Thursday, June 13, 2013

PSG YAJIWEKA TAYARI KUPAMBANA NA MADRID KUHUSU BALE"

Mabingwa wa ligi kuu nchini ufaransa msimu huu Club ya Paris Saint-Germain-PSG inajiandaa kupambana na klabu ya Real Madrid katika kumuwania mshambuliaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs Gareth Bale anayekisiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 85. Mabingwa hao wa ligi nchini Ufaransa wanataka kumchukua meneja Spurs Andres Villas-Boas ili aweze kumshawishi nyota huyo kumfuata kwenda huko. Hatahivyo, hata kama Villas-Boas akiamua kubakia jijini London, hilo haliwezi kuzuia nia ya klabu hiyo tajiri nchini Ufaransa kuvunja benki na kumsajili mchezaji huyo kwa dau kubwa. PSG imetumia zaidi ya paundi milioni 200 katika usajili wa nyota mbalimbali kuanzia mwaka 2011 wakati Kampuni ya Michezo inayosimamiwa na familia ya kifalme ya Qatari ilipoinunua klabu hiyo. Kwasasa PSG wameshakubali kuwa lazima wavunje rekodi ya usajili kama wanataka kumng’oa nyota huyo kutoka Tottenham, rekodi ambayo bado inashikiliwa na Cristiano Ronaldo ambaye Real Madrid walimnunua kwa paundi milioni 80 kutoka Manchester United.

LAPORTA AMKINGIA KIFUA MKALI WA DUNIA -MESSI

RAIS wa zamani wa mabingwa wa Hispania, Barcelona Joan Laporta amemkingia kifua nyota wa klabu hiyo Lionel Messi dhidi ya tuhuma za ukwepaji kodi zinazomkabili. Laporta ambaye ameiongoza Barcelona kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 aliiambia radio moja nchini humo kuwa ana uhakika kuwa si Messi wa baba yake wamefanya kitedo hicho. Messi na baba yake Jorge wameshitakiwa na jana na mwendesha mashtaka Raquel Amado wa mji wa Gava uliopo karibu na Barcelona ambapo anaishi nyota huyo, kwa kosa kukwepa kodi inayofikia kiasi cha euro milioni 4.1 kati ya mwaka 2007 na 2009. Laporta amesema hakumbuki katika kipindi chake chote cha uongozi kama nyota huyo alikuwa akijishughulisha na makampuni yasiyo halali, na anachojua yeye Messi aliyofautiana na mmoja wa washauri wake hivyo anadhani tuhuma hizo zimetoka huko.

FABREGAS AKANUSHA TUHUMA ZA KUREJEA JIJINI LONDON.

KIUNGO nyota wa klabu ya Barcelona Cesc Fabregas amekanusha  na kutanabaisha kuwa tuhuma  za kwamba anataka kurejea jijini London nchini Uingereza baada ya kukosa namba ya kudumu katika klabu hiyo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barcelona mwaka 2011 lakini Manchester United na klabu yake ya zamani ya Arsenal wanaaminika kutaka kumchukua mchezaji huyo kutoka Camp Nou. Fabregas amesema siku zote amekuwa na furaha Barcelona na yoyote anayesema kwamba anataka kuondoka hamjui na hajawahi kuzungumza nae.
Kiungo huyo ametokea katika shule ya vipaji ya Barcelona akiwa na miaka 10 mpaka 16 alisajiliwa na Arsenal, na ameichezea klabu hiyo mechi 303 kwa kipindi cha miaka nane na kufanikiwa kufunga mabao 57.

TIKETI MECHI YA STARS KUANZA KUUZWA KESHO

Wakati timu ya Ivory Coast inatarajiwa kuwasili leo usiku (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum, tiketi kwa ajili ya mechi kati yake na Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa zinaanza kuuzwa kesho mchana (Juni 14 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Vituo vitakavyotumika kwa mauzo hayo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani. Viingilio katika mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika katika kundi C ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, sh. 7,000 viti vya rangi ya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000. Pia viti 100 vilivyo katika sehemu ya Wageni Maalumu (VVIP) vitauzwa kwa sh. 50,000 kila kimoja. Tiketi hizo zitauzwa katika ofisi za TFF, na watakaonunua watapewa kadi maalumu zenye majina yao, majina ambayo pia watayakuta katika vita watakavyokaa. Kwa maana hiyo hakutakuwa pasi maalumu (free pass) za kuingia VVIP.

