Akizungumza na mtandao huu,
Mwambusi amesema kocha Phiri ana historia ya kufundisha soka la Tanzania
kwa ngazi ya klabu wakati Maximo amefundisha timu ya Taifa, lakini wote
wataleta changamoto nzuri kwake.
Thursday, September 11, 2014
MWAMBUSI ASEMA PHIRI, MAXIMO, ASEMA NGOMA DAKIKA 90.
Wednesday, September 10, 2014
JE TUFIKA KUHUSU TAIFA STARS HII AMA NDIO MWISHO
Hakuna kitu kinawaumiza watanzania kuhusu kilio kikubwa cha wadau na wapenzi wa soka nchini Tanzania ni kuitaka serikali, TFF na vyama wanachama wake pamoja na klabu zote kuwekeza katika soka la vijana kwa manufaa ya Taifa.
Aina ya wachezaji wanaopatikana Tanzania ni wale wasiokuwa na misingi ya mpira tangu utotoni, kwasababu hakuna akademi za kisasa na hata za kawaida kwa maeneo mengi ya nchi hii, hivyo vijana wenye vipaji vya soka hujikuta hawana kwa kujiendeleza.
Soka la vijana ni muhimu na lazima Taifa kama Taifa liandae mpango mkakati wa kitaifa kwa malengo ya kuwa na falsafa ya Taifa na mfumo sahihi wa kuibua, kukuza na kulinda vipaji vya soka.
Marsh aliachishwa kazi ya kuinoa Stars sambamba na kocha Mdenish, Kim Poulsen kwa madai ya wawili hao kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa na Shirikisho la soka la Tanzania, TFF.
Hata hivyo wakati Kim anavunjiwa mkataba, Mashi alikuwa wodini akipata matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Usidhani huwa anakaa bure. Marsh ni moja ya watu wachache nchini wenye kiu ya kuona soka la nchi hii linapiga hatua.
Tangu mwaka 1991 anamiliki kituo chake cha kuibua, kulea na kukuza vipaji mkoani mwanza.
WADHAMINI WA VPL WAGAWA JEZI KWA TIMU ZA VPL KWA AJILI YA SEPT 20 VPL
Ikiwa zimebaki siku 10 kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu msimu wa 2014-2015 wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom watoa jezi kwa vilabu vyote 14 vitakavyoshiriki ligi hiyo.
Katika hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu za Ligi Kuu msimu mpya leo, Vodacom wamekabidhi jezi za rangi ya kijani na njano kwa Yanga na nyekundu na nyeupe kwa Simba, lakini muundo ni mmoja kila kitu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwakilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye alihakikisha timu zote 14 za Ligi Kuu zinapatiwa vifaa hivyo.
Timu zote 14 zilituma wawakilishi wao katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam.
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu, mabingwa watetezi, Azam FC wakifungua dimba na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC wataanza kampeni ya kutwaa tena taji hilo Septemba 21 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumapili wiki hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Yanga SC.
MAJIMAJI YAWEKA HADHARANI KIKOSI CHAKE KWA AJILI YA LIGI DARAJA LA KWANZA
ya zamani Tanzania, Majimaji FC WANALIZOMBE ya Songea mkoani Ruvuma imetaja kikosi cha wachezaji 26 iliyowasajili kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara msimu wa 2014-2015.
Ofisa Habari wa Majimaji ya Songea, Nathan Mtega ametaja kikosi cha msimu ujaoAmesema katika kikosi hicho, wachezaji 12 ni wapya ambao ni Oswald Issa, Samir Said, Emmanuel Maganga, Ally Mohamed, Kudra Omary, Said Fundikira, Mrisho Said, Idd Kipagule, Mohamed Omary, Yohana Kimburu na Msafiri Abdallah.
Amewataja wachezaji wa zamani 14 watakaoendelea kuitumikia klabu hiyo kuwa ni pamoja na Anthony Mwingira, Eliuta Ndunguru, Bahati Yussuf, Gerarrd Mbena, Abdallah Aus, Ditram Nchimbi, Filoteus Mahundi, Mpoki Mwakinyuke, Alex Zegega, Sadiq Gawaza, Odo Nombo, Frank Sekule, Marcel Boniventure na Freddy Mbuna.
