Saturday, June 29, 2013

ARSENAL WAMTAKA KIPA JULIO CESAR WA QPR ILIYOSHUKA DARAJA"

Wanted: Julio Cesar is set to join Arsenal following Queens Park Rangers' relegation to the Championship WASHIKA Bunduki wa jiji London Club ya Arsenal itaangalia uwezekano wa kukamilisha usajili wa kipa namba wa Brazil na klabu ya Queens Park Rangers, Julio Cesar baada ya Kombe la Mabara.
Arsene Wenger anataka kipa mzoefu atengeneze ushindani kwa Lukasz Fabianski na Wojciech Szczesny.
Mazungumzo baina ya wawakilishi wa Cesar na viongozi wa Gunners tayari yamefanyika, lakini hayajamalizika kwa kuwa kipa huyo yupo kwenye majukumu ya kimataifa.
Wanted: Julio Cesar is set to join Arsenal following Queens Park Rangers' relegation to the Championship
ARSENAL sasa inatarajiwa kumaliza dili hilo mara moja tu, baada ya kubainika Roma ya Italia nayo imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya Cesar.
Kipa huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye yupo huru kuondoka Loftus Road kufuatia kushuka kwa QPR hadi Championship, anataka kubaki London ambako amezoea maisha tangu awasili msimu uliopita akitokea Inter Milan.
Na The Gunners – ambayo inatumai kukamilisha pia usajili wa Gonzalo Higuain wiki ijayo, baada ya kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti kufungua njia kwa mshambuliaji huyo kuondoka  Hispania – inajiamini dili hilo litakamilishwa baada ya Fainali ya Kombe la Mabara Jumapili.
Wenger alitaka kusajili kipa wa Stoke, Asmir Begovic na wa Liverpool, Pepe Reina lakini, licha ya kuwa na fungu la bajeti ya usajili la Pauni Milioni 70, kocha huyo wa Arsenal ameona  hana sababu ya kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kipa.
Rangers itasikiliza ofa ya kiasi cha Pauni Milioni 2 kwa Cesar, wakati mshahara wake wa Pauni 70,000 kwa wiki halitakuwa tatizo kwa The Gunners, ambayo imetuma waangalia vipaji wake nchini Brazil kumuangalia Cesar anachokifanya katika Kombe la Mabara.
Pamoja na mpango wa kuwasajili Cesar na Higuain, The Gunners pia wanataka kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams na kiungo wa Everton, Marouane Fellaini. Lakini masuala ya kifedha yanatia saka kama Arsenal itaweza kusajili wachezaji wote hao.
Hadi sasa, Arsenal imegoma kumpa Fellaini mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki na pia imeshindwa kufika dau la Pauni Milioni 24 za kumnunua.
Missing out? Arsenal look set to be priced out of moves for Marouane Fellaini and Ashley Williams (below) Amekosekana? Arsenal inataka kuwasajili Marouane Fellaini

MBEYA MWENYEJI WA NETIBOLI TENA KWA MARA YA PILI MFULULIZO".

Jiji la Mbeya kwa mara ya pili mfululizo,litakuwa mwenyeji wa ligi kuu ya Netiboli taifa ambapo  naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo anatarijiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi kuanzia Agosti 24 hadi Septemba 7.
Mwenyekiti wa chama cha Netiboli Mkoa wa Mbeya, Mary Mung’ong’o ameumabia mtandao huu kuwa ligi hiyo inafanyika kwa mara nyingine kutokana na ombi la Waziri Mulugo kwa vile ligi hiyo haikuwa imefana, hivyo akaiomba CHANETA kuwapa Mbeya fursa nyingine ya uwenyeji.
Alisema maandalizi ya ligi yameanza na kusema zinahitajika sh milioni 16 kufanikisha na kuongeza kuwa hadi sasa, hawajajua timu ngapi zitashiriki kutokana na jukumu hilo kuwa chini ya Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA).
Hata hivyo, mwenyekiti huyo ametoa wito kwa viongozi wa ngazi mbalimbli wakiwemo wadau wenye mapenzi na mchezo kutoka mkoani hapa kujitoa kwa hali na mali kuyafanikisha ili yawe chachu ya kukua kwa mchezo huo nchini kwa maslahi ya vijana na taifa.
Aidha, mwenyekiti huyo alitamtambulisha Nwaka Mwakisu kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo.
Akizungumzia mashindano hayo, Mwakisu alisema ni fursa kwa watu wa Mbeya kujitangaza kibiashara kupitia mchezo huo na kufuta makosa yaliyofanyika mwaka jana.
Alisema katika kufakisha mashindano hayo, nguvu ya pamoja inahitajika kuanzia viongozi wa kisiasa, serikari na vyombo vya habari.

MBASPO FC YATWAA UBINGWA WA AIRTEL RISING KWA MKOA WA MBEYA"

Kama kawaidaTimu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Mbaspo imefanikiwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mbeya baada ya kukusanya pointi nne sawa na mahasimu wao Mbosa fc lakini wakiwa na magoli mengi ya kufunga. Timu ya Mbeya Secondari haikupata hata pointi moja katika michuano hiyo ya kusaka vipaji

Mbaspo walianza mbio zao za kutwaa ubingwa kwa kutoshana nguvu ya 3-3 dhidi ya Mbosa siku ya Jumatatu Juni 24 kabla ya kufanya mauaji makubwa ya 6-0 dhidi ya timu dhaifu ya Mbeya Sekondari siku ya Jumanne. Michezo yote imefanyika kwenye uwanja wa Magereza jijini Mbeya.
Mbosa walifikisha point nne juzi Jumatano walipoitandika Mbeya Sekondari 3-0 hivyo kumaliza wakiwa na point nne na magoli sita wakati wapinzani wao Mbaspo wakifikisha jumla ya magoli tisa ya kufunga. Katika mechi ya juzi, magoli ya Mbosa yalitiwa kwenye kamba na Michael Mwashilanga, Riziki Juma na Julius Landa.
Wakati huo huo, chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya kimetangaza kikosi cha wachezaji 18 kuuwakilisha mkoa huo kwenye michuano ya Taifa ya Airtel Rising Stars inayoanza kutimua vumbi kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2.

Wachezaji hao ni Ismail Yesaya, Emmanuel Alex, Gift Sanga, Jackson Mwaibambe, Boaz Mwangole, Costa Sanga, Seif Zubery, Stanley Angelo, Enock Sikaonga, Kaunda Malata, Joel Kasimila, Hamprey Nyeo, Elia Salengo, Peter Noah, Emmaneul Mtimbi, Michael Bosco, Richard Kalinga na Zamoyoni Mwashambwa. 

Katika mkoa wa Morogoro, mji kasoro bahari, timu ya Moro Kids imetoka sare ya bila kufungana na Techfort katika mchezo wa kushambuliana kwa zamu uliopigwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Morogoro juzi Jumatano na kushuhudiwa na mashabiki wengi wa mji huo
Airtel Rising Stars vile vile imeanza kutimua vumbi katika jiji la Mwanza ambapo timu ya Marsh Athletical imedhihirisha umwambe wake katika soka baada ya kuifunga Nyamagana United 2-0 kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana.
Timu za mikoa zimepangwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki tayari kwa ajili ya kindumbwe ndumbwe cha Airtel Rising Stars ngazi ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Wachezaji 16 watachaguliwa wakati wa mashindano hayo ili kuunda timu itakayoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars. Nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa baadaye mwezi ujao.