Thursday, May 8, 2014

PLUIJM ABWAGA MANYANGA YANGA SC, ATIMKIA HUKO UARABUNI

KOCHA  mkuu wa Young Africans, Mholanzi, Hans Van der Pluijm amepata kazi mpya nchini Saudi Arabia na tayari ameshaaga rasmi mchana huu kwa wachezaji wake, viongozi, wapenzi na wanachama wa klabu hiyo.
Pluijm aliyejiunga na Yanga mapema januari mwaka huu umepata shavu hilo katika klabu ya Al Shoalah FC inayoshiriki ligi kuu soka nchini Saudi Arabia.
SAM_2259Mholanzi huyo amemaliza mkataba wake wa miezi sita na klabu ya Yanga, lakini mbaya zaidi ameshindwa kuwasaidia wanajangwani kutetea ubingwa wao msimu huu uliomalizika aprili 19 mwaka huu. 
Yanga chini ya Pluijm ilimaliza katika nafasi ya pili, huku Azam fc chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog wakibeba taji lao la kwanza tangu wapande ligi kuu msimu wa 2008/2009. 
Pluijm alirithi mikoba ya mholanzi mwenzake, Ernie Brandts aliyetimuliwa mwezi desemba mwaka jana baada ya kufungwa mabao 3-1 na Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe.