Saturday, April 26, 2014

TAIFA Star ya Tanzania,yapokea kipigo ambapo imeleta simanzi kwa wananchi kuwafanya wamalizie vibaya sherehe za miaka 50 za Muungano baada ya kufungwa mabao 3-0 na Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Stars iliyotumia wachezaji wengi chipukizi waliopatikana kwa njia ya maboresho ya timu hiyo, leo ilionekana kuzidiwa katika idara na Burundi iliyotumia wachezaji wake wazoefu.

Mshambuliaji wa Yanga SC na Nahodha wa Int’hamba Murugamba, Didier Kavumbangu alifungua pati la mabao ya Burundi dakika ya 45 akifunga kwa ustadi wa hali ya juu baada ya kumalizia pasi nzuri ya Ndarusanze Claude aliyeingia dakika ya 32 kuchukua nafasi ya Paschal Hakizimana.

Burundi walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza kwa bao hilo 1-0 na kipindi cha pili Stars ilidhoofika zaidi na kuongezwa mabao mawili ndani ya dakika nne.
Alianza mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Bara, Amisi Tambwe anayechezea Simba SC dakika ya 56 aliyefumua shuti akiwa ndani ya eneo la hatari baada ya kutengewa mpira kwa kifua na Kavumbangu kufuatia koris ya Cedric Amisi

Yussuf Ndikumana alifunga bao la tatu dakika ya 60 kwa shuti la umbali wa mita 50 baada ya kukutana na mpira akiwa katikati ya Uwanja na kumtazama kipa Deo Munishi ‘Dida’ aliyekuwa ametoka langoni mwake na kumtungua kiulaini.
Bao hilo liliamsha Stars na kutoka wote kushambulia kusaka japo bao la kufutia machozi na Simon Msuva alitengeneza nafasi tatu nzuri na zote wenzake wakashindwa kuzitumia vizuri.
Nafasi nzuri zaidi ilikuja dakika ya 85 baada ya Msuva kuteleza kulia mwa Uwanja na kuingia hadi kwenye boksi akamkatia pande safi Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye alipiga nje.
Mchezo wa leo umeonyesha Tanzania bado ina safari ndefu na ngumu kuweza kupata timu bora ya taifa.

Kikosi cha Tanzania leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Omar Kindamba/Himid Mao, Edward Peter, Aggrey Morris, Said Mourad, Said Juma/Jonas Mkude, Simon Msuva, Frank Domayo, Ayoub Lipati/Omar Nyenje, Mohamed Seif/Haroun Chanongo na Ramadhani Singano ‘Messi’.


Burundi; Arthur Arakaza/Biha Omar, Kiza Fataki, Rugonumugabo Stephane, Issa Hakizimana, Rashid Leon, Yusuf Ndikumana/Nahimana Chasil, Steve Nzigamasabo, Amisi Cedric, Didier Kavumbangu, Paschal Hakizimana/Ndarusanze Claude na Amisi Tambwe/Shaaban Hussein. 

MART NOOIJ AKABIDHIWA RASMI MIKOBA TAIFA STARS



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi Mart Nooij kutoka Uholanzi kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars).
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemtambulisha kocha huyo leo (Aprili 26 mwaka huu) kwenye mkutano na waandishiMartinus_Ignatius_Maria_maarufu_kama_Mart_Nooij wa habari uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akiwa amefuatana na Makamu wake Wallace Karia, amesema anafurahi kumtangaza Nooij na ana matarajio kuwa Tanzania itanufaika na uzoefu wake mkubwa wa ukocha, hasa katika bara la Afrika.
“Nawaahidi Watanzania kuwa sitomuingilia kocha katika kazi yake. Kama mimi sitomuingilia kocha, basi hakuna mtu yeyote atakayemuingilia. Tumemwajiri yeye kwa vile ni mtaalamu, hivyo hakuna sababu ya kumuingilia,” amesema Rais Malinzi.
Naye Nooij ambaye amepewa mkataba wa miaka miwili amesema yeye ni mtu wa maneno mafupi, hawezi kuahidi kitu lakini ana matarajio ya kuifanya Taifa Stars ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali.
Amesema kabla ya kukubalia kufundisha Taifa Stars alikuwa na klabu ya St. Georges ya Ethiopia, lakini vilevile amewahi kufundisha mpira wa miguu barani Afrika katika nchi za Burkina Faso, Mali na Msumbiji.
Wasifu wa Nooij umeambatanishwa (attached).
NGORONGORO HEROES, KENYA UWANJANI DAR
Timu ya vijana ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Kenya zinapambana kesho (Aprili 27 mwaka huu) katika mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo ya mechi hiyo ya marudiano itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ndiyo yatakayoamua ni timu ipi kati ya hizo itakayocheza raundi inayofuata katika michuano hiyo dhidi ya Nigeria.
Ngorongoro Heroes inayofundishwa na John Simkoko ilitoka suluhu na Kenya katika mechi ya kwanza iliyochezwa Machakos, Kenya wiki tatu zilizopita, na imekuwa kambini jijini Dar es Salaam kwa wiki mbili kujiwinda kwa mechi hiyo.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 na sh. 5,000 ambapo Kenya iliyowasili nchini jana (Aprili 25 mwaka huu) usiku imefanya mazoezi yake ya mwisho leo (Aprili 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa..
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi wakiongozwa na Pacifique Ndabihawenimana wakati Kamishna ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
BEACH SOCCER YAZINDULIWA RASMI
Michuano ya mpira wa miguu ya ufukweni (Beach Soccer) inazinduliwa rasmi kesho (Aprili 27 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar es Salaam na kushirikisha timu 13.
Uzinduzi huo utaanza saa 2 asubuhi. Michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini inashirikisha timu 13 kutoka vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam.
Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Ardhi (AU), Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Vingine ni Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Utawala wa Kodi (ITA) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Michuano hiyo itakuwa inachezwa Jumamosi na Jumapili kwenye fukwe za Escape One na Gorilla Beach iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.
BONIFACE WAMBURA

OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
CURRICULUM VITAE
Name:                  Mart Nooij.
First name(s):      Martinus Ignatius Maria (Mart).
Nationality:                   Dutch.
Age:                     59 years (born 03.07.1954).
Profession:                    Football Coach.
Euro – pro licence 2010 – 2011.
Teacher in Sports and Physical Education.
Coach in Burkina
Faso: From September 2001 until December 2003: National Technical Adviser of  FBF (FA), send out by KNVB (Holland FA).
Coach of the National Team U 20 (Etalons Juniors).
Participation:
The African Cup of Nations Juniors 2003 (4ième place) in Ouagadougou, Burkina Faso.
The Festival des Espoirs in Toulon (France) 2003.
The Afro-Asiatic Games in October 2003, Hyderabad, India.
The World Cup U 20 (EAU 2003) Burkina Faso reached the second round.
Coach KNVB:
KNVB- coach in the Dutch National Plan (1989 – 2001).
Responsible for coach education in the western part of the country.
KNVB- coach clinics abroad (1998 – 2005):
Seattle (USA) in July 1998 (Lake Washington Youth Soccer Ass.).
Ouagadougou (BF) in April 1999.
Maputo (Mozambique) in July 1999.
Bobo-Dioulasso (BF) in December 1999.
Preparation of National Team of Kenya (The Harambe Stars)  for
The Castle Cup in Nairobi in October 2000.
KNVB- course of the “CTR de la FBF” in Holland, May 2001.
International KNVB coach clinic in Ouagadougou for French speaking African countries in August 2003 (BF).
Willemstad, Curaçao. Dutch Antilles (February- April 2004).
Bishkek, Kyrgyzstan.  October – November 2004.
Bishkek, Kyrgyzstan July 2005.
Project manager: Manager of the project “Reinforcement of the capacity INJEPS Ouagadougou 2004 – February 2007“ send out by the Ministry of Sports in Holland.
Coach in
Mozambique:       Coach of the national team of Mozambique, February 2007 – October 2011.
Merdeka Football tournament Malaysia 2008.
4 CAN qualifiers (CAN Ghana 2008).
12 CAN and WC qualifiers (CAN + WC 2010).
CAN 2010 (Angola 2010).
COSAFA 2007/2008/2009.
Mozambique is the best mover up in FIFA ranking 2007.
6  CAN qualifiers (CAN 2012 Gabon).
All African Games 2011 Mozambique.
Coach of the National Team of Mozambique and the Olympic
Team of  Mozambique (U 23).
Contract 19/07/2010 – 31/10/2011.
Recently:             Head coach of Santos FC Cape Town South Africa
(until 31 January 2013).
At the moment:   Head coach of St George FC in Addis Ababa, Ethiopia.