Tuesday, October 14, 2014

SIMBA KESHO KUONYESHANA KAZI NA JOMO COSMOS THN KURUDI DAR

Timu ya simba wekundu wa MSimba kesho inataraji kushuka dimba kupapatuana katika mechi yake ya mwisho ya kirafiki kesho dhidi ya Jomo Cosmos.

Mechi hiyo itapigwa jijini Johannesburg na baada ya hapo Simba itaanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi dhidi ya watani wake Yanga, Oktoba 18.
Wekundu hao tayari Simba wamecheza mechi mbili za kirafiki, dhidi ya Orlando Pirates ambayo ilitoka sare ya ya bila kufungana kabla ya kupata kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa Wits.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Kassim Dewji amewataka mashabiki wa Msimbazi kutotegemea mambo makubwa sana katika mechi yao ya Oktoba 18 dhidi ya Yanga.

Dewji ambaye yuko Johannesburg, Afrika Kusini ambako kikosi cha Simba kimeweka kambi, amesema bado kuna mambo mengi yanapaswa kubadilishwa.

KIINGILIO MECHI YA WATANI WA JADI YANGA NA SIMBA 7,000/-

Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.

KUIONA SIMBA VS YANGA KIINGILIO KINAANZIA 7000
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.


Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani Kilimanjaro.

Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi.


Magari maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia Barabara ya Mandela. Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa. Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.