Monday, August 18, 2014

SIMBA YAENDELEA NA TIZI ZANZIBAR

Simba wekundu wa Msimbazi Simba wanaendelea vyema na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi septemba 30 mwaka huu.
Simba wameweka kambi visiwani Zanzibar (Unguja) chini ya kocha mkuu mpya, Mzambia, Patrick Phiri akisaidiwa na kocha msaidizi, kiungo wa zamani wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ na kocha wa makipa, Idd Pazzi ‘Father’.

FIFA KUBORESHA MAKAO MAKUU YA TFF

ofisi-za-TFFSHIRIKISHO la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limeahidi kuboresha makao makuu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yaliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala ili yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na vitendea kazi na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa ofisi.
Hatua hiyo itaiwezesha TFF kuwa na mazingira bora ya kufanya shughuli zake kwa ufanisi. Vilevile kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya Goal, FIFA imeahidi kushirikiana na TFF katika kuendeleza mradi wa kiuchumi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

YANGA YATUA PEMBA KUWEKA CHIMBO LA VPL SEPT 20,2014

Msafara wa watu 35 ukiwa na wachezaji 27 na benchi la Ufundi 8 wa timu ya Young Africans tayari umeshawasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kujiandaa na mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Kocha mkuuu Marcio Maximo na kikosi chake wamefikia katika hoteli ya kitalii ya Pemba Misali iliyopo eneo la Wesha na watakua wakijifua kwa muda wa takribani siku 10 kabla ya kurejea jijini Dar es salaam mwisho wa mwezi huu.
Kikosi cha Young Africans kitakua kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani mjini Chake Chake na siku ya alhamis wanataraji kucheza wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya Chipukizi ya kisiwani Pemba.
Kulingana na program ya bench la Ufundi kisiwani Pemba, Young Africans inatarajia kucheza michezo mitatu ya kirafiki na timu za kutoka Visiwa vya Pemba na Unguja na baadae kurejea Dar es salaam kwa michezo mwili ya kimataifa kabla ya kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani septemba 13, 2014.
Wachezaji waliondoka kuelekea Pemba ni:
Walinda Mlango:
Juma Kaseja, Ally Musatfa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida"
Walinzi wa Pembeni:
Juma Abdul, Salum Telea, Oscar Joshua, Edwad Charles na Amos Abel
Walinzi wa Kati:
Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Rajab Zahir na Pato Ngonyani.
Viungo:
Mbuyu Twite, Said Juma "Makapu", Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis Thabit.
Viungo wa Pembeni:
Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Andrey Coutinho.
Washambuliaji:
Geilson Santos "Jaja", Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein Javu 
Benchi la Ufundi walioko Kisiwani Pemba ni:
Kocha Mkuu : Marcio Maximo
Kocha wasaidizi Leonado Neiva, Salvatory Edward
Kocha wa Makipa:  Juma Pondamali
Daktari wa timu: Dr Suphian Juma
Meneja wa timu:  Hafidh Saleh
Mchua Misuli: Jaco Onyango
Mtunza Vifaa: Mahmod Omar "Mpogolo"