Wednesday, November 26, 2014

BARCA,MADRID,BAYERN YATAWALA ORODHA YA MABEKI FIFPRO WORD XI 2014


KLABU za Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich zimetawala orodha ya mabeki wateule katika kikosi cha dunia cha FIFPro World XI 2014 chama cha wachezaji wakulipwa, baada majina 12 ya wachezaji wao kuingia katika orodha kati ya majina 20 yaliyoteuliwa.
Wachezaji wote wanne walioshinda nafasi ya kuwemo katika kikosi hicho mwaka jana wamejumuishwa wakiwemo Dani Alves, Philipp Lahm, Sergio Ramos na Thiago Silva. Leighton Baines, Ashley Cole, Dante na Nemanja Vidic ndio ambayo hayamo katika orodha hiyo ukilinganisha na ya mwaka jana. 
Kwa upande wa Madrid wamo Dani Carvajal, Pepe, Ramos, Raphael Varane na Marcelo wakati Barcelona wamo Jordi Alba, Alves, Javier Marscherano na Gerard Pique huku Bayern wakiwa na David Alaba, Lahm na Jerome Boateng. 
Mabeki wengine wnakamilisha orodha hiyo ni pamoja na David Luiz na Thiago Silva wa Paris Saint-Germain, Pablo Zabaleta na Vincent Kompany wa Manchester City, Branislav Ivanovic na Filipe Luis wa Chelsea, Diego Godin wa Atletico Madrid na Mats Hummels wa Borussia Dortmund. 
Majina manne ya washindi wa beki bora wa dunia yataamuliwa kwa kupiga kura miongoni mwa wachezaji ambapo zaidi ya wachezaji wa kulipwa 20,000 wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo.

CAF YAZINDUA MPIRA AINA YA MARHABA KUTOKA ADIDAS KWA AJILI YA AFCON 2015


SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas wametoa mpira wa Marhaba kuwa maalumu kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta mwakani.
Mpira huo unatarajiwa kutambulishwa rasmi Desemba 3 mwaka huu katika shughuli za upangaji ratiba za michuano hiyo ambazo zitakazofanyika jijini Malabo. 
Mpira huo umebuniwa kwa rangi za aina mbalimbali ambazo zinawakilisha uwanda mpana wa bara la Afrika kuanzia jangwa la sahara, rangi ya ang’avu ya samawati katika anga la bahari ya Hindi na Atlantic. 
Mpira huo wa Marhaba umefanyiwa vipimo vyote stahiki na kuthibitishwa kuwa unaweza kutumika katika hali yeyote katika michuano hiyo.


SERIKALI YATOA SH. BILIONI 5 KIANZIO UJENZI WA JENGO LA MAABARA YA UPASUAJI.

JUMLA  ya shilingi  bilioni tano  zimetolewa  na serikali  kama kianzio cha ujenzi wa jengo la upasuaji  ujenzi wa maabara pamoja na kununua dawa katika hospitali teule ya rufaa  ya Tumbi mkoani Pwani.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Aggrey Mwanri mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu ambapo amekiri kuwa miundombinu ya hospitali hiyo haiendani na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya upanuzi wa hospitali hiyo, ambapo inakadiriwa shilingi bilioni 30 zilitumika kwa ajili ya shughuli za ujenzi huo kwa mwaka 2010.

ASKARI POLISI WILAYA CHUNYA ATIWA NGUVUNI KWA TUHUMA ZA MAUAJI.

ASKARI polisi wa kitengo cha usalama barabarani Wilayani Chunya Mkoani Mbeya, PC  Zeferin Didas Focas mwenye umri wa miaka (34) amefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuhusika na mauji ya raia Abisai Wadi mwenye miaka 22.
Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kufukwa kazi kwa askari huyo baada ya husika na mauji ya raia huyo yaliyotokea  katika Kata ya Igalula barabara ya Itindi Mkwajuni  Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Amesema,  askari huyo akiwa na mwezie aliisimamisha pikipiki iliyokuwa imempakia abiria nyuma ambapo dereva huyo alikaidi, ndipo askari huyo alichukua jiwe na kuitupia pikipiki hiyo iliyokuwa katika mwendo kasi  na kumpata abiria huyo.
Amesema, jiwe hilo linasemekana lilimkuta abiria aliyepakizwa kwenye poikipiki hiyo lakini haikuwekwa wazi kwamba jiwe hilo lilimpata katika sehemu ipi ya mwili wa marehemu huyo.

Amesema, askari huyo ambaye kwa sasa anatambulika kwa namba ya X6710 anatarajiwa kufikishwa mahakamani  ili kujibu tuhuma za mauji zinazomkabili mbele yake.