Wakala wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o anatarajiwa kuwa
nchini Uingereza wakati wa krismasi ili kuzungumzia suala la kuongeza mkataba
na klabu ya Everton.
Mkataba
aliosaini mshambuliaji huyo wakati akitua Goodison Park kama mchezaji huru
katika majira ya kiangazi una kipengele ambacho kinaruhusu mazungumzo kufanyika
pindi mechi 15 zinazpokuwa zimechezwa.
Kutoka
na umuhimu wa Eto,o katika klabu hiyo baada ya kufunga mabao manne na kusaidia
mengine mawili katika mechi 15 za mashindano yote, Everton wanaonekana kuwa
tayari na mazungumzo hayo.
Mara kadhaa kocha wa Everton, Roberto Martinez
amekiri kuwa angependa kumbakisha Eto’o mwenye umri wa miaka 33 katika kikosi
chake.
