Saturday, November 1, 2014

JUMUIYA YA WAZAZI YA(CCM) MKOA WA DAR YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed amewata viongozi wa jumuia hiyo kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuifanya jumuia hiyo kukua kiuchumi.
Moto huo ameutoa wakati akizindua Daftari la Wanachama wa Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam leo.
Alisema kwa mfano katika shule ya jumuia hiyo ya Boza iliyopo mkoani Tanga kuwa ina ardhi ya kutoka lakini haifanyiwi uzarishaji mali wowote.
Mohamed alipongeza Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha daftari hilo kwani litasaidia kuwatambua wanachama wao kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa hivyo kurahisisha shughuli za kisiasa kwa kutambuana katika chaguzi mbalimbali na shughuli za maendeleo.
Katika hatua nyingine Mohamed alisema wanajumuia wote ya wazazi wanaiunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyopendekezwa na Bunge Maalumu na kuwa wao wanautaka muundo wa serikali mbili kwani ndio utalipeleka mbele Taifa la Tanzania. 
Ametoa mwito kwa wanachama wote wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao kuanzia ngazi za mashina wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni.
Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje alisema mpango wa kuanzisha daftari hilo ni moja ya mikakati yao ya kuibadilisha jumuia hiyo kiutendaji badala ya kuegemea katika eneo moja la siasa.

TANZANIA NA BURUNDI ZA SAINI MKATABA WA MIAKA 50 KUSAFIRISHA UMEME.

SERIKALI ya Tanzania na Burundi zimesaini mkataba wa miaka 50 wamakubaliano wa mradi wa pili wa kusafirisha umeme utakaozalishwa kwenye kituo cha Rusumo.
Awali Tanzania, Burundi na Rwanda zilisaini mkataba wa kwanza wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme cha rusumo chenye mega watt 80, kilichopo wilayani Ngara, Mkoani Kagera, mwaka 2013 ambacho kiligharimu takribani dola za kimarekani milioni 340 zilizotolewa na benki ya Dunia.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo, alisema mkataba huo umezihusisha nchi mbili ambapo alibainisha kuwa kupitia mradi huo ambao umeanza katika sehemu ya mwisho ya kutekeleza mradi wa kwanza ulioanza mwaka jana yapo baadhi ya maeneo nchini yatapata umeme.

Alisema kupitia mradi huo nchi itaweza kuimarisha grid ya Taifa na kupunguza tatizo la umeme kwenye maeneo mengi nchini.
Waziri Muhongo aliongeza kuwa pamoja na hatua hiyo pia kuitia mradi huo utaajiri wafanyakazi kutoka nchi zote tatu na hata wa mataifa mwengine ambapo alibainisha kuwa kwa sasa katika kituo cha mto rusumo wapo walioajiriwa kutoka nchi husika na miradi hiyo na mataifa mengine.

Kuhusu ujenzi wa mfumo wa usafirishaji umeme alisema kila nchi itajitegemea katika kusafirisha umeme na kubainisha kuwa Tanzania itajenga mfumo huo kuanzia miaka michache ijayo.

Hata hivyo Prof. Muhongo hakubainisha kiasi halisi kitakacho tumika kuendeshea mradi huo wa wamu ya pili

VPL:AZAM FC, YANGA ZAPIGWA KIMOJA, SIMBA YALE YALE.

MATOKEO:
Jumamosi Novemba 1
Kagera Sugar 0 Yanga 1
Coastal Union 1 Ruvu Shooting 0
Ndanda FC 1 Azam FC 0
Mtibwa Sugar 1 Simba 1
JKT Ruvu 1 Polisi Moro 2
Stand United 0 Prisons 1

MABINGWA wa Ligi Kuu Vodacom Azam FC Leo Wameambua kipigo cha pili mfululizo baada kuchalazwa1-0 na Ndanda FC huko Nangwanda, Mtwara.
Wikiendi iliyopita, Azam FC, wakiwa kwao Azam Complex, walichapwa 1-0 na Ruvu JKT.

Huko Kaitaba, Bukoba, Kager Sugar iliifunga Yanga Bao 1-0 kwa Bao la Paul Ngway la Dakika ya 52 na Yanga kumaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada Nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa tuhuma za kucheza vibaya.
Nao Simba wameendeleza mwendo wao ule ule wa kutoka Sare Mechi zao zote za Ligi Msimu huu baada ya kutoka 1-1 na Mtibwa Sugar huko Jamhuri, Morogoro.
Simba walitangulia kufunga Dakika ya 35 kwa Bao la Kichwa la Joseph Owino na Mchezaji wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, kuiswazishia Mtibwa kwenye Dakika ya 58.
Huko Mkwakwani, Tanga, Coastal Union waliichapa Ruvu Shooting Bao 1-0 na kuchupa hadi Nafasi ya Pili.
Ligi hii inaendelea hapo Kesho huko Mkwkwani Tanga kwa Mechi kati ya Mgambo JKT v Mbeya City.