Saturday, June 7, 2014

MASHABIKI WA YANGA MBEYA WAUTAKA UONGOZI WA YANGA KUMUELEZA MAXIMO KUZIBA PENGO LA KAVUMBAGU

Mashabiki na wadau wa soka mkoani mbeya wameutaka Uongozi wa Yanga sc kuhusu wameutaka uongozi huo kupendekeza kumweleza kocha mpya anayetarajiwa kuja kuinoa yanga kocha Marcio Maximo kumpata mshambuliaji mahiri wa kuziba nafasi ya Didier Kavumbagu, kabla ya kuanza kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi ya Tanzania Bara.

Wakizungumza na mtandano wa mkali wa dimba kupitia sayari ya michezo wames
ema kuwa kutokana habari zilizo tolewa katika Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
katika kikao cha wanachama wa club ya yanga kilicho fanyika Juni 1 mwaka huu uongozi wa yanga Ulimtangaza kuwa Maximo kama kocha anayetarajiwa kuinoa Yanga.

Wamesema kuwa Maximo anatakiwa kutazama mchezaji sahihi atakae ziba pengo la mshambuliaji Didier Kavumbagu kwa ajili ya kuunda upya timu hiyo licha ya kuwa na Wachezaji wengi katika safu ya Ushambuliaji.
 Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kutoka ndani ya yanga Taarifa zinasema mazungumzo na Kocha Maximo yamefikia sehemu nzuri kwa ajili ya kuja Tanzania kuinoa Yanga SC.

TFF YATOA RAMBIRAMBI MISIBA YA KANALI MWANAKATWE NA GEBO PETER!

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wake (wakati huo ikiitwa FAT), Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe kilichotokea leo asubuhi (Juni 7 mwaka huu) katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam.
TFF_LOGO12
Kwa mujibu wa binti wa marehemu, Sophia, baba yake alianguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Lugalo ambapo ndipo umauti ulipomfika wakati madaktari wakimpatia matibabu.
Kanali Mwanakatwe alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1993 mjini Kibaha mkoani Pwani.
Baada ya kuondoka FAT, aligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kufanikiwa kushinda katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1997.
Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini na Afrika kwa ujumla kwani, Kanali Mwanakatwen enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi, na mkufunzi wa utawala wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Pia aliwahi kuwa Kamishna wa CAF.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, DRFA, na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na hoteli ya Giraffe wakati ndugu wakisubiriwa kutoka mikoani. TFF tunasubiri taratibu hizo ili tujipange jinsi ya kushiriki katika msiba huo.
Sisi sote ni waja wake Mola. Hakika kwake tutarejea.