Wednesday, February 5, 2014

LOGARUSIC AFUNGUKA KUHUSU MTIBWA

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, ametanabaisha na kufunguka kuwa, anahofia kikosi chake kupata majeruhi katika kipindi hiki cha lala salama kwani watamharibia mipango yake.
 
Simba ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu kufuatia kuwa na pointi 30, nyuma ya Mbeya City yenye pointi 31, ambapo inahitaji kujipanga ili iweze kufanikiwa kusonga mbele.
Loga alisema anahofia majeruhi katika kikosi chake kwani wanaweza kusababisha kutokuwa na kikosi kizuri kwa kuwa kila mchezaji anamtumia kulingana na mfumo.
Ligi ni ngumu na hakuna timu kubwa wala ndogo katika kipindi hiki kwani kila timu imejiandaa vya kutosha, hivyo tunahitaji kujipanga pindi tunapokutana na timu yoyote.
Kwa sasa sina kikosi cha kwanza na ninatumia mchezaji kulingana na mechi kwani kuna baadhi wanajua mfumo huu na wengine wanajua mfumo mwingine, hivyo wote wapo sawa.
Wachezaji ambao ni majeruhi kwa sasa ni Said Nassoro ‘Chollo’ ambapo Donald Musoti alikuwa anasumbuliwa na malaria, pia kuna baadhi ya wachezaji wanacheza huku wakisumbuliwa na majeraha madogo-madogo.

PAWASA NA WENGINE WATEULIWA KUSAKA VIPAJI KWA AJILI YA TAIFA STAR

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeteua kikosi cha makocha 40 kutoka sshehemu mbalimbali, Tanzania Bara na Zanzibar ili kung’amua vipaji katika mpango wa kuboresha timu ya Taifa (Taifa Stars).
Makocha hao ambao watafanya kazi hiyo katika michuano maalumu ya mikoa wanatakiwa kuripoti katika ofisi za TFF siku ya Jumamosi (Februari 8 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa ajili ya kupewa maelekezo zaidi.
Walioteuliwa ni Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Ali Bushiri (Zanzibar), Ali Mayay (Dar es Salaam), Ally Mtumwa (Arusha), Ayoub Selemani (Zanzibar), Boniface Pawasa (Dar es Salaam), Dan Korosso (Mbeya), Dk. Mshindo Msolla (Dar es Salaam) na Edward Hiza (Morogoro).
Elly Mzozo (Dar es Salaam), Fred Minziro (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), Hafidh Badru (Zanzibar), Hamimu Mawazo (Mtwara), Idd Simba (Mwanza), Jabir Seleman (Zanzibar), John Tegete (Mwanza), Juma Mgunda (Tanga) na Kanali mstaafu Idd Kipingu (Dar es Salaam).
Kenny Mwaisabula (Dar es Salaam), Khalid Abeid (Dar es Salaam), Madaraka Bendera (Arusha), Madaraka Selemani (Dar es Salaam), Mbarouk Nyenga (Pwani), Mohamed Mwameja (Dar es Salaam), Musa Kissoki (Dar es Salaam), Nicholas Mihayo (Dar es Salaam), Patrick Rweyemamu (Dar es Salaam) na Peter Magomba (Singida).
Peter Mhina (Songea), Salvatory Edward (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Morogoro), Sebastian Nkoma (Dar es Salaam), Sekilojo Chambua (Dar es Salaam), Shaban Ramadhan (Zanzibar), Steven Nemes (Dar es Salaam), Sunday Manara (Dar es Salaam), Tiborowa Jonas (Dar es Salaam), Yusuf Macho (Dar es Salaam), Zamoyoni Mogela (Dar es Salaam).

OKWI ATINGA KAMBINI BAGAMOYO

Mshambuliajih hatari Emmanuel Okwi amejiunga na kambi ya Yanga mjini Bagamoyo.
Okwi ambaye usajili wake umesimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ameanza mazoezi na wenzake.

Akizungumza na mkali wa dimba Okwi amesema ameanza mazoezi na wenzake baada ya kufanya pekee kwa zaidi ya wiki.

TFF imesimamisha usajili wake kwa madai kwamba kuna kesi tatu za msingi ambazo ni Simba kuishitaki Etoile du Sahel ikitaka kulipwa dola 300,000, Okwi kuishitaki timu hiyo na yenye pia imemshitaki Fifa.
Okwi alikuwa jukwaani akiishuhudia Yanga ikivunja mwisho wa msimu kwa kuifunga Mbeya City bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.