Malawi tayari ipo jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya mechi hiyo wakati Taifa Stars iliyopiga kambi yake
Tukuyu mkoani Mbeya inawasili jijini Dar es Salaam kesho (Mei 27 mwaka
huu) saa 4 asubuhi kwa ndege ya Air Tanzania.
Monday, May 26, 2014
TAIFA STARS, MALAWI KUONESHANA SHUGHULI DAR, KIINGILIO BUKU 5 TU!
Saturday, May 24, 2014
MBEYA CITY YAANZA VYEMA YAITANDIKA ACADEMI YA BURUNDI 3-MTUNGI
WAWAKILISHI wa Tanzania katika
michuano mipya ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea nchini Sudan ,
Mbeya City fc wameanza kutupa karata yao ya kwanza vyema hii leo majira ya
11:30 jioni kwa saa za Sudan dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Ambapo katika mchezo huo mbeya city imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 3-2 mabao hayo yakiwekwa kimiani na Paul nonga,kaptein Mwagane yeya pamoja Themi felix katika mechi hiiyo iliopigwa uwanja wa Al-Merreikh mjini Khartoum
.
TP MAZEMBE SAMATA, ULIMWENGU DHIDI YA AS VITA MJINI LUBUMBASHI
Timu hizi hasimu zitakutana katika mchezo wa kesho zikiwa na kumbukumbu ya kusababisha maafa ya vifo vya watu zaidi ya 15 katika mchezo wao wa ligi kuu ya DR Congo wiki za karibuni.
Tukio hilo baya lilitokea mjini Kinshasa baada ya mashabiki wa AS Vita kutoridhishwa na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzania wao TP Mazembe.
Mchezo wa kesho umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka, kwani timu hizi zinapokutana, upinzani unakuwabmkubwa mno nje ya uwanja na ndani ya uwanja.
FAINALI BEACH SOCCER KUTIMUA VUMBI KESSHO JUMAPILI
Fainali ya michuano ya mpira wa miguu ya ufukweni (beach soccer) kati ya timu za Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) inachezwa kesho (Mei 25 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika fainali hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Azam Tv atakuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na itaanza saa 4.15 asubuhi. Fainali hiyo itatanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya AU na TIA kuanzia saa 3 kamili asubuhi.
Michuano hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika nchini ilishirikisha vyuo 13 vya Dar es Salaam, na ilianza Aprili 20 mwaka huu katika fukwe za Escape One na Gorilla iliyopo Kigamboni.
Vyuo vingine vilivyoshiriki ni Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Vingine ni Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Utawala wa Kodi (ITA), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ).
Tanzania itashiriki katika michuano ya Afrika ya mpira wa miguu wa ufukweni itakayofanyika mwakani nchini Shelisheli
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
STARS KUPASHA MISULI NA MALAWI JUMANNE KABLA YA KWENDA ZIMBABWE
Mechi hiyoakuwa ya mwisho kwa Taifa Stars kujipima kabla ya kucheza mchezo wa marudiano wa michuano ya Afrika na Zimbabwe (Mighty Warriors) utakaofanyika Juni Mosi mwaka huu jijini Harare.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini Tukuyu mkoani Mbeya chini ya Kocha wake Mart Nooij kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi na ile ya Zimbabwe.
Na Boniface Wambura, Dar es salaamFriday, May 23, 2014
TANZANIA U15 YAANZA NA SARE DHIDI YA AYG
Tanzania imeanza Michezo ya Afrika kwa
Vijana (AYG) inayofanyika nchini Botswana kwa kutoka sare ya bao 1-1 na
Mali kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka
15 katika mechi iliyochezwa leo (Mei 22 mwaka huu).
Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa SSKB
jijini Gaborone ambapo Tanzania ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya
52 mfungaji akiwa Amani Ali. Hata hivyo, Mali walifanikiwa kusawazisha
bao hilo dakika ya 61.
Tanzania itacheza mechi yake ya pili
kesho (Mei 23 mwaka huu) kwa kuwakabili wenyeji Botswana kwenye uwanja
huo huo kuanzia saa 8 kamili mchana kwa saa za Tanzania. Mechi hizo
zinaoneshwa moja kwa moja na kituo cha SuperSport.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo,
Tanzania itacheza mechi nyingine Mei 25 mwaka huu dhidi ya Swaziland,
itakuwa tena uwanjani Mei 27 mwaka huu kuikabili Nigeria wakati mechi ya
mwisho itakuwa Mei 29 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Uongozi
wa Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa zilizoandikwa kwenye
mojawapo ya vyombo vya habari juu ya Wanachama wa Tawi la Tandale
kusema hawatambui kufutwa kwa Tawi lao ni za Ubabaishaji.
Mnamo Mei 04, 2014 Mwenyekiti wa Klabu ya Young
Africans Bw Yusuf Manji alitangaza kulifuta Tawi la Tandale kutokana na
kua chanzo cha migogoro ndani ya klabu kwa kipindi cha mrefu, ili hali
likiwa halina hadhi ya kuwa Tawi Kamili.
Ibara
ya 13, kipengele cha 2 kinasema " Kutolipa ada zake za uanachama kwa
muda wa miezi sita mfululizo bila ya sababu maalum inayokubalika na
Kamati ya Utendaji"
Baadhi ya Wanachama walijifuta
uanchama wao kutokana na kushindwa kulipia ada zao za uanachana kwa
kipindi cha zaidi ya miezi sita, kama inavyojieleza kwenye Katiba kwamba
mwanachama asipolipia ada yake zaidi ya miezi sita moja kwa moja
anajifuta uanachama wake.
Hivyo Uongozi wa klabu
ya Yanga SC unaomba Umma na Wanachama wake Duniani kote watambue kuwa
Tawi la Tandale lilifutwa kwa kutokana na kutokidhi vigezo, huku
wanachama wake wengine watano wakijifuta uanachama kwa kushindwa kulipia
ada zao kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.
Mwisho
wanachama wa klabu ya Yanga SC wanaombwa kulipia ada zao za uanchama
mapema kabla ya muda wao kumalizika ili waweze kushiriki mkutano mkuu wa
marekebisho ya Katiba utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -
Oysterbay Juni Mosi 2014.
Beno Njovu
Katibu Mkuu - Yanga SC
Mei 23, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)