Monday, April 28, 2014

KLABU AFRIKA: DROO ZA MAKUNDI KUFANYIKA KESHO

DROO za kupanga Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Kombe la Shirikisho itafanyika Jumanne Aprili 29 huko Makao Makuu ya CAF Jijini Cairo Nchini Misri.
CAF_DROO
Kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI zipo Timu 8 zilizofuzu hatua hii na Droo hiyo itapanga Makundi mawili ya Timu 4 kila moja ambayo yatacheza mtindo wa Ligi, Nyumbani na Ugenini, ili kupata Timu mbili za juu toka kila Kundi kucheza Nusu Fainali.
Timu hizo 8 ni:
-Al-Ahly Benghazi ya Libya
-Al-Hilal ya Sudan
-AS Vita Club ya Congo DR
-CS Sfaxien ya Tunisia
-Espérance de Tunis ya Tunisia
-ES Sétif ya Algeria
-TP Mazembe ya Congo DR
-Zamalek ya Egypt
Mechi za Makundi zitaanza Wikiendi ya Mei 16 hadi 18.
CAF Kombe la Shirikisho
Kwenye CAF Kombe la Shirikisho, Droo ya hapo kesho Jumanne pia itashirikisha Timu 8 ambazo nazo zitagawanywa Makundi mawili ya Timu 4 kila moja ambayo yatacheza mtindo wa Ligi, Nyumbani na Ugenini, ili kupata Timu mbili za juu toka kila Kundi kucheza Nusu Fainali.
Timu hizo 8 ni:
-Sewe Sport - Ivory Coast
-Al Ahly – Egypt
-AS Real de Bamako – Mali
-AC Leopards de Dolisie – Congo
-ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast
-Coton Sport FC – Cameroon
-E.S. Sahel – Tunisia
Mechi za Makundi zitaanza Wikiendi ya M
ei 16 hadi 18.
CAF Kombe la Shirikisho
Marudiano
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Jumamosi Aprili 26
Bayelsa United – Nigeria 0 Sewe Sport - Ivory Coast 1 [0-3]
Difaa Hassani El Jadidi – Morocco 2 Al Ahly – Egypt 1 [2-2, Al Ahly yasonga kwa Bao la Ugenini]
Jumapili Aprili 26
Djoliba AC – Mali 0 AS Real de Bamako – Mali 0 [1-2]
Medeama – Ghana 2 AC Leopards de Dolisie – Congo 0 [2-2, Penati 4-5]
ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast 1 Kaizer Chiefs - South Africa 0 [3-1]
Petro Atlético de Luanda - Angola 2 Coton Sport FC – Cameroon 2 [3-4]
E.S. Sahel – Tunisia 1 Horoya Athlétique Club – Guinea 0 [1-0]
C. A. Bizertin – Tunisia 1 Nkana FC – Zamba 1 [1-1]

BRENDAN RODGRERS ASEMA CHELSEA WALIPAKI MABASI 2 GOLINI.

Wakati Jose Mourinho akijisifia kwamba timu bora imeshinda, kocha wa Liverpool Brendan Rodgers akiongea na waandishi wa habari ameipaka timu ya Chelsea kwa aina ya uchezaji wao.
morhoChelsea wamepunguza kasi za Liverpool kushinda taji la ubingwa wa EPL baada ya miaka mingi kwa kuwafunga magoli 2 bila huku wakililinda goli lao kwa idadi kubwa ya wachezaji wakiwa ndani ya 18.
Kocha wa Liverpool amesema Chelsea walipaki mabasi mawili golini kwao na ilikuwa ni vigumu kwa wao kupita kujaribu kupata goli.
Licha ya ushindi huo mashabiki wengi wa soka kwenye mtandao wa goal.com wakati post hii inawekwa wameipa nafasi kubwa Manchester city(44.4%) kuchukua taji hilo. Kura hizo zimeipa Liverpool(41%) nafasi ya pili na kumaliza na Chelsea(14.6%).

PFA-LUIS SUAREZ TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA:

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ametwaa Tuzo ya England ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya PFA [Professional Footballers' Association], Chama cha Wanasoka wa Kulipwa, hapo Jana.
Msimu uliopita, kipindi kama hiki, Luis Suarez alikuwa akianza kutumikia Adhabu ya Kifungo cha Mechi 10 baada kumuuma Meno Mchezaji wa Chelsea, Branislav Ivanovic, lakini safari hii ni kidedea.
Suarez alikabidhiwa Tuzo yake Jana Usiku kwenye Hoteli ya Kifahari, Grosvenor House, Jijini London mara baada ya kuruka kutoka Jijini Liverpool baada ya Mechi yao Uwanjani kwao Anfield walikofungwa Bao 2-0 na Chelsea.
Msimu huu, Suarez amefunga Bao 30 katika Mechi 31 za Ligi licha ya k
uzikosa Mechi za mwanzo wa Msimu akiwa bado Kifungoni.
Mchezaji wa Chelsea, Eden Hazard, ambae hakucheza hiy
o Jana huko Anfield, alitwaa Tuzo ya England ya Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka ya PFA.
Kwenye Timu Bora ya Mwaka ya PFA ya Ligi Kuu England, Suarez alijumuika na wenzake wa Liverpool, Daniel Sturridge na Nahodha wao Steven Gerrard.
Chelsea pia walikuwa na Wachezaji watatu ambao ni Petr Cech, Gary Cahill na Hazard.
Manchester City inawakilishwa na Vincent Kompany na Yaya Toure huku Southampton ikiwa na wawili, Luke Shaw na Adam Lallana.
Mabingwa Watetezi, Manchester United nar Arsenal, haina hata Mchezaji mmoja.
PFA-LIGI KUU ENGLAND-TIMU YA MWAKA: Petr Cech (Chelsea); Luke Shaw (Southampton), Vincent Kompany (Manchester City), Gary Cahill (Chelsea), Seamus Coleman (Everton); Eden Hazard (Chelsea), Yaya Toure (Manchester City), Steven Gerrard (Liverpool), Adam Lallana (Southampton); Luis Suarez (Liverpool), Daniel Sturridge (Liverpool)

WANASOKA BORA WA MWAKA ENGLAND

Mchezaji Bora wa Mwaka: Luis Suarez (Liverpool).
Mchezaji Bora Chipukizi wa mwaka: Eden Hazard (Chelsea).
Mchezaji Bora wa kike wa Mwaka: Lucy Bronze (Liverpool Ladies).
Mchezaji Bora chipukizi wanawake: Martha Harris (Liverpool Ladies).