KATIKA mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon ambazo
zinazotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo tarehe 2 Machi, 2014 mjini Moshi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dk. Fenella Mukangara anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi.
Aggrey
Marealle, Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, Waratibu wa mbio hizo
alisema jana kuwa Dr. Mukangara amekubali kuwa mgeni rasmi na
atahuduria sherehe ya utoaji zawadi ambapo atatoa zawadi kwa washindi
kumi wa mbio defu za kilomita 42 maarufu kama Full Marathon kwa wanaume
na wanawake.
Dk.
Mukangara ameeleza mara kadhaa kwamba serikali inaunga mkono
Kilimanjaro Marathon kwa kutambua mchango wake michezo, utalii na
uchumi,” alisema Marealle.
Marealle ameongeza baada ya sherehe ya utoaji zawadi Waziri ataungana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na mpenda michezo Mhe. Leonidas Gama, wawakilishi wa wadhamini na watu wengine mashuhuri kwenye mlo maalum wa mchana uliodhaminiwa na Kibo Palace Hotel. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro binafsi na kupitia ofisi yake amekuwa muungaji mkono wa Kilimanjaro Marathon na amekuwa akifurahia kukaribisha maelfu ya watu wanaokuja Moshi kutoka mataifa mbalimbali.
Marealle ameongeza baada ya sherehe ya utoaji zawadi Waziri ataungana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na mpenda michezo Mhe. Leonidas Gama, wawakilishi wa wadhamini na watu wengine mashuhuri kwenye mlo maalum wa mchana uliodhaminiwa na Kibo Palace Hotel. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro binafsi na kupitia ofisi yake amekuwa muungaji mkono wa Kilimanjaro Marathon na amekuwa akifurahia kukaribisha maelfu ya watu wanaokuja Moshi kutoka mataifa mbalimbali.
John
Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo
alisema “mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia
ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za
kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume
watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni
mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu.
Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za nusu marathon (km 21) wanawake
kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja,
shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi
wa tatu.Addison aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu. Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa t-shirts baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za kuvutia kupitia droo.
Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water,Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne,