Friday, May 10, 2013

YANGA CHATUA VISIWANI PEMBA KUJIWEKA SAWA KUFUTA KIPIGO CHA 5-0

Wanandinga wa jangwani  Yanga SC wamewasili kisiwani Pemba kuweka kambi ya kujiandaa na mtanange mkali dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC Mei 18,  katika dimba la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
wanajangwani hao watakuwa huko hadi siku moja kabla ya mechi itakaporejea  jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwa  Yanga tayari imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu, lakini imeipa uzito mkubwa mechi hiyo kwa sababu inataka kulipa kisasi cha kufungwa 5-0 na wapinzani wao hao wa jadi mwaka jana.
Tangu utawala mpya  uingia madarakani, uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Mehboob Manji umekuwa ukiumia kichwa na kipigo cha 5-0 mwaka jana.

Mara kadhaa Manji amewahi kukaririwa  akisema kwamba 5-0 zinamuumiza kichwa hasa katika wakati ambao idadi ya mabao katika mechi za timu hiyo ilipungua.
Kihistoria, Simba SC imewahi kuipa Yanga vipigo viwili vitakatifu 6-0 mwaka 1977 na 5-0 mwaka jana, wakati Yanga iliifunga SImba 5-0 mwaka 1969.  
Safari hii, Yanga imepania kuweka heshima kwa kuhakikisha inaitwangwa simba kwa  kipigo kitakatifu  na kuvunja rekodi ya 6-0 ya vipigo hivyo.


IFAHAMU KWA UNDANI ZAIDI YANGA KATIKA HARAKATI ZASOKA"

JINA KAMILI :Young  afrikani Sports Club
ILIANZISHWA : mwaka 1935
KOCHA: Ernie Brandts
LIGI: Ligi Kuu ya Tanzania bara
LIGI KUU TANZANIA:  Mara 24
1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011,2013
TANZANIA KOMBE  : Mara 4
1975, 1994, 1999, 2000.
CECAFA CLUB KOMBE / KAGAME INTERCLUB KOMBE:  Mara 5
Mwaka : 1975, 1993, 1999, 2011, 2012
UTENDAJI KATIKA MASHINDANO YA CAF   SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU AFRIKA:
CAF LIGI YA MABINGWA: KUSHIRIKI  MARA 8
1997 - Raundi ya mchujo
1998 - Hatua ya makundi
2001 - Raundi ya Pili
2006 - Raundi ya mchujo
2007 - Raundi ya Pili
2009 - Raundi ya kwanza
2010 - Raundi ya mchujo
2012 - Raundi ya mchujo
KOMBE LA MABINGWA WA KLABU: 11 KUSHIRIKI
1969 - Robo Fainali
1970 - Robo Fainali
1971 - aliondoka katika raundi ya pili
1972 - Raundi ya kwanza
1973 - Raundi ya kwanza
1975 - Raundi ya Pili
1982 - Raundi ya Pili
1984 - Raundi ya kwanza
1988 - Raundi ya kwanza
1992 - Raundi ya kwanza
1996 - Raundi ya mchujo
KOMBE LA SHIRIKISHO LA CAF: 3 KUONEKANA
2007 – Raundi ya  mzunguuko wa  kati
2008 - Raundi ya kwanza
2011 - Raundi ya mchujo
CAF KOMBE: 2 KUONEKANA
1994 - Raundi ya kwanza
1999 - Raundi ya kwanza
Kombe la CAF la washindi: 2 kuonekana
1995 - Robo Fainali
2000 - Raundi ya kwanza

KAGERA SUGAR, SHOOTING KUUMANA KAITABA VPL

Kagera Sugar inaikaribisha Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo pekee wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaofanyika kesho (Mei 11 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kaitba mjini Bukoba.

Ingawa timu zote mbili hazipambani kutafuta ubingwa ambao tayari umetwaliwa na Yanga wala kukwepa kushuka daraja, mechi hiyo bado ni muhimu kwao katika mazingira matatu tofauti.

Kagera Sugar inayonolewa na kocha mkongwe kuliko wote katika VPL, Abdallah Kibaden na ikiwa na pointi 40 yenyewe inasaka moja kati ya nafasi nne za juu ambazo zina zawadi kutoka mdhamini wa ligi, lakini pia timu zinazoshika nafasi hizo za juu zinapata tiketi ya kucheza michuano ya BancABC Super 8.

Kwa upande wa Ruvu Shooting ya Kocha Charles Boniface Mkwasa yenye pointi 31 inasaka moja ya nafasi sita za juu ambazo ni fursa ya kuingia kwenye Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) ambayo inatarajiwa kuundwa baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 28 mwaka huu.

Wagombea nafasi za uenyekiti na makamu wake ni lazima watoke katika timu zilizoshika nafasi sita la juu katika VPL msimu uliopita. Uchaguzi wa TPL Board utafanyika siku moja kabla ya ule wa TFF uliopangwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.

Raundi ya 25 ya ligi hiyo itakamilika keshokutwa (Mei 12 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Mgambo Shooting ya Tanga. Mechi hiyo namba 169 itachezwa katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Azam yenye pointi 48 inahitaji moja zaidi ili kutetea nafasi yake ya umakamu bingwa iliyoutwaa msimu wa 2011/2013 na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Wakati Azam ikisaka pointi hiyo moja, Mgambo Shooting inayofundishwa na wachezaji wa zamani wa mabingwa wa Tanzania Bara mwaka 1988, Mohamed Kampira akisaidiwa na Joseph Lazaro ni moja ya timu ziko katika hatari ya kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Mgambo Shooting inahitaji pointi moja tu katika mechi mbili ilizobakiza kukwepa kurudi FDL, ikishindwa kupata pointi hiyo huku Polisi Morogoro na Toto Africans ya Mwanza zikishinda mechi zao za mwisho kwa uwiano mzuri wa mabao itakuwa imekwenda na maji.

Mechi ya Azam dhidi ya Mgambo Shooting itachezeshwa na refa Jacob Adongo kutoka Mara, na atasaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Charles Mbilinyi wa Mwanza. Mwamuzi wa mezani atakuwa Idd Lila wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Omari Walii wa Arusha.

SIMBA, MGAMBO SHOOTING ZAINGIZA MIL 16
Mechi namba 149 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Mgambo Shooting iliyochezwa juzi (Mei 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 imeingiza sh. 16,651,000.

Watazamaji 3,006 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,226,125 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,539,983.05.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,640,402.54, tiketi sh. 3,175,000, gharama za mechi sh. 984,241.53, Kamati ya Ligi sh. 984,241.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 492,120.76 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 382,760.60.

TFF YATAKA MAELEZO YA BARUA YA FIFA KWA DAUDA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti yawww.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo.

FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)