SUAREZ AJA NA MTAZAMO MPYA KUHUSU KUBAKIA LIVERPOOL
Mshambuliaji mahiri wa club ya Liverpool, Luis Suarez amebadili mawazo kuhusu mustakabali wake
na kusisitiza kuwa ameamua kubakia Anfield. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Uruguay amekuwa akitaka kuondoka Uingereza
kutokana na kuchoshwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo lakini
Liverpool walikuwa hawako tayari kumuachia nyota huyo.
Arsenal
ambao ushiriki wao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ulionyesha
kumvutia Suarez, walijitahidi kujaribu kumsajili nyota huyo mwenye umri
wa miaka 26 kwa kutoa ofa ya paundi milioni 42 ambayo ingevunja rekodi
yao ya usajili lakini walikataliwa. Akihojiwa
jijini Tokyo akiwa katika majukumu ya timu yake ya taifa, Suarez
amebainisha kuwa ameamua kubakia kwa ajili ya mashabiki wa klabu hiyo
ambao wameonyesha mapenzi makubwa kwake.