Sunday, May 5, 2013

SIMBA YAITWANGA RUVU SHOOTING BA 3-1 NAKUJIWEKA NAFASI YA 3


Wekundu wa msimbazi SIMBA leo imefanikiwa  kuitandika Ruvu Shootin kwa jumla ya  Bao 3-
katika Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom na kufanikiwa kukwea mpaka nafasi ya tatu. 
mabao ya Simba yafungwa  katika  Dakika ya 14 mfungaji akiwa Amri Kiemba Bao huku 
Kipindi cha Pili Ruvu Shootinga walichomoa katika Dakika ya 52 kwa Bao la Abdulrahman Musa
huku  Edward Christopher, Dakika ya 86 na Ismail Mkoko, Dakika ya 88.

MSIMAMO:


TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
YANGA
25
17
6
2
45
14
31
57
2
AZAM FC
24
14
6
4
42
20
22
48
3
SIMBA SC
24
11
9
4
37
23
14
42
4
KAGERA SUGAR
24
11
7
6
25
18
7
40
5
MTIBWA SUGAR
25
10
9
6
29
24
5
39
6
COASTAL UNION
25
8
11
6
25
23
2
35
7
RUVU SHOOTING
24
8
7
9
21
23
-2
31
8
JKT OLJORO
25
7
8
10
21
26
-5
29
9
TANZANIA PRISONS
25
7
8
10
16
22
-6
29
10
JKT RUVU
25
7
5
13
21
38
-17
26
11
MGAMBO SHOOTING
23
7
4
12
16
23
-7
25
12
POLISI MOROGORO
25
4
10
11
13
23
-10
22
13
TOTO AFRICAN
25
4
10
11
21
33
-12
22
14
AFRICAN LYON
25
5
4
16
16
38
-22
19

CHELSEA YAITANDIKA MAN UNITED MOJA TU KWA MTUNGI'


Katika mechiya BPL, Barclays Premier League, iliyopigwa hii leo  Uwanjani Old Trafford Chelsea imefanikiwa kuibuka na ushindi wa Bao 1-0  kuwafanya kupanda hadi nafasi ya 3.

MATOKEO YA LEO 
Jumapili 5 Mei
Liverpool 0 Everton 0
Man United 0 Chelsea 1 mfungaji dakika ya 87.
MSIMAMO WA LIGI KUU UINGEREZA BPL
BINGWA TAYARI NI MANCHESTER UNITED'
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man Utd
36
42
85
2
Man City
35
30
72
3
Chelsea
35
34
68
4
Arsenal
36
31
67
5
Tottenham
35
18
65
6
Everton
36
14
60
7
Liverpool
36
25
55
8
West Brom
35
1
48
9
Swansea
35
-1
43
10
West Ham
36
-8
43
11
Stoke
35
-10
40
12
Fulham
36
-11
40
13
Aston Villa
36
-21
40
14
Southampton
36
-11
39
15
Norwich
36
-22
38
16
Newcastle
36
-23
38
17
Sunderland
35
-12
37
18
Wigan
35
-22
35
19
Reading
36
-26
28
20
QPR
37
-29
25
TIMU HIZI TAYARI ZIMESHUKA DARAJA QPR & READING
kesho Jumatatu Mei 6
[Saa 4 Usiku]
Sunderland v Stoke
Jumanne Mei 7
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Man City v West Brom
Wigan v Swansea
KAZI IPO KATIKA TIMU HIZI KUWANIA 4 BORA KUCHEZA UEFA CHAMPIONS LIGI MSIMU UJAO
A. CHELSEA imeshuka dimbani mara 35 ikiwa na jumla ya pointi 68.
 Mechi zilizobakisha kwa upande wake.
Jumatano Mei 8
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Tottenham
Jumamosi Mei 11
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Aston Villa v Chelsea
Jumapili 19 Mei
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
B. ARSENAL imecheza dimbani mara 36 ikijikusanyia pointi 67
Mechi ilizobakisha kwa upande wake.
Jumanne Mei 14
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Wigan
Jumapili 19 Mei
[Saa 12 Jioni]
Newcastle v Arsenal.
C.TOTTENHAM imeshuka uwanjani mara 35 ikiwa na jumla ya pointi 65.
Mechi zilizobaki kwa upande wake.
Jumatano Mei 8
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Tottenham
Jumapili Mei 12
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Stoke v Tottenham
Jumapili 19 Mei
[Saa 12 Jioni]
Tottenham v Sunderland

