Thursday, June 5, 2014

UBORA DUNIANI: SPAIN BADO 1, GERMANY 2, BRAZIL SASA 3, STARS YAKWEA HADI 113

Timu ya Taifa ya Brazil,ambao ni Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia wamepanda juu nafasi 1 na sasa wako Nafasi ya 3 katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo huku Mabingwa wa Dunia Spain wakibakia Nafasi ya 1, wakifuata Germany na Tanzania ikipanda Nafasi 9 na kukamata Nafasi ya 113.
England imerudi 10 Bora kwa kuishusha Greece wakati Argentina imepanda Nafasi 2 na ipo ya 5 na Uswisi ikoya 6 baada kupanda Nafasi 2.
Kwa Afrika, Timu ya juu kabisa ni Algeria iliyo Nafasi ya 22 baada kupanda Nafasi 3 na kuipiku Ivory Coast ambayo iko ya 23 baada kushuka Nafasi 2.
BRAZIL_SAMBA25 BORA:
1        Spain [Iko pale pale]
2        Germany [Iko pale pale]
3        Brazil [Imepanda Nafasi 1]
4        Portugal [Imeshuka Nafasi 1]
5        Argentina [Imepanda Nafasi 2]
6        Switzerland  [Imepanda Nafasi 2]
7        Uruguay [Imeshuka Nafasi 1]
8        Colombia [Imeshuka Nafasi 3]
9        Italy  [Iko pale pale]
10      England [Imepanda Nafasi 1]
11      Belgium [Imepanda Nafasi 1]
12      Greece [Imeshuka Nafasi 2]
13      USA   [Imepanda Nafasi 1]
14      Chile  [Imeshuka Nafasi 1]
15      Netherlands [Iko pale pale]
16      Ukraine[Imepanda Nafasi 1]
17      France [Imeshuka Nafasi 1]
18      Croatia [Imepanda Nafasi 2]
19      Russia [Imeshuka Nafasi 1]
20      Mexico [Imeshuka Nafasi 1]
21      Bosnia and Herzegovina [Imepanda Nafasi 4]
22      Algeria [Imepanda Nafasi 3]
23      Denmark [Iko pale pale]
23      Côte d'Ivoire [Imeshuka Nafasi 2]
25      Slovenia [Imepanda Nafasi 4]
TANZANIA-NAFASI ILIPO:
108    Kenya
109    Latvia
110    Bahrain
110    Canada
112    Niger
113    Tanzania [Imepanda Nafasi 9]
114    Namibia
115    Kuwait
116    Liberia
116    Rwanda

CECAFA NILE BASIN CUP: VICTORIA UNIVERSITY BINGWA, WAULA DOLA 30,000!!


UNI2
UNI1VICTORIA UNIVERSITY wamefanikiwa kuwa Mabingwa wa Mashindano mapya ya CECAFA NILE BASIN CUP baada kuichapa AFC Leopards ya Kenya Bao 2-1 katika Fainali iliyochezwa huko Khartoum International Stadium Jijini Khartoum Nchini Sudan hapo Jana.
Haya ni Mashindano ya kwanza kabisa ya Kombe hilo yaliyoshindaniwa na Klabu kadhaa toka Nchi za Afrika Mashariki na ya Kati ambao ni Wanachama wa CECAFA.
Kwa ushindi huo, Victoria University pia wamejinyakulia Donge nono la Dola 30,000 na ni baraka kwa Klabu changa iliyoshiriki michuano ya CECAFA kwa mara ya kwanza kabisa.
Victoria University ndio waliowatoa Wawakilishi wa Tanzania Bara, Mbeya City, kwenye Robo Fainali baada ya kuwafunga Bao 1-0 kwa Bao la Penati.
UNI3Kwa kuwa Washindi wa Pili, AFC Leopards walipewa Dola 20,000.
MAGOLI:
Victoria University 2
-Odongo Mathew Dakika ya 29
-Mutyaba Muzamir 90+2
AFC Leopards 1
-Ikene Austin Dakika ya 45

Nao, Timu ya Sudan, Al Shandy, ilinyakua Dola 10,000 kwa kumaliza Washindi wa Tatu baada ya kuifunga Academie Tchite ya Burundi Bao 4-1.
Klabu zilizoshiriki muchuano hii ni:
KUNDI A
-Polisi [Zanzibar]
-Victoria University Uganda]
-Malakia [South Sudan]
Al Merreikh [Sdan]
KUNDI B
-Mbeya City [Tanzania Bara]
-AFC Leopards [Kenya]
-Academie Tchite [Burundi]
-Enticelles [Rwanda]
KUNDI C
-Defence [Ethiopia]
-Dkhill FC [Djibouti]
-Al Shandy [Sudan]

TAIFA STARS: 28 WAITWA KUPIGA KAMBI YA SIKU 3 KUANZIA JUNI 11

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea taarifa za kutolewa wito bungeni wa kulitaka litumie tiketi za elektroniki katika kukusanya mapato.
Tunataka ieleweke wazi kwa umma wa Watanzania kuwa si nia yetu kuchelewesha matumizi ya uingiaji mpirani kwa tiketi za elektroniki. Ieleweke kuwa mfumo wa kuingia kwenye mbuga, KCMC, mipakani ni tofauti na uingiaji mpirani.
Katika mpira wa miguu wanaingia maelfu ya watu katika kipindi kifupi. Kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda usalama wa watazamaji na miundombinu ya viwanja ndio maana tulisitisha matumizi ya tiketi za elektroniki hadi tujihakikishie usalama wa matumizi yake.
Tunafanya jitihada kwa karibu na mzabuni benki ya CRDB ili kuhakikisha mfumo huu unaanza kutumika mara moja.
Kwa niaba ya sekta ya michezo tunatoa wito kwa Serikali kushusha au kuondoa kodi kubwa zinazotozwa kwenye vifaa vya michezo, hasa vinavyotumiwa na watoto kuanzia umri wa miaka 6-12, ili watoto wetu waweze kuvipata kirahisi toka kwa wazazi wao ili waweze kujifunza kucheza michezo kisasa tangu wakiwa wadogo.
TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI JUNI 11
Kikosi cha Taifa Stars kinaingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)