Thursday, July 10, 2014

SIMBA YAMNASA HUSSEIN SHARRIF KUTOKA MTIBWA

Simba Wekundu wa Msimbazi, Simba wamekamilisha usajili wa kipa namba moja wa Mtibwa Sugar, Hussein Sharrif `Iker Casillas` na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Kwa muda mrefu Simba ilionesha nia ya kumsajili mlinda mlango huyo bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita, lakini ilimkosa mara kadhaa na sasa ndoto zimetimia.
Casillas aliyekuwa tegemeo katika klabu ya  Mtibwa Sugar ameungana na makipa Ivo Mapunda na Abuu Hashim katika kikosi cha Simba.


SERENGETI BOYZ VS AFRICA KUSINI AZAM COMPLEX

index
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boyz) inacheza mechi ya kujipima nguvu kesho (Julai 11 mwaka huu) dhidi ya Azam U-20 kwenyeUwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la Serengeti Boyz likiongozwa na kocha Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa 2 kamili asubuhi.
Serengeti Boyz itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) siku ya Ijumaa, Julai 18 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.
Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boyz ni Abdallah Shimba, Abdulrasul Bitebo, Abutwalibu Mshery, Adolf Bitegeko, Ally Mabuyu, Ally Mnasi, Amin Noren, Athanas Mdamu, Badru Othman, Baraka Baraka, Hatibu Munishi na Issa Athuman.
Wengine ni Juma Yusuf, Kelvin Faru, Kelvin Kamalamo, Martin Luseke, Mashaka Ngajilo, Mechata Mnata, Mohamed Abdallah, Mussa Vicent, Nazir Barugire, Omary Omary, Omary Wayne, Prosper Mushi, Seif Seif na Yahya Hafidh.