Ujumbe huo wa FIFA utakaokuwa na
maofisa sita, baada ya ziara yake utashauri jinsi ya kuboresha
uendeshaji huo katika kikao cha pamoja kati yake na Kamati ya Utendaji
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kitakachofanyika mwishoni
mwa wiki ijayo.
Saturday, August 9, 2014
UJIO WA MAOFISA WA FIFA NCHINI.
Wednesday, August 6, 2014
SIMBA YA MNASA ABDI BANDA WA COASTAL UNION
CLUB ya Simba sc wazee wa Msimbazi wamefanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa
Coastal Union Abdi Banda baada ya kumuweka kwenye rada zake kwa muda mrefu.
Banda aliwahi kuripotiwa
kuwindwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili mwaka huu, lakini
ilishindikana kwasababu alikuwa na mkataba na wagosi wa kaya na viongozi wa
klabu hiyo walilalamika kitendo cha wanajangwani kumrubuni kijana huyo.
YANGA WAISHANGA CECAFA KUWEKA PEMBENI.
UONGOZI wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
Tuesday, August 5, 2014
AZAM FC YACHUKUA NAFASI YA YANGA KAGAME CUP 2014 BAADA YA YANGA SC KUSUASUA.
BARAZA la vyama vya mpira wa miguu
Afrika Mashariki na kati, CECAFA limeiengua rasmi klabu Yanga kushiri
kombe la Kagame 2014 na nafasi yake imechukuliwa na mabingwa wa ligi kuu
soka Tanzania bara, Azam fc.
Tangu awali, CECAFA walitoa
taarifa kuwa Azam watapewa nafasi ya upendeleo katika michuano hiyo
inayoanza kushika kasi Agosti 8 mwaka huu, mjini Kigali nchini Rwanda, lakini mpaka jana wana Lambalamba walikuwa hawana taarifa rasmi.
Yanga sc ndio walitakiwa kushiriki
michuano hiyo, lakini waliamua kupeleka kikosi B ambapo CECAFA
ilikikataa na kuitaka timu hiyo ya makutano ya Twiga na Jangwani,
Kariokoo jijini Dar es salaam ipeleke kikosi cha kwanza pamoja na kocha
mkuu, Mbrazil Marcio Maximo.
Lakini Baada ya Yanga sc kuenguliwa
kushiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na
kati , maarufu kama Kombe la Kagame, kwa kugoma kupelekea kikosi cha
kwanza kama walivyoagizwa, Shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema
klabu hiyo ina haki kutoshiriki mashindano kama inaona haijajiandaa.
Boniface Wambura Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Mgoyo huu mchana
huu ameumbia mtandao wa mkali dimba tz kuwa klabu inapokuwa bingwa, hakuna kanuni inayoibana
kwamba lazima ishiriki mashindo fulani, bali kama wanaona hawapo tayari
wanaweza kuwasiliana na TFF, halafu klabu nyingine inatafutwa.
MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA MAKAMU WA RAIS FIFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais
wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora.
Ameongeza kuwa Grondora alikuwa
mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia
mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo
utaendelea kukumbukwa wakati wote.
Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole
kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya FIFA na kuwataka kuwa
na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.
Monday, August 4, 2014
WASIWASI MCHEZO UMEIGHARIMU TAIFA STARS- NOOIJ
Taifa Stars iliruhusu bao la kwanza sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya makundi iliyochezwa leo (Agosti 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto hapa Maputo.
Bao hilo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 lilifungwa kwa kichwa na mshambuliaji Josemar Machaisse.
Nooij alisema wasiwasi katika kipindi cha kwanza ndio ulioipa Msumbiji fursa ya kutawala mechi hiyo katika kipindi hicho na kukimalizia ikiwa mbele kwa bao hilo la mshambuliaji huyo wa klabu ya Bravos de Maquis ya Angola.
Alisema timu yake ilitulia kipindi cha pili baada ya kumuingiza Amri Kiemba badala ya Khamis Mcha. Pia alilalamikia bao ambalo Taifa Stars ilifunga dakika ya 16 kupitia kwa John Bocco lakini likakataliwa na mwamuzi Dennis Bate kutoka Uganda.
Aliongeza kuwa mchezaji Elias Pelembe aliyeifungia Msumbiji bao la pili dakika ya 83 kwa mpira wa adhabu nje ya eneo la hatari ndiye aliyemaliza mchezo huo. Pia ni mchezaji huyo aliyebadili matokeo ya mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam ambapo Msumbiji ilisawazisha dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na ambayo ilicheza vizuri kipindi cha pili ilipata bao lake dakika ya 78 na Mbwana Samata kwa shuti la pembeni akiwa nje ya eneo la hatari na kumshinda kipa Ricardo Campos.
Matokeo hayo yameipeleka Msumbiji katika kundi C lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia. Mechi za hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco zitaanza kuchezwa mwezi ujao.
Mechi hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali itakayofanyika mwakani nchini Morocco.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.
Taifa Stars inarejea Dar es Salaam kesho (Agosti 4 mwaka huu) saa 8 mchana kwa ndege ya Air Tanzania.
Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Deogratias Munishi, Said Moradi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto, Mcha Khamis/Amri Kiemba, John Bocco/Simon Msuva, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu/Mrisho Ngasa
Tuesday, July 22, 2014
CECAFA KAGAME CUP: RATIBA HADHARANIYANGA KUANZA NA RAYON!
Ratiba ya Mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA KAGAME CUP, ambayo yatachua nafasi huko Kigali
Nchini Rwanda kuanzia Agosti 8 na kumalizika Agosti 24.
Yanga, ambao walipangwa Kundi A, wataanza kwa kuivaa Rayon Sports ya Rwanda kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali hapo Ijumaa Agosti 8.
KMKM ya Zanzibar, ambao wako Kundi moja na Yanga, wataanza kwa kuivaa Atlabara ya South Sudan Siku hiyohiyo Agosti 8 kwenye Uwanja wa Nyamirambo huko Kigali.
MAKUNDI:
KUNDI A
-Rayon Sports [Rwanda]
-Yanga [Tanzania]
-Coffee [Ethiopia]
-Atlabara [South Sudan]
-KMKM [Zanzibar]
KUNDI B
-APR FC [Rwanda]
-KCCA [Uganda]
-Flambeau de l'est [Burundi]
-Gor Mahia [Kenya]
-Telecom [Djibouti]
KUNDI C
-Vital'O [Burundi]
-El Merreikh [Sudan]
-Benadir [Somalia]
-Polisi [Rwanda]
Michezo yote zitachezwa Mjini Kigali kwenye Viwanja vya Amahoro na Nyamirambo huku Rubavu ikiwa ni Uwanja wa Akiba.
Tangu Mwaka 2002 Mdhamini wake mkuu ni Rais Paul Kagame wa Rwanda ambae amekuwa akitoa Dola 60,000 kila Mwaka.
Mashindano haya yatarushwa moja kwa moja kwenye TV na SuperSport International ambacho hivi karibuni kilisaini Mkataba wa Miaka Minne na CECAFA.
Ratiba kamili itatolewa baadae na CECAFA baada Timu zote kuthibitisha kushiriki.
Mbali ya kutwaa Kombe, Bingwa wa Kagame Cup huzoa Donge la Dola 30,000, Mshindi wa Pili Dola 20,000 na Timu ya Tatu hupata Dola 10,000.
RATIBA KAMILI:
MUDA WA KUANZA MECHI UTAAMULIWA KATI YA CECAFA, FERWAFA NA SUPERSPORT KWA AJILI YA MATANGAZO LAIVU YA TV.
KMKM ya Zanzibar, ambao wako Kundi moja na Yanga, wataanza kwa kuivaa Atlabara ya South Sudan Siku hiyohiyo Agosti 8 kwenye Uwanja wa Nyamirambo huko Kigali.