Tuesday, September 9, 2014
STAND UNITED YAPATA UDHAMINI WA MWAKA MMOJA
klabu ya Stand United imeingia mkataba na Beki ya Exim Tanzania udhamini wa mwaka mmoja na inayojiandaa kushiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 unaotarajia kuanza septemba 20 mwaka huu.
Stand United yenye makao makuu yake Mkoani Shinyanga itaanza kampeniza zake nyumbani kwa kuvaana na wageni wenzao wa ligi kuu, Ndanda fc kutoka Mtwara.
Taarifa zanaeleza kuwa katika mkataba hao, Stand United watalamba milioni 10 za Kitanzania.
Huu ni udhamini wa pili kwa klabu hiyo kwani tayari walishalamba udhamini wa kampuni ya Binslum sambamba na klabu za Mbeya City na Ndanda fc ya Mtwara.
Kwa maana hiyo, Stand United watakuwa wanakusanya fedha za udhamini kutoka Binslum, Azam TV na Benk ya Exim Tanzania.
Hivi karibuni wachezaji wa Stande United waliripotiwa kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa mishahara, lakini uongozi ukafafanua kuwa kuna mahali kulitokea tatizo na fedha zipo.
Viongozi hao walikiri kufanya uzembe na walifanikiwa kumaliza tatizo.
Kwa udhamini huu, Stand United watakuwa na uwezo wa kufanya mambo ya msingi klabu kwao.
PATA UFAFANUZI WA YANGA NA EMMANUELI OKWI HUU HAPA
UTANGULIZI
Kwa niaba ya mteja wetu, Emmanuel Arnold Okwi, napenda kutoa
maelezo kuhusu Uamuzi wa kihistoria katika soka la Tanzania ambao umefanywa na
Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF. Uamuzi huo ni wa kihistoria kwa
misingi ifuatayo:
PILI: Kamati
ikiongozwa na Mwenyekiti ilitumia busara ya hali ya juu kwa kukataa ombi la
Yanga la kutengua uteuzi wa Bw. Hans Pope katika Kamati hiyo. Ikumbukwe kuwa
Yanga ilileta hoja ya kumkataa Bw. Hans Pope kwa misingi ya mgongano wa
kimaslahi na kumtaka mwenyekiti atoe uamuzi juu ya suala hilo. Endapo
mwenyekiti angetoa maamuzi ya kumuondoa Hans Pope, basi angejiingiza katika
uvunjaji wa Katiba ya TFF kwasababu yeye sio mamlaka ya uteuzi wa Hans Pope
katika Kamati hiyo. Mwenye mamlaka hayo ni Kamati ya Utendaji ya TFF. Hivyo
Yanga walipaswa kuelewa hilo na si kuishinikiza kamati, hususan Mwenyekiti,
amuondoe Hans Pope kwenye Kikao.
TATU: Maamuzi ya Kamati
yamefungua njia kwa wachezaji wengi ambao mikataba yao inachezewa na vilabu kwa
muda mrefu pasipo kuwa na nafuu yoyote ya kisheria kwa wachezaji hao ambao ndio
nguzo ya muhimu katika mpira wa Tanzania. Hata hivi sasa kuna wachezaji ambao
bado hawajalipwa stahili za mikataba yao ndani ya Yanga. Tunawaomba wajitokeze
ili tuwasaidie wapate haki zao za kisheria kama ambavyo imetokea kwa Okwi.
NNE: Pamoja na madai ya
Yanga ya kukata rufaa FIFA / CAS, naomba wajue kuwa haki yao ya kukata rufaa
inatokana na ukweli kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF
imetekeleza wajibu wake. Uamuzi huo wa Kamati umejenga msingi muhimu sana
katika suala zima la kuheshimu na kutekeleza mikakaba kwa mujibu wa kanuni za
FIFA. Endapo Yanga watakata rufaa kama wanavyodai, itakuwa ni hatua muhimu
katika kuhakikisha nguzo ya kuheshimu mikataba ya wachezaji inapewa msisitizo
unaostahili.
