Friday, May 3, 2013

SEPP BLLATTER - AWEKA NIA YA KUGOMBEA TENA URAIS WA FIFA

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter ametoa dondoo ya kwamba ana mpango wa kugombea tena nafasi hiyo kwa miaka minne mingine wakati wa hotuba yake mara baada ya mkutano na viongozi wa Shirikisho la Soka la Asia-AFC nchini Malaysia. Mapema Machi mwaka huu Blatter amesema ana mpango kwa kuachia ngazi wakati atakapomaliza kipindi chake cha miaka minne kitakapoisha mwaka 2015 lakini akaongeza kuwa ataachia nafasi hiyo pale atakapoamini kwamba atakayemwachia anaweza kulisongesha mbele gurudumu la shirikisho hilo. Blatter mwenye umri wa miaka 77 alirudia tena kauli ya katika mkutano wa AFC jijini Kuala Lumpur jana akidai kuwa yeye ni nahodha na hawezi kuachia meli yake izame wakati bado anaona ana nguvu za kuizuia isifanye hivyo. Kauli hiyo ya Blatter imewafanya wachambuzi wa mambo ya soka wadai kuwa rais huyo ana mpango wa kugombea urais kwa kipindi kingine baada ya kumaliza hiki cha sasa mwaka 2015. Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini ambaye alikuwepo katika mkutano huo ambao ulishuhudia Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa wa Bahrain akiteuliwa kuwa rais wa AFC, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kushika nafasi ya Blatter atakapoacia madaraka. 

BENITEZ AWATAKA MASHABIKI WA CHELSEA KUMUHESHIMU


Rafael Benitez kocha wa muda wa chelsea amesema anastahili kuheshima kwa kuipeleka Chelsea kutinga Fainali ya EUROPA LIGI ambapo watakutana na Benfica huko Amsterdam ArenA hapo Mei 15.








Wakiwa katika dimba la uwanja wa Stamford Bridge katika Mechi ya Marudiano ya
Nusu Fainali ya EUROPA LIGI na FC Basel huku wakiwa wameshinda Bao 2-1
toka Mechi ya kwanza, Chelsea walitanguliwa Bao 1-0 hadi Mapumziko
 lakini Kipindi cha Pili waliisambaratisha Basel kwa kuitandika Bao 3 ndani ya
Dakika 9 kwa Bao za Torres, Moses na Luiz.
MAGOLI:
Chelsea 3
*Torres Dakika ya 50
*Moses 52
*Luiz 59
FC Basel 1
*Salah Dakika ya 45
Hii ni Fainali ya 10 kwenye himaya ya Mmiliki Roman Abramovic huku
 Chelsea wakitwaa  Mataji 11 na watakuwa wakiwania Rekodi ya kuwa
 Klabu ya 4 Barani Ulaya kuweza kutwaa Mataji yote makubwa ya Ulaya
yakiwemo UEFA CUP WINNERS CUP [Kombe la Washindi] na
UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Chelsea, ambao walitwaa Kombe ambalo sasa halipo, Kombe la Washindi,
mara mbili Miaka ya 1970/71 na 1997/98, pamoja na la Klabu Bingwa Ulaya Mwaka jana
, hawajawahi kutwaa UEFA CUP, ambalo sasa ndio EUROPA LIGI.
Klabu nyingine 3 ambazo zimefuzu kutwaa Mataji yote hayo makubwa ni Juventus, Ajax
 na Bayern Munich.
MAKOMBE ENZI ZA ABRAMOVICH:
*BPL 3
*FA CUP 3
*KOMBE LA LIGI 2
*UEFA CHAMPIONZ LIGI 1
*NGAO YA HISANI 2

LIEWIG AFUNGUKA KUHUSU MECHI NA WATANI ZAO WA JADI


Kocha Mkuu wa Wekundu wa msimbazi Simba, Patrick Liewig amesema kuwa silaha yake kubwa katika mechi dhidi ya Yanga  may 18 mwaka huu ni kasi ya wachezajiwake, ingawa amekiri wanatakiwa kuwa makini kwa dakika zote 90 za mchezo.

