BEKI wa Liverpool Joel
Matip ni mmoja kati ya wachezaji saba ambao wamesema hawataki kwenda
kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika ambayo inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi Januari 14 mwakani.
Kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na
Shirikisho la Soka la nchi hiyo-FECAFOOT imedai kuwa beki huyo ametoa
kauli hiyo kupitia uzoefu wake aliopata katika benchi la ufundi
lililopita. Beki wa West Browich Albion, Allan Nyom ni miongoni mwa
orodha ya wachezaji saba waliogoma.
FECAFOOT inaweza kuliagiza
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwasimamisha wachezaji hao kuzitumikia
klabu zao kwa kipindi cha wiki tatu michuano hiyo itakapokuwa
ikiendelea.
Kocha wa Cameroon, Hugo Broos amesema wachezaji hao
waliogoma wameweka maslahi yao mbele kuliko yale ya timu ya taifa na
shirikisho lina haki ya kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za FIFA.
WEngine waliopo katika mgomo huo ni pamoja na Andre Onana wa Ajax
Amsterdam, Guy N’dy Assembe wa Nancy, Maxime Poundeje wa Bordeaux,
Andre-Frank Zambo Anguissa wa Marseille na Ibrahim Amadou wa Lille.
Cameroon imepangwa kundi A sambamba na wenyeji Gabon, Burkina Faso na
Guinea Bissau.