Sunday, November 23, 2014

WENGER ALAUMU SAFU YAKE YA ULINZI DHIDI YA MAN UNITED.

Kocha wa Arsenal Arsene wenger amesema kuwa safu ya ulinzi ya Arsenal ni hafifu baada ya kushindwa 2-1 na Manchester United katika uwanja wa Emirates.
Arsenal walipatikana wakiwa wazi katika safu ya nyuma walipojaribu kutafuta bao la kukomboa baada ya Kieran Gibs kujifunga.
Wenger amesema kuwa kwa sasa safu hiyo ya ulinzi haina uzoefu wa kutosha kuweza kusoma mechi.
Katika mechi hiyo Arsenal walifanya mashambulizi 23 katika lango la Manchester United.
Wenger amesema Mwisho wa mechi hatukuwa imara katika safu ya Ulinzi na tulifanya makosa ambayo walichukua fursa na kutuadhibu.

NFA YA ZAMBIA YAMNYEMEREA PHIRI KUIONOA TIMU YA TAIFA


Shirikisho la Soka la Namibia (NFA), limeendelea kuonyesha nia ya kumpata Kocha Patrick Phiri kukinoa kikosi chake cha timu ya taifa.
Mmoja wa mtandao wa michezo wa Namibia umeandika kuwa NFA imefanya mazungumzo na Phiri kumshawishi ajiunge na kuchukua nafasi ya kocha wa sasa.
Kwa sasa, Namibia inanolewa na nyota wake wa zamani, Ricarco Manetti ambaye aliwahi kung’ara na Santos ya Afrika Kusini.
Akizungumzia hilo Phili kutoka Lusaka Zambia amekiri kwa mara nyingi kuwa aliwahi kuzungumza na uongozi wa NFA lakini si hivi karibuni.
Phiri yuko mapumzikoni kwao nchini Zambia, anatarajiwa kurejea nchini siku chache zijazo kiuendelea na kazi.

RONALDO NAE YU MBIONI KUVUNJA REKODI LA LIGA"MESSI SAFI

WAKATI Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi Jana akivunja Rekodi na kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya La Liga, Cristiano Ronaldo yuko mbioni kuivunja Rekodi ya kufunga Bao nyingi katika Msimu mmoja wa Ligi hiyo ambayo inashikiliwa na Messi.
Messi aliweka Rekodi ya Bao nyingi katika Msimu mmoja kwenye Msimu wa 2011/12 alipofunga Bao 50.
Lakini Jana Ronaldo alifunga Bao 2 wakati Timu yake Real Madrid inaichapa Eibar Bao 4-0 na sasa amefikisha Bao 20 katika Mechi 11 za La Liga Msimu huu kwa jinsi mwendo wake wa kufunga Mabao ulivyo Msimu huu Wachambuzi wanahisi Ronaldo, ambae ni Mchezaji Bora Duniani, anao uwezo wa kufunga zaidi ya Mabao 60 kwa Msimu huu.
Tayari Ronaldo, mwenye Miaka 29, ameweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza katika Historia ya La Liga kufikisha Bao 20 katika Raundi 12 za mwanzo za Ligi za Msimu huu.
Tangu ajiunge na Real kutoka Manchester United Mwaka 2009, Ronaldo amefunga Mabao 197 kwa Mechi 176 za La Liga na Messi Mabao 253 katika Mechi 289 kuanzia 2004 ambayo ndio hiyo Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya La Liga.
Lakini pia vita hii ya Rekodi za Magoli kati ya Ronaldo na Messi zitaendelea tena kati Wiki wakati Real na Barcelona zitakapojikita kwenye Mechi za 5 za Makundi yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Kwenye UCL, Messi amefunga Bao 71 sawa na Mchezaji wa zamani wa Real, Raul, na wao ndio wanaongoza Kihistoria katika Ufungaji Bora kwa Ulaya lakini Ronaldo akiwa na Bao 70 yuko nyuma kwa Bao 1.
Jumanne Barcelona wako Ugenini huko Cyprus kucheza na Apoel Nicosia na Jumatano Real nao wako Ugenini kucheza huko Uswisi na FC Basel.

LIVERPOOL HOI VIPIGO MFULULIZO WAKAA 3-1 KWA C"PALACE

Majogoo wa Jiji la Landon Liverpool wakiwa katika dimba la Ugenini huko Selhurst Park Jijini London waliongoza baada ya Sekunde 90 tu Bao la Rickie Lambert lakini walijikuta wakiambulia kipigo cha Bao 3-1 na Crystal Palace katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Palace walisawazisha Bao katika Dakika ya 17 kwa Bao la Dwight Gayle alienasa Shuti la Yannick Bolasie lililopiga Posti na kumrudia.
Kipindi cha Pili Dakika ya 78 Joe Ledley aliwapeleka Palace mbele 2-1 na kisha Dakika 3 baadae Frikiki ya Mita 25 ya Mile Jedinak ilitinga na kuwapa Palace Bao lao la 3.
Mechi hii imewaacha Wadau wa Liverpool wakihoji uchezaji wa Nahodha wao Steven Gerrard na Raheem Sterling ambao wameonyesha kufifia mno.
Kipigo hiki cha Leo kinawafanya Liverpool wawe wamechapwa Mechi 3 mfulilizo za Ligi na kushinda Mechi 1 tu kati ya 5 zilizopita na kuwaacha wakiwa Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 18 nyuma ya Vinara Chelsea.
Katika Mechi zao 2 zilizopita, Liverpool wametandikwa 2-1 na Chelsea na 1-0 na Newcastle.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Novemba 23
Crystal Palace 3 Liverpool 1        
1900 Hull City v Tottenham  
Jumatatu Novemba 24
2300 Aston Villa v Southampton 
Jumamosi Novemba 29
1545 West Brom v Arsenal
1800 Burnley v Aston Villa          
1800 Liverpool v Stoke              
1800 Man Utd v Hull                 
1800 QPR v Leicester                
1800 Swansea v Crystal Palace            
1800 West Ham v Newcastle                
2030 Sunderland v Chelsea                     
MSIMAMO:
BPL-TEBO-23NOV-A