RATIBA RCL KUPANGWA J’NNE, LIGI KUANZA MEI 12


Upangaji ratiba (draw) ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) uliokuwa ufanyike juzi (Mei 3 mwaka huu), sasa utafanyika Jumanne (Mei 7 mwaka huu) na ligi hiyo itaanza Mei 12 mwaka huu kama ilivyopangwa.

Uamuzi huo umefanya na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Mei 5 mwaka huu) kujadili maandalizi ya ligi hiyo, yakiwemo maombi ya baadhi ya mikoa ambayo haijamaliza yao kutaka RCL isogezwe mbele.

Kamati ya Mashindano chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ilipitia maombi hayo na kuangalia athari ambazo zinaweza kujitokeza huko mbele iwapo RCL itasogezwa mbele.

Baadhi ya athari iwapo RCL itasogezwa mbele ni timu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutopata muda wa kufanya usajili wa wachezaji kwa msimu mpya.

Hivyo draw hiyo itakayofanyika saa 6 mchana itahusisha mikoa ambayo tayari imemaliza ligi na kuwasilisha majina ya mabingwa wao. Mabingwa ambao wamewasilishwa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United (Pwani), Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).

Mingine ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe (Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1), Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).

Ada ya ushiriki ni sh. 100,000 wakati usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya Mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.

Mikoa iliyoshindwa kuwasilisha mabingwa wake ni Dodoma, Geita, Iringa, Lindi, Manyara, Mtwara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Tanga.

TAIFA STARS KUANZA COSAFA JULAI 6
Taifa Stars imepangwa kundi A la michuano ya Kombe la COSAFA ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Julai 6 mwaka huu jijini Lusaka, Zambia dhidi ya Shelisheli.

Upangaji ratiba (draw) wa mashindano hayo ulifanyika juzi (Mei 3 mwaka huu) jijini Lusaka ambapo timu nyingine zilizo na Taifa Stars katika kundi hilo ni Namibia na Mauritius. Kundi la Taifa Stars litachezea mechi zake jijini Lusaka.

Mechi ya pili ya Taifa Stars katika hatua ya makundi itakuwa Julai 8 mwaka huu dhidi ya Mauritius. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo itakuwa Julai 10 mwaka huu dhidi ya Namibia.

Kundi B lina timu za Kenya (Harambee Stars), Botswana (Zebras), Lesotho na Swaziland. Hatua itakayofuata baada ya hapo ni ya mtoano (knockout) na kila kundi litatoa timu moja tu.

Iwapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itafuzu kwa hatua itakayofuata itacheza Julai 13 mwaka huu na Afrika Kusini (Bafana Bafana) ambayo pamoja na timu nyingine tano zimekwenda moja kwa moja katika hatua ya mtoano.

Nyingine zilizokwenda moja kwa moja hatua ya mtoano ni wenyeji Zambia, Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Malawi ambazo kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ziko juu ya zile zilizoanzia hatua ya makundi.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, fainali ya michuano ya Kombe la COSAFA itafanyika Julai 20 mwaka huu.

AZAM FC KUREJEA NYUMBANI KESHO
Timu ya Azam inatarajiwa kurejea nchini kesho (Mei 6 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates kutoka Morocco ambapo jana (Mei 5 mwaka huu) ilicheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya huko.

Azam ilipoteza mechi hiyo kwa mabao 2-1, hivyo kutolewa katika raundi ya pili ya mashindano hayo. Mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka suluhu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)