwanjani toka alipomng’ata mkono beki wa Chelsea Branislav Ivanovic msimu uliopita wakati alipotokea benchi katika mchezo wa kirafiki walioshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Melbourne. Suarez alijiunga na Liverpool akitokea klabu ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi mwaka 2011 kwa ada ya paundi milioni 22.7.