Wednesday, July 16, 2014

CHELSEA YAMNASA MBADALA WA COLE KUTOKA ATLETICO.

KLABU ya Atletico Madrid imetangaza kuwa imefikia makubaliano na Chelsea kuhusu uhamisho wa Filipe Luis. Chelsea kwa kipindi kirefu amekuwa wakihusishwa na kutaka kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 huku mwezi Juni wakiipa taarifa Atletico kuwa wako tayari kutoa paundi milioni 20 zilizowekwa katika mkataba wake. Atletico wamethibitisha rasmi kuwa wameshakubaliano juu ya uhamisho huo na kilichobakia ni mchezaji huyo kufanyiwa vipimo vya afya na Chelsea. Luis anatarajiwa kuziba nafasi ya Ashley Cole aliyeruhusiwa kuondoka kwenda Roma kama mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake. Beki huyo wa kushoto atajiunga na mchezaji mwenzake Diego Costa ambaye naye alikamilisha usajili wake kutoka Atletico uliogharimu kiasi cha paundi milioni 35 mapema wiki hii. Luis anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Chelsea katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya kusajiliwa kwa Costa, Cesc Fabregas na kiungo chipukizi Mario Pasalic.



NBA: DENG AENDA KUZIBA PENGO LA LEBRON JAMES.

MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu kutoka nchini Uingereza, Luol Deng amejiunga na timu ya Miami Heat kama mchezaji huru. Deng ambaye amezichezea timu za Cleveland Cavaliers na Chicago Bulls msimu
uliopita anatarajiwa kuchukua nafasi ya LeBron James ambaye amehamia Cavaliers wiki iliyopita. Rais wa Heat, Pat Riley amesema Deng ni mmoja ya mchezaji muhimu waliomsajili katika historia ya timu hiyo. Deng ambaye ni mzaliwa wa Sudan aliiwakilisha Bulls kutoka mwaka 2004 mpaka 2014 na mara mbili amefanikiwa kuchaguliwa katika kikosi cha wachezaji nyota wa mchezo huo nchini Marekani, aliuzwa Cavaliers Januari mwaka huu. Heat wamefanikiwa kutinga fainali nne zilizopita za Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani-NBA ambapo walishinda mwaka 2012 na 2013 lakini walichapwa na San Antonio Spurs msimu uliopita.

GARETH BALE LEO ATIMIZA MIAKA 25 AKIWA NDANI YA REAL MADRID


 
Gareth Bale
 


Kuhusu yeye binafsi
Full name

Gareth Frank Bale
Date of birth
16 July 1989 (age 25)
Place of birth
Cardiff, Wales
Height
1.83 m (6 ft 0 in)
Playing position
Timu ya sasa
Current team
Number
11
Timu za Vijana
2005–2006
Timu za ukubwa
Years
Team
  Mechi
(Goli)
2006–2007
40
(5)
2007–2013
146
(42)
2013–
27
(15)
Timu ya Taifa
2005–2006
7
(1)
2006
1
(1)
2006–2008
4
(2)
2006–
44
(12)

AFRIKA KUSINI YAWASILI KUIVAA SERENGETI BOYS


tff_LOGO1Afrika Kusini (Amajimbos) imewasili nchini kuikabili Tanzania (Serengeti Boys) katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 itakayochezwa keshokutwa (Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo yenye msafara wa watu 37 ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku (Julai 15 mwaka huu) na imefikia hoteli ya Sapphire. Amajimbos itafanya mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo kutoka Shelisheli wakiongozwa na Allister Barra tayari wamewasili nchini. Kamishna wa mechi hiyo ni Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.
Makocha wa timu za Seregenti Boys na Amajimbos pamoja na manahodha wao watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000. Tiketi zitauzwa uwanjani katika magari maalumu siku ya mechi.
SAMATA, ULIMWENGU WATUA, MWINYI KAZIMOTO KESHO
Washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wamewasili nchini leo asubuhi (Julai 16 mwaka huu) kutoka Tunisia kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao wamefikia hoteli ya Courtyard, Seaview Upanga na leo (Julai 16 mwaka huu) watafanya mazoezi kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij wakati wakiwasubiri wenzao.
IMG_0750Naye kiungo Mwinyi Kazimoto anayecheza mpira wa miguu katika klabu ya Almarhiya ya Qatar atawasili nchini kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili Dar es Salaam kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 3.20 asubuhi kwa ndege ya Fastjet kutoka Mbeya tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Msumbiji.

RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari Ijumaa (Julai 18 mwaka huu).