Thursday, April 3, 2014

MADRID YAICHALAZA DORTMUND 3-0 CHELSEA YAPINGWA 3-1 NA PSG.

CLUB ya Real Madrid, ikiwa katika dimba la Uwanjan wa nyumbani wa  Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini Spain, jana  usiku wamefanikiwa kuifumua Borussia Dortmund Bao 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mchezaji Gareth Bale ndie aliefunga Bao la Kwanza katika Dakika ya 3 tu baada kuunganisha pasi safi ya Daniel Carvajal na kumzidi akili Kipa Roman Weidenfeller
Bao la Pili la Real lilifungwa katika Dakika ya 27 kupitia Isco kwa Shuti la chini toka Mita 20.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa Real 2 Dortmund 0.
Kunako Dakika ya 57, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alipiga Bao la 3 baada kumtoka Kipa Roman Weidenfeller kufuatia kupokea pasi safi ya Luka Modric.
Hilo ni Bao la 14 kwa Ronaldo kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu na ameifikia Rekodi ya Ronaldo ya Lionel Messi aliefunga Bao 14 katika Mechi 11 za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2011/12 wakati Ronaldo amechukua Mechi 8 tu.
Ronaldo hakumaliza Mechi hii baada ya kuumia na kutolewa nje katika Dakika ya 80.
Timu hizi zitarudiana huko Signal Iduna Park, Jijini Dortmund, Germany Jumanne Aprili 8.
VIKOSI:
REAL MADRID: Casillas, Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Modric, Alonso, Isco, Bale, Benzema, Ronaldo
Akiba: Diego Lopez, Varane, Casemiro, Nacho, Morata, Illarramendi, Jose Rodriguez.
BORUSSIA DORTMUND: Weidenfeller, Piszczek, Hummels, Papastathopoulos, Durm, Kehl, Sahin, Grosskreutz, Mkhitaryan, Reus, Aubameyang
Akiba: Langerak, Friedrich, Hofmann, Jojic, Kirch, Schieber, Duksch.
REFA: MARK CLATTENBURG (ENGLAND)
Katika mtanange mwingine Paris Saint-Germain, wakiikaribisha chelsea katika nyasi za  Uwanja wa nyumbaniwa Parc des Princes huko Paris, France, jana Usiku wameisasambua  Chelsea ya England Bao 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mchezaji Ezequiel Lavezzi alitangulia kuwapa PSG Bao la kuongoza katika Dakika ya 4 baada kuweka gambani Mpira uliookolewa kwa Kichwa na John Terry na kufumua Shuti moja kwa moja na kumpita Kipa Petr Cech.
Chelsea walisawazisha kwa Penati ya Dakika ya 27 iliyopigwa na Eden Hazard na ilitolewa na Refa Milorad Mazic kutoka Serbia alipoamua Sentahafu wa PSG Thiago Silva ‘kamwangusha’ Oscar.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 1-1.
PSG walifunga Bao lao la 2 baada ya Ezequiel Lavezzi kupiga Frikiki safi ambayo Kipa Petr Cech alishindwa kuzuia na kumparaza Zlatan Ibrahimovic kisha Mchezaji wa Chelsea David Luiz kuusindikiza wavuni.
Nchezaji alietoka Benchi, Javier Pastore, aliipa PSG Bao la 3 katika Dakika ya 90 baada ya kupokea Mpira wa kurushwa na kuwatoka Cesar Azpilicueta, Frank Lampard na John Terry kisha kupiga Shuti la chini chini na kumshinda Kipa Petr Cech.
Timu hizi zitarudiana huko Stamford Bridge Jumanne Aprili 8.
VIKOSI:
PSG: Sirigu, Jallet, Alex, Thiago Silva, Maxwell, Verratti, Thiago Motta, Matuidi, Cavani, Ibrahimovic, Lavezzi.
Akiba: Douchez, Cabaye, Marquinhos, Digne, Rabiot, Pastore, Lucas Moura.
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Luiz, Willian, Oscar, Hazard, Schurrle.
Akiba: Schwarzer, Lampard, Torres, Mikel, Ba, Ake, Kalas.
REFA: MILORAD MAZIC (SERBIA)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Marudiano
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Aprili 8
Chelsea v Paris Saint-Germain [1-3]
Borussia Dortmund v Real Madrid [0-3]
Jumatano Aprili 9
Bayern Munich v Manchester United [1-1]
Atletico Madrid v Barcelona [1-1]
-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili
-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
WASHINDI [Miaka ya karibu]:
MSIMU MSHINDI NCHI MSHINDI WA PILI NCHI GOLI
2012-13 Bayern Munich Germany Borussia Dortmund Germany 2-1
2011-12 Chelsea England Bayern Munich Germany 1-1 (4–3)
2010-11 Barcelona Spain Manchester United England 3-1
2009-10 Internazionale Italy Bayern Munich Germany 2-0
2008-09 Barcelona Spain Manchester United England 2-0
2007-08 Man United England Chelsea England 1-1 (6–5)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
WAFUNGAJI BORA 2013/14:
C. Ronaldo-Real Madrid Goli 14
Zlatan Ibrahimovic-PSG Goli 10 [Penati 1]
Messi-Barcelona Goli 8 [Penati 2]
Diego Costa-Atletico Madrid Goli 7
Sergio Agüero-Manchester City Goli 6 [Penati 2]