PONGEZI KWA RAIS MPYA WA ZFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amempongeza Rais mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Ravia Idarous Faina aliyechaguliwa katika uchaguzo mdogo uliofanyika hivi karibuni. Amesema ushindi aliopata Faina unaonyesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA walivyo na imani naye katika kuhakikisha maendeleo ya mpira wa miguu visiwani humo. Rais Tenga amesema ni imani yake kuwa Rais Faina ataendeleza ushirikiano uliopo kati ya TFF na ZFA kwa ajili ya ustawi wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kumtakiwa kila kheri katika wadhifa wake huo mpya.

WAAMUZI WATATU WAFUNGIWA MIEZI MITATU

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefungia miezi mitatu waamuzi watatu walioshindwa kuchezesha mechi namba 32 ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Mpwapwa Stars ya Dodoma na Machava FC ya Kilimanjaro iliyokuwa ichezwe Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. TFF kupitia Kamati yake ya Waamuzi iliyokutana katika kikao chake cha Juni 12 mwaka huu kupitia taarifa mbalimbali za waamuzi wa RCL ilibaini makosa yaliyofanywa na baadhi ya waamuzi na kuyatolea uamuzi. Waamuzi hao waliofungiwa ambao wanatoka mkoani Singida ni Jilili Abdallah, Amani Mwaipaja na Theofil Tegamisho. Wamefungiwa kwa kutoripoti katika kituo walichopangiwa (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma) na kutoa taarifa ya uongo kwa kushirikiana na Kamishna wa mechi hiyo. Kanuni iliyotumika kuwafungia ni ya 28 kifungu (d) na (g) ya Ligi za TFF, na adhabu hiyo imeanza Juni 13 mwaka huu. Waamuzi hao pamoja na kamishna badala ya kwenda Uwanja wa Jamhuri, wao walikwenda kwenye Uwanja wa Mgambo ulioko Mpwapwa na kuandika ripoti iliyoonesha kuwa timu ya Machava FC haikufika uwanjani wakati wakijua kuwa mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa katika Uwanja wa Jamhuri.

TAFAKARI YA LEO BARCA ILIVYOFANYA JEURI KUMTAFUTIA MESSI COMBINATION JE KWA NEYMA ITAKUWAJEEEE??

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Barcelona imetumia jumla ya Euro 205 milioni kwa ajili ya kusaka mshambuliaji ambaye anaweza kumpunguzia Messi mzigo wa ustaa alioubeba kwa muda mrefu klabuni hapo.
Hivyo kuwasili kwa mshambuliaji wa Santos na timu ya taifa ya Hispania, Neymar, katika kikosi cha Barcelona, inamaanisha kuwa Barcelona imeendelea kutumia fedha nyingi kusaka mshambuliaji ambaye anaweza kung’ara vyema kwa pamoja na staa wao, Lionel Messi.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Barcelona imetumia jumla ya Euro 205 milioni kwa ajili ya kusaka mshambuliaji ambaye anaweza kumpunguzia Messi mzigo wa ustaa alioubeba kwa muda mrefu klabuni hapo.
Thierry Henry
Katika msimu wake wa kwanza tu ndipo Henry alifikia matarajio ya mashabiki wa Barcelona. Baadaye kuibuka kwa kinda wa Kihispaniola, Pedro Rodriguez, kulimfanya Henry apate nafasi finyu ya kucheza katika kikosi cha kwanza na mwisho aliamua kutimkia Marekani katika klabu ya New York Bulls.
Hata hivyo Henry hakufikia kiwango alichokuwanacho wakati anachezea Arsenal chini ya Arsene Wenger ingawa katika kipindi chake na Barcelona alishinda mataji kadhaa.
Zlatan Ibrahimovich
Ukitazama hapa katika hali ya kawaida kilikuwa kipindi kibaya katika harakati za maisha ya soka ya Ibrahimovich. Tofauti na matarajio ya wengi, licha ya kusajiliwa kwa Euro 46 milioni huku pia Barcelona wakimtoa  Samuel Eto’o kwenda Inter Milan, bado Ibrahimovich hakutamba sana Nou Camp.
Mwishowe alijikuta akiingia katika mgogoro mkubwa na kocha wa wakati huo, Pep Guardiola. Ibrahimovich alimshutumu Guardiola kwamba alikuwa anampendelea zaidi Messi huku wakati mwingine akimchezesha nafasi ya kati wakati yeye yuko benchi.
Baada ya msimu mmoja tu, Zlatan aliondoka akarudi Italia ambako alijiunga na AC Milan.
David Villa
Alionekana mmoja kati ya wachezaji ambao wangeweza kumpunguzia mzigo wa mabao staa huyu wa Argentina. Alianza vema, lakini baadaye aliumia katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia, ilikuwa Desemba 2011.
Mbali na hilo tangu hapo kasi yake imepungua uwanjani na sasa inasemekana ataondoka zake Barcelona katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji.

