Wednesday, April 9, 2014

RUVU SHOOTING VS AZAM YAAHIRISHWA! YANGA YAPIGA 2-1 KAGERA KWA TABU.

VPL: LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Jumatano Aprili 9
R/Shooting v Azam FC {Mechi imeahirishwa hadi alhamis aprili 10 mwaka huu}
Yanga 2 Kagera Sugar 1
MABINGWA Watetezi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara, Wanajangwani Yanga sc, wakishuka katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuibuka na ushindi ya kuinyuka Kagera Sugar Bao 2-1 na kujiwekea uimara katika mbio za kuwania ubingwa baada ya kujizatiti katika Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Azam FC ambao Leo walishindwa kucheza Mechi yao kutokana na Mvua.
Hii Leo, Azam FC walikuwa wacheze huko Mabatini, Mlandizi dhidi ya Ruvu Shooting lakini Mechi hiyo ililazimika kuahirishwa kutokana na Mvua kubwa kufanya Uwanja ufurike maji.
Huku Timu zote zikiwepo Uwanjani, Waamuzi waliukagua Uwanja wa Mabatini na kujiridhisha kuwa haufai kuchezwa na ndipo wakaamua kuahirisha Mechi hiyo.
Habari za awali zimesema kuwa Mechi hii itachezwa kesho.
Huko Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga waliifunga Kagera Sugar Bao 2-1 kwa Bao za Kipindi cha Kwanza zikifungwa na Hamisi Kiiza, Dakika ya 3, na Didier Kavumbagu, Dakika ya 34 wakati Kagera Sugar walifunga Bao lao Dakika ya 63 kupitia Daud Jumanne.
Yanga, ambao wako Pointi 1 nyuma ya Vinara Azam FC, sasa wamebakisha Mechi mbili dhidi ya JKT Oljoro, huko Arusha, na Simba wakati Azam FC wana Mechi 3 dhidi Ruvu Shooting, Mbeya City huko Mbeya na JKT Ruvu.
RATIBA:
Jumamosi Aprili 12
Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting (Manungu, Morogoro),
Coastal Union vs JKT Ruvu (Mkwakwani, Tanga),
Tanzania Prisons vs Rhino Rangers (Sokoine, Mbeya).
Jumapili Aprili 13
Mgambo Shooting vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga),
Simba vs Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
Mbeya City vs Azam (Sokoine, Mbeya)
JKT Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
GF
PTS
1
Azam FC
23
15
8
0
31
45
53
2
Yanga SC
24
15
7
2
41
58
52
3
Mbeya City
24
12
10
2
13
30
46
4
Simba SC
24
9
10
5
15
40
37
5
Kagera Sugar
24
8
10
6
2
22
34
6
Ruvu Shooting
22
9
7
6
0
27
34
7
Mtibwa Sugar
25
7
10
8
0
28
31
8
Coastal Union
24
6
11
7
-2
16
29
9
JKT Ruvu
23
8
1
14
-19
19
25
10
Mgambo Shooting
23
6
6
11
-16
16
24
11
Ashanti UTD
23
4
7
12
-20
17
19
12
JKT Oljoro
24
3
9
12
-17
17
18
13
Prisons FC
22
3
9
10
-11
17
18
14
Rhino Rangers
23
3
7
13
-17
15
16

UCL:CHELSEA YAIPAPATUA PSG 2-0 YACHUPA NUSU FAINALI.

Matokeo Marudio.
Jumanne Aprili 8
aprilChelsea 2 Paris Saint-Germain 0 [3-3, Chelsea wamesonga kwa Bao la Ugenini]
Borussia Dortmund 2 Real Madrid 0 [2-3]
CHELSEA FC 2 PARIS SAINT-GERMAIN 0
-Stamford Bridge, London
Club ya Chelsea imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL baada ya Bao la Demba Ba la Dakika ya 87 kuwapa ushindi wa Bao 2-0 katika Mechi ya Marudiano iliyochezwa Stamford Bridge na kufanya Jumla ya Mabao kuwa Bao 3-3 katika Mechi mbili na wao kutinga hatua inayofuata ya Nusu fainali kwa  Bao la Ugenini.
Bao la Kwanza la Chelsea lilifungwa na Andre Schurrle, alieingizwa kumbadili Eden Hazard alieumia, katika Dakika ya 32.
Demba Ba ambae alitokea Benchi na Bao lake la ushindi kwa Chelsea lilimfanya Meneja wao Jose Mourinho ashangilie kwa aina ya kipekee.
VIKOSI:
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Luiz, Lampard, Willian, Oscar, Hazard, Eto'o.
Akiba: Schwarzer, Cole, Kalas, Mikel, Schurrle, Ba, Torres.
PSG: Sirigu, Jallet, Alex, Silva, Maxwell, Verratti, Motta, Matuidi, Lucas, Cavani, Lavezzi.
Akiba: Douchez, Marquinhos, Digne, Van der Wiel, Cabaye, Menez, Pastore.
REFA: Pedro Proença (Portugal) 

UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Marudiano
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumatano Aprili 9
Bayern Munich v Manchester United [1-1]
Atletico Madrid v Barcelona [1-1]
DONDOO MUHIMU:
-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili
-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
WASHINDI [Miaka ya karibu]:
MSIMU MSHINDI NCHI MSHINDI WA PILI NCHI GOLI
2012-13 Bayern Munich Germany Borussia Dortmund Germany 2-1
2011-12 Chelsea England Bayern Munich Germany 1-1 (4–3)
2010-11 Barcelona Spain Manchester United England 3-1
2009-10 Internazionale Italy Bayern Munich Germany 2-0
2008-09 Barcelona Spain Manchester United England 2-0
2007-08 Man United England Chelsea
England
1-1 (6–5)