Tuesday, August 5, 2014

AZAM FC YACHUKUA NAFASI YA YANGA KAGAME CUP 2014 BAADA YA YANGA SC KUSUASUA.

BARAZA la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na kati, CECAFA limeiengua rasmi klabu Yanga kushiri kombe la Kagame 2014 na nafasi yake imechukuliwa na mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc.
Tangu awali, CECAFA walitoa taarifa kuwa Azam watapewa nafasi ya upendeleo katika michuano hiyo inayoanza kushika kasi Agosti 8 mwaka huu, mjini Kigali nchini Rwanda, lakini mpaka jana wana Lambalamba walikuwa hawana taarifa rasmi.
azam-vs-yanga
Yanga sc ndio walitakiwa kushiriki michuano hiyo, lakini waliamua kupeleka kikosi B ambapo CECAFA ilikikataa na kuitaka timu hiyo ya makutano ya Twiga na Jangwani, Kariokoo jijini Dar es salaam ipeleke kikosi cha kwanza pamoja na kocha mkuu, Mbrazil Marcio Maximo.
Lakini Baada ya Yanga sc kuenguliwa kushiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati , maarufu kama Kombe la Kagame, kwa kugoma kupelekea kikosi cha kwanza kama walivyoagizwa, Shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema klabu hiyo ina haki kutoshiriki mashindano kama inaona haijajiandaa.
Boniface Wambura Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Mgoyo huu mchana huu ameumbia mtandao wa mkali dimba tz kuwa klabu inapokuwa bingwa, hakuna kanuni inayoibana kwamba lazima ishiriki mashindo fulani, bali kama wanaona hawapo tayari wanaweza kuwasiliana na TFF, halafu klabu nyingine inatafutwa.

MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA MAKAMU WA RAIS FIFA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora.
julio1 Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).
 Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.
 Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya FIFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
 Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.