Kiungo nyota wa kimataifa wa
Mexico, Giovani Dos Santos amekamilisha usajili wake wa kujiunga na
klabu Villareal ambayo imepanda ligi msimu huu akitokea klabu ya Real
Mallorca zote za Hispania. Dos
Santos mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha
Mexico kilichonyakuwa medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki
jijini London mwaka jana, amesaini mkataba wa miaka minne na klabu
hiyo. Kiungo huyo
mshabuliaji aliibukia katika shule ya watoto ya Barcelona kabla ya
kwenda katika klabu ya Tottenham Hotspurs mwaka 2008 kwa uhamisho wa
euro milioni sita. Hata
hivyo Dos Santos alishindwa kung’aa sana katika kikosi cha kwanza na
kujikuta akipelekwa kwa mkopo katika timu ya daraja la pili ya Ipswich
Town na baadae kwenda Galatasaray ya Uturuki na Racing Santander.