MGOGORO KATI YA YANGA NA OKWI
Mkataba wa Yanga na Okwi, ambao ulisainiwa tarehe 12 Disemba
2014 umekuwa na mapungufu yafuatayo:
Kamati ililiona hilo na kusema wazi kuwa hilo sio sahihi. Ni
vema wachezaji wajue kuwa hilo sio jukumu lao.
2.Pili
Yanga, kwa mujibu wa mkataba, walikuwa na haki ya kumkata mchezaji theluthi
moja ya mshahara wake wa mwezi endapo atakosa mechi tatu au zaidi. Yanga
walimkata Okwi Mishahara ya miezi mitano, kinyume na matakwa ya mkataba na
pasipo maelelzo yoyote.
3.Yanga
na Okwi walikubaliana kuwa mchezaji atalipwa ada ya kusaini mkataba (signing on
– fee) ya US$ 100,000, kwa Awamu mbili. Awamu ya kwanza wakati wa kusaini
mkataba na awamu ya pili tarehe 27 Januari 2014. Mpaka hivi sasa, Yanga
wamelipa US$ 50,000 tu na bado kuna deni la US$ 50,000. Huu ni uvunjaji wa
mkataba wa wazi kabisa.
4. Kipindi
chote mchezaji akiwa na klabu ya Yanga, hajapewa nyumba kama ambayo
walikubaliana. Huu ni ukiukwaji mwingine wa mkataba.
Baada ya Okwi kuanza kudai haki zake tajwa hapo juu, Yanga
waliamua kutomlipa mteja wetu mishahara ya miezi mitano kinyume na matakwa ya
mkataba kati yao.
MPANGO WA SIRI WA YANGA
Yanga walikuwa na mpango wa siri wa kuvunja mkataba na Emmanuel
Okwi ili wamkomoe mteja wetu, ashindwe kucheza mpira, kiwango chake kiporomoke
na itumike kama onyo kwa wachezaji wengine ambao wanadai haki zao. Mpango huu
ulitekelezw kama ifuatavyo:
b.Tarehe
25 Julai 2014, Yanga waliandika barua ya pili kukumbushia barua yao ya tarehe
27 Juni 2014. Barua hiyo ya pili haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye
upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
c.Tarehe
20 Agosti 2014 Yanga waliandika barua nyingine tena wakikumbushia hoja zao
tajwa hapo juu. Kwa mara ya tatu, barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye
ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
d. Yanga
waliandika barua nyingine ya nne tarehe 25 Agosti 2014 ikiwa na hoja zile zile
za kusitisha mkataba na mteja wetu. Kwa mara ya nne barua hiyo haikuwa na
nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
Baada ya TFF kupanga tarehe ya kikao cha Kamati ya Sheria na
hadhi ya wachezaji na kutoa barua ya wito tarehe 27 Agosti 2014 ndipo kwa mara
ya kwanza mchezaji Emmanuel Okwi akafahamu kuwa Yanga wameomba kuvunja mkataba
wake.
Tarehe 27 Agosti 2014,
Emmanuel Okwi aliiandikia Yanga KUKUBALI ombi lao la kuvunja mkataba.
Mosi, Kama Mkataba ulikuwa
ni kati ya Yanga na Okwi, ni kitu gani kiliifanya Yanga ishindwe kumpa angalau
nakala ya barua nne ambazo ilizipeleka TFF?
Pili, Wakati Yanga
wanaomba kuvunja mkataba, walikuwa wameshamlipa Okwi stahili zake kwa mujibu wa
Mkataba huo?
Tatu, Je visingizio vya
kuvunjwa kwa mkataba wa Okwi vina uhusiano na idadi ya majina ya wachezaji wa
kigeni wa Yanga?
Ni bayana kuwa Yanga walitafuta kila aina ya kisingizio ili
mteja wetu aonekane kuwa ndio amevunja mkataba wakati ni wazi kuwa Yanga ndio
waliokuwa wa kwanza kuvunja mkataba huo tarehe 27 Januari 2014 kwa kushindwa
kumlipa mteja wetu US$ 50,000 za ada ya kusaini mkataba.
