Thursday, August 21, 2014

YANGA YAITUNGUA 1-0 CHIPUKIZI YA ZANZIBAR KATIKA MECHI YA KIRAFIKI

DSC_0018Club ya yanga imefanikiwa kuitandika bao 1-0 dhidi ya Chipukizi FC ya Zanzibar katika mchezo wa kwanza wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Mbrazil, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ katika dakika ya 6 ya mchezo.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa kocha wa Yanga,  Mbrazil, Marcio Maximo kuwaona wachezaji wake wakicheza mechi ya kirafiki.
Ili kuhakikisha anawaona wachezaji wote, Maximo alitumia vikosi viwili tofauti kwa kila kipindi.