LIONEL MESSI NA MZAZI WAKE WA KIUME WAINGIA MATATANI.

Mshambuliaji nyota  wa Barcelona  na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi na babake wanatuhumun kwa tuhuma za kukwepa kulipa kodi nchini Hispania huivyo serikali ya nchi hiyo ipo katika zaidi ambapo inasadikika kuwa na deni la paundi milioni tatu nukta nne.

Mchezaji huyo kutoka Argentina na babake, Jorge wanatuhumiwa kuibia serikali ya nchi hiyo, kwa kujaza fomu zisizokuwa za ukweli za marejesho ya kodi kati ya mwaka wa 2007 na 2009.Hata hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hajasema lolote kuhusiana na madai hayo.
Messi hulipwa Euro milioni kumi na sita kila mwaka na ndiye mchezaji anayelipwa kiasi cha juu zaidi duniani.Lakini mwendesha mashtaka Raquel Amado, aliwasilisha nyaraka za mahakama nyumbani kwa mchezaji huyo katika mtaa wa kifahari wa Gava mjini Barcelona.
Jaji mjini humo ni sharti waidhinisha malalamishi dhidi ya mshukiwa yeyote kabla hajafunguliwa mashtaka.Messi na babake wanashukiwa kutumia kampuni katika mataifa ya ng’ambo, mjini Belize na Uruguay kuuza haki za kutumia picha ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo na babake wanatuhumiwa kutumia kampuni hizo zilizoko nje ya Hispania, ambako anaishi na kucheza soka ya kulipwa, kukwepa kulipa kodi inayokisiwa kuwa paundi milioni tatu na nusu.

MASCHERANO AOMBA RADHI KUMPIGA TEKE DAKTARI WA TIMU:

KIUNGO nyota wa Club ya Barcelona na timu ya  taifa ya Argentina Javier Mascherano ameomba radhi baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga teke daktari wakati wa mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kati ya timu ya taifa ya nchi yake na Ecuador.
Kiungo huyo ambaye kucheza katika vilabu vya Liverpool na West Ham United alitolewa baada ya kumpiga teke dereva wa gari maalumu la kubebea wachezaji walioumia dakika ya 87 ya mchezo huo. 
Nyota huyo ambayo alikuwa nahodha katika mchezo huo aliomba radhi kwa tukio hilo na kudai kuwa alimuonya dereva kwa kwenda kasi mpaka kutaka kumdondosha ingawa amedai alichokifanya hakikubaliki.
Katika mchezo huo Argentina ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi Ecuador na kuendelea kubakia kileleni wakiwa na alama 27 wakifuatiwa na Colombia waliopo nafasi ya pili wakiwa na alama 26 huku Ecuador wakibakia nafasi ya tatu wakiwa na alama 22.

ESSIEN ASEMA NIPOM TAYARI KUCHEZA NAFASI YOYOTE UWANJANI:

KIUNGO nyota wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ghana Michael Essien amesema kuwa amejiandaa kucheza nafasi yoyote chini ya kocha mpya wa klabu hiyo Jose Mourinho. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ghana alikuwa akipewa nafasi kidogo ya kucheza chini Roberto Di Matteo baada kusumbuliwa na majeraha ya mguu lakini alipata ahueni wakati Mourinho alipomwita kwa mkopo wakati akifundisha Real Madrid. Mourinho amekuwa akimchezesha Essien kama beki au kiungo wakati akiwa Santiago Bernabeu na sasa yuko tayari kucheza nafasi yoyote ambayo Mreno huyo atamchezesha. Essien mwenye umri wamiaka 30 alisajiliwa na Mourinho wakati akiwa Chelsea mwaka 2005 kwa ada ya paundi milioni 29 akitokea klabu ya Lyon ya Ufaransa.