Kikosi cha Taifa Stars, chini ya Kocha
mpya wa Mart Nooij leo amekiongoza kikosi chake kutoka sare ya bao
0-0 dhidi ya Malawi katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya, leo.
Nooij
raia wa Uholanzi alikipanga kikosi chake leo kikiongozwa na wachezaji wengi wazoefu kilishambulia zaidi lakini hakikuweza kupata bao kutoka na kukosa mawasiliano mazuri katika safu ya ushambuliaji.
Hata
hivyo Malawi nao walijibu mashambulizi katika kipindi cha pili lakini hawakuweza kupata bao ambapo katika mtanange huo mashabiki wengi mashabiki mbalimbali mkoani mbeya wamejitokeza kuiunga mkono stars ya Mart Nooij.