HOJA MBELE YA KAMATI
Mbele ya Kamati Yanga walileta hoja kuwa: Hans Pope ana mgongano
wa maslahi kwa kuwa amemsajili Okwi Simba na yeye ni mjumbe wa Kamati hii; Okwi
amekataa kuongeza au kupunguza mkataba kama ilivyopendekezwa na Yanga; Okwi
ameleta madai yasiyo na msingi ya kutaka apewe nyumba ya kuishi; hajacheza
mechi 6 hivyo kuikosesha Yanga ubingwa. Okwi amefanya makubaliano na Klabu ya
Wadi Geldi ya Misri wakati ana mkataba na Yanga. Hivyo basi Yanga waliitaka
Kamati itamke kuwa mkataba kati yao na Okwi umesitishwa, imfungie Okwi kucheza
mpira Tanzania Maisha na ailipe Yanga dola za kimarekani laki mbili.
Baada ya Maswali toka kwa Kamati kwa pande zote mbili, Yanga
waliomba kufuta barua zao, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na kamati.
Kamati, hatimaye ilifanya maamuzi ya kihistoria katika kulinda
haki za kimkataba za wachezaji kama ambayo imeelezwa hapo juu.Kwa mtu yoyote
mwenye akili timamu, anapaswa kuipongeza kwa dhati kamati kwa maamuzi ambayo
wanajenga mpira wa nchi hii. Vilabu vinapaswa kufahamu kuwa haki za mchezaji
lazima ziheshimiwe.
Hoja za Yanga kuwa hakukuwa na madai ya fedha sio sahihi
kwasababu Majibu toka kwa Okwi na mabishano ya maneno mbele ya kamati hiyo
ilijadili kwa kina madai ya fedha ya Okwi na hata Yanga walikiri kutolipa madai
hayo. Hivyo basi si sahihi kusema kuwa eti suala la madai ya fedha
halikujadiliwa. (ona kiambatisho MNA1)
Msingi wa malalamiko ya Yanga ni barua ya tarehe 27 Juni 2014,
ambayo hakuna sehemu ambayo inatamka suala la Simba. Kama kuna kesi dhidi ya
Simba, wasubiri wakati wa kupitia pingamizi za usajili lakini suala ambalo
Yanga walilalamikia ni kusitisha mkataba na Okwi na madai ya fidia.
Kamati ya Sheria na Mwenyekiti wake hawana mamlaka ya kujadili
uteuzi au uwepo wa Hans Pope kwenye kikao hicho. Mamlaka ya Uteuzi ndio, kwa
mujibu wa katiba ya TFF, yenye uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu suala hilo.
Kwakuwa rufaa ni haki ya kila mtu, Uamuzi wa kukata rufaa Fifa /
CAS ni haki ya kisheria lakini tuwakumbushe Yanga kuwa “UKITAKA HAKI, TENDA
HAKI KWANZA”.
DK. DAMAS DANIEL NDUMBARO (PhD)
Maleta & Ndumbaro Advocates
Muwakili wa Mchezaji
Monday, September 8, 2014
KOCHA PATRIC PHIRI ASEMA KIKOSI KIPO KAMALI KWA VPL
Kocha mkuu wa timu ya soka ya Simba Patrick Phiri amesema amelizishwa na kiwango cha timu hiyo mara baada
ya kuitandika timu ya Gor mahia kutoka Kenya kwa mabao 3
kwa 0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam siku ya jumamosi.
Akizungumza na mkali wa dimba tz.blogspot.com Patrick Phiri amesema kuwa wachezaji wake wanajituma katika michezo yao na kucheza vizuri katika mechi zote anazoziongoza.
Phiri amesema wanacheza
vizuri uwanjani,uwezo umeongezeka,wamecheza na timu bora kutoka
kenya,kwa hiyo naweza kusema hiki ni kipimo sahihi kwa timu
yangu"alisema Patrick Phiri
Patrick Phiri amesema maandalizi waliyoyafanya visiwani Zanzibar kumewafanya wachezaji wake wawe vizuri na anafuraha kuona kikosi chake kimeimalika.
Subscribe to:
Posts (Atom)
