Saturday, April 20, 2013

WENGER AKATAAA KUFUNGUKA KUSUHU MAN U
BOSI wa Washika bunduki wa jiji la london Arsenal, mzee Arsene Wenger, amegoma kuzungumza lolote kuhusu kuipa Man United heshima wanayostahili ikiwa watatwaa Ubingwa na wakati huo huo Jumapili, Meneja wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez, atarudi tena Anfield kwa mara ya kwanza tangu atimuliwe na safari hii anaiongoza Chelsea, Timu ambayo baadhi ya Washabiki wake hawamkubali kabisa hasa kwa sababu ya uhasama wake na Chelsea alipokuwa Liverpool.

PATA HABARI KAMILI:
RATIBA- BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE:

Jumamosi Aprili 20
[Saa 11 Jioni]
Fulham v Arsenal
Norwich v Reading
QPR v Stoke
Sunderland v Everton
Swansea v Southampton
West Brom v Newcastle
West Ham v Wigan
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
WENGER NA MAN UNITED
Wakati Arsene Wenger akimsifia Straika wake Olivier Giroud kwa kuwa na Msimu mzuri wa kwanza na Arsenal, Meneja huyo aligoma kujibu hoja ya Wanahabari ya uwezekano wa Manchester United, ikiwa na Straika wake wa zamani Robin van Persie, kutua Emirates Jumapili ijayo Aprili 28 na kutwaa Taji la Ubingwa wa BPL, Barclays Premier League, Uwanjani hapo.
Upo uwezekano kwa Man United kutwaa Taji lao la 20 Jumatatu Usiku kwa kuifunga Aston Villa na katika Mechi inayofuata huko Emirates dhidi ya Arsenal, Klabu hiyo ya London itawajibika kuweka Gwaride la misitari miwili ya Wachezaji wake kabla Mechi kuanza na kuipigia makofi Timu ya Man United ikiingia Uwanjani kama Bingwa.
Kitendo hicho, huku Staa wao wa zamani Robin van Persie akiwemo Man United baada ya kuihama Arsenal mwanzoni mwa Msimu huu, bila shaka kitawakera sana Arsenal.
Wenger alikataa kuzungumzia hilo na kusema mkazo wake ni Mechi yao ya leo na Fulham na si Mechi ijayo na Man United.
Alisema: kikubwa  ni ushindi dhidi ya Fulham Jumamosi. Sioni sababu ya kuzungumzia Man United leo. Niulize tena Wiki ijayo"
MENEJA WA CHELSEA RAFAEL BENITEZ USO KWA USO NA LIVERPOOL"
BOSI wa muda wa  club ya Chelsea Rafael Benitez anategemea mapokezi mazuri kutoka kwa Mashabiki wa Liverpool wakati atakapotua Anfield kwa mara ya kwanza tangu atimuliwe huko Mwaka 2010 hapo Jumapili wakati Chelsea itakapocheza na Liverpool Mechi ya BPL.
Akiwa na Liverpool kwa Miaka 6, Benitez alimudu kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI na FA CUP.
BENITEZ NA LIVERPOOL:
Juni 2004 - Aondoka Valencia kwenda Liverpool kumbadili Gerard Houllier
Mei 2005 - Liverpool waitoa AC Milan kwa Penati, watwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mei 2006 - Liverpool waitoa West Ham kwa Penati, watwaa FA Cup
Mei 2007 - Liverpool wafungwa 2-1 na AC Milan Fainali UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mei 2009 - Liverpool wamaliza Nafasi ya 2 BPL nyuma ya Manchester United
Mei 2010 - Liverpool wamaliza Nafasi ya 7 BP –ikiwa nafasi ya chini kabisa tangu 1999
3 Juni 2010 - Benitez atimuliwa Liverpool
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KOCHA huyo ametamka: “Nina Marafiki wengi huko lakini safari hii mkazo ni Soka tu. Ni kweli nilikuwa na Liverpool kwa Miaka 6 na kutwaa Mataji mengi lakini nadhani Mashabiki wataelewa sasa ni mpinzani na wao wataishabikia Timu yao!”
Akiwa na Liverpool, Benitez aliongoza Liverpool kuifunga Chelsea kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na hatimae kutwaa Kombe Mwaka 2005 na pia kutwaa FA CUP na vilevile kuifunga tena Chelsea kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2007.
Matokeo hayo yalileta ushindani mkubwa kati ya Benitez na Chelsea na hasa Meneja wao wa wakati huo, Jose Mourinho.
Matukio hayo yamewafanya baadhi ya Mashabiki wa Chelsea kutomkubali Benitez kama Meneja wao tangu alipoteuliwa Meneja wa muda Mwezi Novemba Mwaka jana ili kumbadili Roberto Di Matteo.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
RATIBA- BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE:
Jumapili Aprili 21
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Tottenham v Man City
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v Chelsea
Jumatatu Aprili 22
[Saa 4 Usiku]
Man United v Aston Villa
MSIMAMO==BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
MAN UNITED
33
26
3
4
75
35
40
81
2
MAN CITY
32
20
8
4
58
27
31
68
3
CHELSEA
32
18
7
7
64
33
31
61
4
ARSENAL
33
17
9
7
64
35
29
60
5
TOTTENHAM
32
17
7
8
55
40
15
58
6
EVERTON
33
14
14
5
51
37
14
56
7
LIVERPOOL
33
13
11
9
59
40
19
50
8
WBA
32
13
5
14
42
43
-1
44
9
SWANSEA
32
10
11
11
43
42
1
41
10
FULHAM
33
10
10
13
44
51
-7
40
11
WEST HAM
33
10
9
14
38
47
-9
39
12
SOUTHAMPTON
33
9
11
13
47
54
-7
38
13
NEWCASTLE
33
10
6
17
42
59
-17
36
14
NORWICH
33
7
14
12
31
52
-21
35
15
SUNDERLAND
33
8
10
15
37
45
-8
34
16
STOKE CITY
33
7
13
13
28
41
-13
34
17
ASTON VILLA
33
8
10
15
36
60
-24
34
18
WIGAN
32
8
7
17
37
58
-21
31
19
QPR
33
4
12
17
29
54
-25
24
20
READING
33
5
9
19
36
63
-27
24

NANI MKALI KATI YA MESSI' VS NEYMA VS C.RONALDO