Mchezaji tenisi nyota
Rafael Nadal amefanikiwa kutawadhwa bingwa mpya wa michuano ya Kombe la
Rogers baada ya kugaragaza Milos Raonic wa Canada. Nadal mwenye umri wa
miaka 27 kutoka Hispania alitumia dakika 68 pekee kushinda mchezo huo
kwa 6-2 6-2 na kunyakuwa taji lake la nane kwa mwaka huu. Toka arejee
tena uwanjani Februari mwaka huu baada ya kupona majeraha, Nadal
amefanikiwa kushinda michezo 48 kati ya 51 aliyocheza na kufanikiwa
kushinda taji lake la nane katika michuano ya wazi ya Ufaransa. Kwa
upande wa wanawake mwanadada anayeshika namba moja katika orodha za
ubora Serena Williams wa Marekani naye alifanikiwa taji la michuano hiyo
kwa kumgaragaza Sorana Cirstea wa Romania. Williams mwenye umri wa
miaka 31 alihitaji dakika 65 pekee kummaliza mpinzani wake kwa 6-2 6-0
na kunyakuwa taji hilo kwa mara ya tatu.
Monday, August 12, 2013
TOURE YAYA ATWAA UCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA ASILIMIA 32%
YaYa Toure kiungo mahiri
wa kimataifa wa Ivory Coast na club ya man city ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka
wa nchi hiyo katika msimu wa 2012-2013 baada ya kupata asilimia 32 ya
kura zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo na watumiaji wa
mtandao. Toure mwenye umri wa miaka 30 anayecheza katika klabu ya
Manchester City anafuatia na mshambuliaji nyota wan chi hiyo Didier
Drogba aliyepata asilimia 24 wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Bony
Wilfried aliyepata asilimia 17. Wengine ni Aroune Kone ambaye amejiunga
na timu ya Everton akitokea Wigan mwezi uliopita pamoja na Gervino
aliyejiunga na AS Roma akitokea Arsenal ambao wote kwa pamoja wamepata
asilimia 15 ya kura zilizopigwa. Hiyo inakuwa mara ya tatu Toure
kushinda tuzo hiyo mara nyingine ikiwa mwaka 2008 na 2009.
LIVERPOOL YAIKINGIA KIFUA BARCA KUHUSU AGGER
Wakala wa beki mahiri wa club ya Liverpool, Daniel Agger amesema kuwa Liverpool imeitupilia mbali ofa iliyotumwa
na Barcelona kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo. Barcelona imekuwa
ikihusishwa na kutaka kusajili mabeki kadhaa wa Ligi Kuu nchini
Uingereza ambapo tayari walishatoa kitita cha euro milioni 25 kwa ajili
ya beki wa Chelsea David Luiz. Chelsea waliweka wazi kuwa mabingwa wa
soka nchini Hispania wanapoteza muda wao na sasa wakala wa Agger aitwaye
Per Steffensen naye amebainisha kuwa Liverpool tayari wamepiga chini
ofa hiyo. Wakala huyo amesema mteja wake bado ana mkataba wa miaka
mitatu na Liverpool hivyo ni juu ya makubaliano ya klabu hizo mbili
kuhusu ada ya uhamisho.
MAKOCHA 32 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA COPA COCA-COLA
Makocha
32 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanashiriki kozi ya Copa
Coca-Cola inayoanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam
chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa
Miguu (FIFA).
Kozi
hiyo itakayomalizika Agosti 17 mwaka huu itafunguliwa saa 3 kamili
asubuhi kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre na washiriki wote tayari
wameshawasili Dar es Salaam. Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo
kutoka Mauritius.
Washiriki
wa kozi hiyo ni Ahazi Ibrahim Kasegese (Mbeya), Aloyce Mayombo (Pwani),
Andrew Zoma (Tabora), Asuri Msakamali (Simiyu), Bakari Khamis Kilambo
(Kaskazini Pemba), Chacha Sambulo (Mara), Charles Rwezaura (Kagera),
Daniel Sambala (Njombe), Dudu Haruni (Iringa) na Emmanuel Kapurata
(Rukwa).
Faki
Makame Haji (Kaskazini Unguja), Fatawi Khamis Sheha (Kusini Pemba),
Hamisi Omary Mabo (Kigoma), Hussein Maulid (Morogoro), Issa Lugaza
(Kilimanjaro), James Gaspar (Shinyanga), James Wambura (Arusha), Jomo
Jackson Puccey (Lindi), Joseph Sihaba (Dodoma), Kelvin Haule (Ruvuma) na
Kessy Juma Abdallah (Tanga).
Kessy Mziray (Mwanza), Menswi Mchwampaka (Kinondoni), Mohamed Abdallah Kweka (Singida), Nurdin Gogola (Temeke), Pius
Kamande (Rukwa), Ramadhan Abrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Ramadhan
Salum Mnyoti (Manyara), Raphael Ngeleja (Geita), Samuel Edgar Maokola
(Ilala), Shaweji Nawanda (Mtwara) na Vuai Abdul Haji (Kusini Unguja).
Fainali za U15 Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa zitafanyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.
SEMINA YA MAKAMISHNA YAANZA DAR, MWANZA
Semina
kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness
test) kwa waamuzi
wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa
2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) katika vituo vya Dar es
Salaam na Mwanza.
