
Timu ya Azam FC ya Tanzania imetolewa rasmi katika Michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa Bao 2-1 na FAR Rabat katika Mechi ya Marudiano iliyochezwa Uwanja wa Complexe Sportif Moulay Abdallah, Jijini Rabat Nchini Morocco.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Wiki mbili zilizopita Timu hizi zilitoka sare ya 0-0.
Nahodha wa Azam, John Bocco, ndie aliefunga bao la kwanza katika Dakika ya 6 na FAR Rabat kusawazisha kwa Penati ya Abderrahim Achakhir na kunako Dakika ya 34 Abderrahim Achakhir huyo huyo alitolewa kwa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya.
Licha ya kuwa 10 dimbani, FAR Rabat walipata Bao la pili katika Dakika ya 43 mfungaji akiwa Moustapha Allaoui.
Kipindi cha Pili, Azam FC walipata pigo pale katika Dakika ya 55 David Mwantika kupewa Kadi Nyekundu na Nyekundu nyingine kufuatia kwa Wazir Omar katika Dakika ya 74.
Hata hivyo, Azam FC walipata nafasi ya dhahabu katika Dakika ya 82 kwa kupewa Penati lakini John Bocco akakosa kufunga Bao la kusawazisha ambalo lingefanya Mechi iwe 2-2 na Azam kusonga kwa Bao za ugenini.
KIKOSI CHA AZAM:
Mwadini, Himidi, Waziri, Mwantika, Atudo, Bolou, Umony, Salum Abubakar, Bocco, Mieno, Kipre
Akiba: Aishi, Mwaipopo, Mwaikimba, Abdi Kassim, Mcha Viali, Jabir, Luckson
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Mei 3
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Al Ismaily – Egypt 0 FC Ahli Shandi – Sudan 0 [4-3]
Jumamosi Mei 4
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
FAR Rabat – Morocco 2 Azam FC– Tanzania 1 [2-1]
Union Sportive Bitam – Gabon 0 Union Sportive Médina d'Alger – Algeria 3 [0-3]
Supersport United - South Africa 1 Enppi – Egypt 3 [1-3]
Lydia LB Académi – Burundi 2 ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast 0 [2-1]
E.S. Sahel – Tunisia 6 Recreativo Da Caala - Angola 1[7-2]
Jumapili Mei 5
[Kwenye Mabano Matokeo ya Kwanza]
Wydad Athletic Club – Morocco v Liga Muculmana de Maputo – Mozambique [0-2]Diables Noirs – Congo v Club Sportif Sfaxien – Tunisia [1-3]