Mzambia Patric phiri atua jijini dar es salaam lengo likiwa ni
kufanya mazungumzo ya kina na uongozi wa club hiyo ili kusaini Mkataba wa
kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC ambayo hivi karibuni ulimtupia
virago alikuwa kocha mkuu Logarusic.
Akitua katika viwanja wa JK nyerere hii leo mashabiki wachache walitokeza
kumpokea kocha huyo hivyo asilimia kubwa ya phiri ndie atakuwa kocha mkuu wa
simba kwa msimu ujao wa ligi kuu vodacom tanzania bara unao tarajiwa kuanza
kutimua vumbi mnamo september 20 mwaka huu.
Katika akifundisha simba Phiri aliwahi kuwa Kocha bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick Phiri anatarajiwa kutua Dar
es Salaam wiki hii kwa ajili Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya
kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004
na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi zake.
Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC,
misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005
la Tanzania na Kenya.
Kiboko ya Yanga anarudi; Patrick Phiri anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam
Ijumaa kusaini Simba SCMazungumzo yamekwishanyika na makubaliano yamefikiwa
baina ya Phiri na Simba SC na sasa atakuja kufanya kazi tena Msimbazi,
akisaidiwa na Nahodha wake enzi zake akifundisha timu hiyo, Suleiman Abdallah
Matola ‘Osama’.
Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC
miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa
zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa
hata mechi moja.
Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC
kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha
mwenye heshima ya kipekee Msimbazi.
Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali,
Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.
Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye
watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green
Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.
Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka
katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani
kwao, Zambia kama mshambuliaji.
Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia
kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya
kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana.
Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya
vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za
Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora
wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.