Thursday, March 27, 2014

TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WAKE MNYANJANI, TANGA

TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WA TANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini Tanga.
TFF_LOGO12Shughuli inayoendelea kwa sasa ni kupima udongo (soil test) na kuandaa michoro kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha michezo (Sports Complex) ukiwemo uwanja wa mpira wa miguu na majukwaa yake.
TFF imetuma maombi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuomba eneo la kujenga kituo cha michezo ikiwemo uwanja wa mipira wa miguu na majukwaa yake.
Pia Mkuu wa mkoa ameombwa kuingilia kati kuwaondoa wafanyabiashara waliovamia uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri (King George Memorial ground) mjini Moshi.
TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WA TANGATFF inawakumbusha viongozi wa vyama vya mikoa ambao hawajaomba maeneo ya kujenga vituo vya michezo vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu, waongeze jitihada za kufanya hivyo, TFF itawaunga mkono.
TFF inachukua fursa hii kuvipongeza vyama vya mpira wa miguu ambavyo ama tayari vimeshachukua hatua au viko mbioni kuchukua hatua kutafuta na kuendeleza maeneo kwa ajili ya matumizi ya mpira wa miguu.
TFF inaahidi kuunga mkono juhudi hizi na pale itakapohitajika kuongeza nguvu haitasita kufanya hivyo.
Wakati huo huo, TFF inalishukuru Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa kukubali kugharamia uwekaji nyasi za bandia kwenye Uwanja wa Kaitaba, na pia kusaidia uendelezaji wa uwanja wa TFF wa Tanga.
JAMAL MALINZI
RAIS
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

BPL-LIVERPOOL YAITUNGUA SUNDERLAND YAKWEA NAFASI YA PILI

Liverpool jana usiku imefanikiwa kuibuka na ushindi kwa Bao za Steven Gerrard na Daniel Stirridge zimewapa Liverpool ushindi wa Bao 2-1 walipocheza na Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na kuzidi kuwapa matumaini ya kuweza kutwaa Ubingwa Msimu huu.
Bao la Sunderland lilifungwa na Ki Su

WEST HAM 2 HULL CITY 1
West Ham wameizibua Hull City Bao 2-1 na kuchupa hadi Nafasi ya 11 katika Msimamo wa Ligi Kuu England.
West Ham walikuwa wa kwanza kupata Penati ya Mark Noble katika Dakika ya 26, Penati ambayo ilitolewa baada ya Kipa Allan McGregor kumwangusha Mohamed Diame na kupewa Kadi Nyekundu.
Hull City waliwasazisha katika Dakika 48 kwa Bao la Nikica Jelavic lakini ushindi ukawa kwa West Ham kwa Bao la James Chester aliejifunga mwenyewe katika Dakika ya 54. 
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA  TIMU  P  W  D  L  F  A GD PTS
1 Chelsea 31 21 6 4 62 23 39 69
2 Liverpool 31 21 5 5 84 39 45 68
3 Man City 29 21 3 5 79 27 52 66
4 Arsenal 31 19 6 6 54 35 19 63
5 Everton 30 16 9 5 46 30 16 57
6 Tottenham 31 17 5 9 40 40 0 56
7 Man United 31 15 6 10 48 37 11 51
8 Newcastle 31 14 4 13 38 43 -5 46
9 Southampton 31 12 9 10 45 40 5 45
10 Stoke 31 9 10 12 36 45 -9 37
11 West Ham 31 9 7 15 34 41 -7 34
12 Aston Villa 30 9 7 14 33 42 -9 34
13 Hull 31 9 6 16 33 39 -6 33
14 Norwich 31 8 8 15 26 48 -22 32
15 Swansea 31 7 9 15 41 47 -6 30
16 West Brom 30 5 13 12 33 45 -12 28
17 Crystal Palace 30 8 4 18 19 39 -20 28
18 Sunderland 29 6 7 16 27 45 -19 25
19 Cardiff 31 6 7 18 26 58 -32 25
20 Fulham 31 7 3 21 30 70 -40 24
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumamosi Machi 29
1545 Man Utd v Aston Villa
1800 Crystal Palace v Chelsea
1800 Southampton v Newcastle
1800 Stoke v Hull
1800 Swansea v Norwich
1800 West Brom v Cardiff
2030 Arsenal v Man City
Jumapili Machi 30
1530 Fulham v Everton
1800 Liverpool v Tottenham
Jumatatu Machi 31
2200 Sunderland v West Ham