Mafunzo
hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi
Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam
wakati kituo cha Mwanza kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.
Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Kituo
cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita,
Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu,
Singida na Tabora.
Kituo
cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya
Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya,
Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Friday, July 26, 2013
BAYERN VS DORTMUND JUMAMOSI
Club ya Bayern Munich na Borussia Dortmund
zinataraji kushuka dimba siku Jumamosi katika Mechi ya fungua pazi Msimu mpya kugombea
German Super Cup haya yakiwa kama Marudiano ya Fainali ya Mwezi Mei Uwanjani Wembley ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Bayern walishinda Bao 2-1 na kuweka historia ya kuwa Klabu ya kwanza Nchini Germany kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa Germany, Kombe la Germany na Ubingwa wa Ulaya.
German Super Cup haya yakiwa kama Marudiano ya Fainali ya Mwezi Mei Uwanjani Wembley ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Bayern walishinda Bao 2-1 na kuweka historia ya kuwa Klabu ya kwanza Nchini Germany kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa Germany, Kombe la Germany na Ubingwa wa Ulaya.
Hata hivyo, Dortmund wamesema wao
hawasaki kisasi pale Beki wao anaechezea Germany, Mats Hummels,
aliposema: “Hii si kisasi cha Wembley! Ni mtihani mzuri kuonyesha Msimu
huu tukoje!”
Kawaida German Super Cup hugombewa na
Bingwa na yule Mshindi wa Kombe la Germany lakini kwa vile vyote
vilichukuliwa na Bayern Msimu uliopita, Mshindi wa Pili wa Bundesliga,
ambae ni Borussia Dortmund aliemaliza Pointi 25 nyuma, ndie atacheza na
Bayern Munich.
Sura Mpya
Kila Timu, Bayern Munich na Borussia
Dortmund, zitaingia kwenye Mechi hii na sura mpya huku Bayern ikiwa na
Kocha mpya Pep Guardiola aliembadili Jupp Heynckes, Thiago Alcantara wa
Spain akiwa Bayern kutoka Barcelona na Mario Gotze akiwa pia Bayern
kutoka Dortmund.
Dortmund pia wanao wapya ambao ni Viungo
Pierre-Emerick Aubameyeng toka St Etienne na Henrikh Mkhitaryan kutoka
Shakhtar Donetsk lakini wote hawa wapya huenda wasicheze kutokana na
kuwa na maumivu.
Tayari Tiketi zote, 80,654 za
Westfalenstadion, kama ilivyo maarufu Signal Iduna Park, zimeshauzwa na
Mechi hii itatangazwa Nchi 195 Duniani.
Thursday, July 25, 2013
MESSI AKIRI KUWA MATATIZO YA KIAFYA YA VILANOVA YAMEMUATHIRI
Mshambuliaji nyota wa Club ya Barcelona na timu ya taifa ya argentina,Lionel Messi amekiri kuwa matatizo ya kiafya ya Tito
Vilanova yamekuwa pigo kubwa kwao lakini ana uhakika kuwa timu hiyo
itafanikiwa kupita katika kipindi hicho kigumu cha kuondoka kwa kocha
huyo. Vilanova
alitangaza kujiuzulu wiki iliyopita ili aweze kuendelea na matibabu yake
ya saratani na Barcelona ikamteua kocha wa zamani wa Newell Old Boys,
Gerardo Martino kuchukua nafasi yake.
Messi
amesema wamesikitishwa kwa kilichotokea kwa Vilanova lakini kikosi chao
bado kipo imara na wataendelea kusonga mbele kwa heshima yake. Messi
ambaye alicheza dakika 45 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bayern
Munich jana ambao walichapwa kwa mabao 2-0, amesema kwasasa yuko fiti na
majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua msimu uliopita yamekwisha.
Messi
amesema wamesikitishwa kwa kilichotokea kwa Vilanova lakini kikosi chao
bado kipo imara na wataendelea kusonga mbele kwa heshima yake. Messi
ambaye alicheza dakika 45 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bayern
Munich jana ambao walichapwa kwa mabao 2-0, amesema kwasasa yuko fiti na
majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua msimu uliopita yamekwisha.HIGUAIN NA PEPE REINA WOTE WAJIUNGA NA CLUB YA NAPOILI YA ITALY
Mshambuliaji nyota wa
kimataifa wa Argentina, Gonzalo Higuain na golikipa wa kimataifa wa
Hispania Pepe Reina wanakaribia kukamilisha uhamisho wao wa kwenda
Napoli baada ya kufaulu vipimo vya afya. Rais
wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis aliandika katika ukurasa wake
wa mtandao wa kimajii wa twitter kuwa wachezaji hao wawili walifaulu
vipimo vyao na wanatarajiwa kujiunga na wenzao muda wowote. 
Higuain ambaye alikuwa akimendewa na klabu za Arsenal na Juventus, ameripotiwa kuigharimu Napoli euro milioni 37 wakati Reina yeye amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea Liverpool. Mwishoni mwa wiki iliyopita Napoli ilimuuza mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uruguay Edinson Cavani kwenda Paris Saint Germain kwa uhamisho ulioweka rekodi wa euro milioni 64.
Subscribe to:
Posts (Atom)




