Sunday, February 2, 2014

AZAM YAITANDIKA KAGERA, YAKAA KILELENI!

Ligi kuu Vodacom Tanzania bara imeendelea leo Jijini Dar es Salaama ambapo Mechi mbili zimepigwa zikihusisha Timu 3 za juu na Azam FC kubaki kileleni baada kuinyuka Kagera Sugara Bao 4-0 huko Azam Complez, Chamazi na Yanga kuipa kipigo cha kwanza kwenye Ligi Mbeya City na kubaki Nafasi ya Pili.
YANGA 1 MBEYA CITY 0
Goli la Dakika ya 16 la Supastraika, Mrisho Ngassa, liliwashushia Mbeya City kipigo cha kwanza kwenye Ligi na kuifanya Yanga izidi kujichimbia Nafasi ya Pili ikiwa Pointi 1 nyuma ya Azam FC.
Mbeya City, ambao walipigana kiume, walipata pigo mara tu baada Kipindi cha Pili kuanza baada ya Mchezaji wao Steven Mazanda kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
AZAM FC 4 KAGERA SUGAR 0
Huko Azam Complex, Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salamm, Wenyeji na Vinara wa VPL, Azam FC, waliendelea kukaa kileleni baada kuinyuka Kager Sugar Bao 4-0.
Bao za Azam FC zilifungwa na Brian Umony, Bao mbili, na nyingine kupitia Jabir Aziz Stima na Kevin Friday.
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano  Februari 5
Tanzania Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya)
Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga)
Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora)
JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi)


MSIMAMO:
NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
29
10
19
36
2
Young Africans
16
10
5
1
34
12
22
35
3
Mbeya City
16
8
7
1
22
13
9
31
4
Simba SC
15
8
6
1
31
13
18
30
5
Mtibwa Sugar
15
5
6
4
19
18
1
21
6
Kagera Sugar
16
5
6
5
15
15
0
21
7
Coastal Union
15
3
9
3
11
8
3
18
8
Ruvu Shootings
14
4
6
4
16
16
0
18
9
JKT Ruvu
14
6
0
8
13
18
-5
18
10
Rhino Rangers
15
2
5
8
9
18
-9
11
11
JKT Oljoro
15
2
5
8
10
15
-5
11
12
Ashanti United
15
2
4
9
13
28
-15
10
13
Tanzania Prisons
13
1
6
6
6
16
-10
9
14
Mgambo JKT
15
2
3
10
7
26
-19
9

MENEJA WA AC-MILAN SEEDORF ASEMA MILAN ITAKUWA POA TU

MENEJA wa klabu ya AC Milan, Clerence Seedorf amedai kuwa klabu hiyo inaendelea kuimarika pamoja na kupata sare ya kufungana mabao 1-1 na Torino katika mchezo wa Serie A uliofanyika jana. Katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa San Siro wageni Torino ndio walioanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Ciro Immobile lakini wenyeji walirudisha bao hilo katika kipindi cha pili kupitia kwa Adil Rami. Sare hiyo inaonekana kumfurahisha Seedorf ambaye anadai kuwa wachezaji wake wameanza kuzoea mfumo anaofundisha. Seedorf amesema ni jambo jema kuona kikosi chake kikianza kuelewana taratibu na kudai kuwa ni dalili nzuri za kufanya vyema huko mbele. Sare hiyo imeiacha Milan katika nafasi ya tisa ya Serie A, wakiwa wanajikongoja toka alipotimuliwa kocha Massimiliano Allegri Januari mwaka huu.

LIBYA WATWAA UBINGWA WA CHAN KWA MARA YA KWANZA VS GHANA

TIMU ya taifa ya Libya wametawadhwa mabingwa wapya wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, CHAN baada ya kuifunga Ghana kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo wa fainali uliochezwa katika Uwanja wa Cape Town nchini Afrika Kusini. Libya walinyakuwa taji lao hilo la kwanza la kihistoria kwa kuigaragaza Ghana kwa penati 4-3 baada ya mchezo huo kumalizika bila ya kufungana mpaka katika muda wa nyongeza. Hiyo inakuwa mechi ya tatu kwa Libya kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kuziengua Gabon na Zimbabwe katika hatua ya robo fainali na nusu fainali. Kwa wa mechi ya kutafuta mshindi wa tatu Nigeria walifanikiwa kuibuka kidedea baada ya kuifunga Zimbabwe kwa bao 1-0.

TPLB YATAKIWA KUKETI MEZANI KUTATHIMINI MECHI YA STEND UNITED VS KANEMBWA JKT

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) imeiagiza Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ifanyie marejeo (review) uamuzi wake wa kuagiza mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) irudiwe mkoani Tabora.
Maagizo hayo yametolewa na Kamati ya Utendaji iliyokutana jana (Februari 1 mwaka huu) baada ya kupokea vielelezo vipya kuhusiana na mechi hiyo iliyochezwa Novemba 22 mwaka jana mjini Shinyanga.
Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ilivunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya kupigwa na wachezaji wa Kanembwa JKT.
Pia Kamati ya Nidhamu ya TFF inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili tukio hilo la Shinyanga wakiwemo wachezaji wanane wa Kanembwa JKT waliripotiwa kumpiga mwamuzi wa mechi hiyo.

TFF,CRDB KUKETI KUTATHIMINI TIKETI ZA ELEKTRONIC

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeagiza kifanyike kikao cha dharura kati ya Sekretarieti ya TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na benki ya CRDB ili kutathimini maendeleo ya matumizi ya tiketi za elektroniki.
Lengo la kikao hicho ni kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki ni kutafuta ufumbuzi pamoja changamoto zake.
Viwanja vinane nchini vimefungwa mfumo huo wa tiketi za elektroniki. Viwanja hivyo ni Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Uwanja wa Kaitaba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Uwanja wa Mkwakwani, na CCM Kirumba.

TARIMBA MWENYEKITI WA ZAMANI WA YANGA APEWA KAMATI YA NIDHAMU TFF

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya uteuzi wa wajumbe kuunda kamati mbili za awali za haki, na kamati mbili za rufani za vyombo hivyo.
Rais wa zamani wa Yanga, Tarimba Abbas ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ataongoza Kamati ya Nidhamu. Wajumbe wanaounda kamati hiyo ni Wakili Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.
Kamati ya Rufani ya Nidhamu inaendelea kuongozwa na Profesa Mgongo Fimbo wakati makamu wake ni Wakili Hamidu Mbwezeleni. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Titus Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza Kamati ya Maadili. Wajumbe ni Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Said Mtanda.
Kamati ya Rufani ya Maadili inaundwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.