Mfaransa huyo alisema jijini Dar es Salaam kuwa tayari wamepoteza ubingwa wa ligi pamoja na nafasi ya pili ambayo
ingeweza kuifanya timu hiyo ishiriki Kombe la CAF mwakani.
aidha amesema hakuna  nafasi tena ya kushinda taji la ligi kwa msimu huu wala kumaliza katika nafasi ya pili ambayo ingetupa fursa ya kushiriki Kombe la CAF mwakani.

kubwa zaidi Kilichobaki ni kulinda heshima yetu kwa kuwafunga mabingwa (Yanga) katika mchezo wetu wa mwisho hiyo Mei 18. Timu yangu ya Simba ina wachezaji wengi vijana ambao wana kasi kubwa kuwazidi Yanga." alisema kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic aliyetupiwa virago na klabu hiyo mwaka jana.
Kocha huyo ameongeza na kusema kuwa Yanga ni timu nzuri hakuna mtu anayepinga hilo, lakini haiwezi kumudu kasi ya wachezaji wangu vijana.

hata hivyo liewing amesema Nimewaona katika mechi kadhaa za ligi, wanacheza vizuri ingawa sitaki kuaminikwamba watashinda mbele ya vijana wangu imara."
Liewig amesema katika kambi ya kujiwinda na mchezo huo ataongeza muda wa programu yake ya mazoezi kuhakikisha kikosi chake kinakuwa katika hali nzuri ya ufiti kabla ya kukutana na watani hao wa jadi katika soka la Tanzania Bara na kuharibu sherehe za ubingwa huo.

25 WARIPOTI KAMBINI YOUNG TAIFA STARS

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Mei 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam kupokea na kupanga utekelezaji wa maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusu uchaguzi wa shirikisho.

Kikao hicho cha dharura chini ya Uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga kitakuwa na ajenda hiyo moja tu katika kuhakikisha utekelezaji wa maelekezo ya FIFA unafanyika haraka ili uchaguzi ufanyike ndani ya muda uliopangwa.

FIFA katika maelekezo yake imetaka kwanza ziundwe Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TFF. FIFA imeagiza uchaguzi uwe umefanyika kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

KILA LA KHERI AZAM KOMBE LA SHIRIKISHO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam katika mechi yake ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayochezwa Morocco kesho (Mei 4 mwaka huu).

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa jijini Rabat kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Morocco. Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.

Azam iko nchini Morocco kwa karibu wiki nzima sasa ikijiandaa kwa mechi hiyo chini ya Kocha wake Stewart John Hall. Msafara wa Azam nchini humo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella.

25 WARIPOTI KAMBINI YOUNG TAIFA STARS
Wachezaji 25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha pili cha Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini ambapo mazoezi yalianza tangu jana jioni (Mei 2 mwaka huu).
Kocha Kim amewaitaka wachezaji katika kambi hiyo ya siku tano ili kuangalia uwezo wao katika maeneo kadhaa kwa lengo la kupata baadhi ambao anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars siku za usoni.

Wachezaji watano walioshindwa kujiunga katika kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula, David Mwantika, Himid Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na timu yao ya Azam.

KAMATI YA MASHINDANO KUPITIA MAANDALIZI RCL
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyopangwa kuanza Mei 12 mwaka huu.

Tayari mikoa 18 kati ya 27 kimpira imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya RCL itakayotoa timu tatu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014).

Kamati hiyo chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF itapokea taarifa ya maandalizi ya ligi hiyo kutoka Idara ya Mashindano ya TFF na kufanya uamuzi juu ya mikoa ambayo haijawasilisha mabingwa wao.

Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na ratiba (draw) itapangwa wakati wowote. Ada ya kushiriki ligi hiyo kwa kila klabu ni sh. 100,000 na usajili utakaotumika na ule ule wa ligi ngazi ya mkoa. Hakutakuwa na usajili mpya wa wachezaji.

LALA SALAMA VPL KUENDELEA JUMAPILI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ruvu Shooting na Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.

Hiyo itakuwa mechi ya raundi ya 24 kwa timu hizo ambapo Simba iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 39 nyuma ya mabingwa Yanga wenye pointi 57, Azam yenye pointi 48 na Kagera Sugar ambayo ina pointi 40. Ruvu Shooting iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 31.

Hadi sasa mabao 348 yameshafungwa katika ligi hiyo huku Yanga ikiongoza kwa kufunga 45. Polisi Morogoro yenye pointi 22 katika nafasi ya 12 ndiyo iliyofunga mabao machache ikiwa nayo 13 tu.

African Lyon yenye pointi 19 katika nafasi ya mwisho ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kadi nyingi. Timu hiyo inayofundishwa na Charles Otieno ina kadi 44 ambapo kati ya hizo nne ni nyekundu. Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro yenyewe inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi nyekundu ambapo hadi sasa inazo saba.

YANGA, COASTAL UNION ZAINGIZA MIL 66
Mechi namba 172 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa juzi (Mei 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 imeingiza sh. 66,022,000.

Watazamaji 11,478 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,378,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,071,152.54.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 10,230 na kuingiza sh. 51,150,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 69 na kuingiza sh. 1,380,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,819,793.62, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,691,876.17, Kamati ya Ligi sh. 4,691,876.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,345,938.09 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,824,618.51.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)