MAKUNDI:
KUNDI A
-Rayon Sports [Rwanda]
-Yanga [Tanzania]
-Coffee [Ethiopia]
-Atlabara [South Sudan]
-KMKM [Zanzibar]
KUNDI B
-APR FC [Rwanda]
-KCCA [Uganda]
-Flambeau de l'est [Burundi]
-Gor Mahia [Kenya]
-Telecom [Djibouti]
KUNDI C
-El Merreikh [Sudan]
-Benadir [Somalia]
-Polisi [Rwanda]
Michezo yote zitachezwa Mjini Kigali kwenye Viwanja vya Amahoro na Nyamirambo huku Rubavu ikiwa ni Uwanja wa Akiba.
Tangu Mwaka 2002 Mdhamini wake mkuu ni Rais Paul Kagame wa Rwanda ambae amekuwa akitoa Dola 60,000 kila Mwaka.
Mashindano haya yatarushwa moja kwa moja kwenye TV na SuperSport International ambacho hivi karibuni kilisaini Mkataba wa Miaka Minne na CECAFA.
Ratiba kamili itatolewa baadae na CECAFA baada Timu zote kuthibitisha kushiriki.
Mbali ya kutwaa Kombe, Bingwa wa Kagame Cup huzoa Donge la Dola 30,000, Mshindi wa Pili Dola 20,000 na Timu ya Tatu hupata Dola 10,000.
RATIBA KAMILI:
| TAREHE | NA | MECHI | KUNDI | UWANJA |
| Ijumaa Agosti 8 | 1 | Atlabara v KMKM | A | NYAMIRAMBO |
| 2 | Rayon v Yanga | A | AMAHORO | |
| 3 | Gor Mahia v KCCA | B | AMAHORO | |
| Jumamosi Agosti 9 | 4 | Vital ‘O’ v Banadir | C | AMAHORO |
| 5 | Police v El Mereikh | C | AMAHORO | |
| 6 | APR v Flambeau | B | AMAHORO | |
| Jumapili Agosti 10 | 7 | KMKM v Young | A | AMAHORO |
| 8 | Telecom Vs KCCA | B | NYAMIRAMBO | |
| 9 | Coffee v Rayon | A | AMAHORO | |
| Jumatatu Agosti 11 | 10 | Banadir v El Mareikh | C | NYAMIRAMBO |
| 11 | Gor Mahia v Flambeau | B | ‘’ | |
| 12 | Vital ’O’ v Police | C | ‘’ | |
| Jumanne Agosti 12 | 13 | KMKM v Coffee | A | ‘’ |
| 14 | Yanga v Atlabara | A | ‘’ | |
| Jumatano Agosti 13 | 15 | APR v Telecom | B | ‘’ |
| 16 | KCCA v Flambeau | B | ‘’ | |
| Alhamisi Agosti 14 | 17 | Coffee v Atlabara | A | |
| 18 | Rayon v KMKM | A | ||
| 19 | Police v Banadir | C | ||
| Ijumaa Agosti 15 | 20 | Flambeau v Telecom | B | |
| 21 | APR v Gor mahia | B | ||
| 22 | El Mareikh v Vital ‘O’ | C | ||
| Jumamosi Agosti 16 | 23 | Coffee v Yanga | A | |
| 24 | Rayon v Atlabara | A | ||
| Jumapili Agosti 17 | 25 | Telecom v Gormahia | B | |
| 26 | KCC v APR | B | ||
| Jumatatu Agosti 18 | MAPUMZIKO | |||
| Jumanne Agosti 19 | ROBO FAINALI | |||
| 27 | C1 v B3 | NYAMIRAMBO | ||
| 28 | A1 v B2 | ‘’ | ||
| Jumatano Agosti 20 | 29 | A2 v C2 | ‘’ | |
| 30 | B1 v A3 | ‘’ | ||
| Alhamisi Agosti 21 | MAPUMZIKO | |||
| Ijumaa Agosti 22 | NUSU FAINALI | |||
| 31 32 |
Mshindi 27 v Mshindi 28 Mshindi 29 v Mshindi 30 |
AMAHORO | ||
| Jumamosi Agosti 23 | MAPUMZIKO | |||
| Jumapili Agosti 24 | MSHINDI WA 3 & FAINALI | |||
| 33 34 |
Mfungwa 31 v Mfungwa 32 Mshindi 31 v Mshindi 32 |
AMAHORO |
Subscribe to:
Posts (Atom)