SHIRIKISHO la Soka la Ghana-GFA limetoa taarifa ya kuinyima ruhusa Sierra Leone
ya kutumia moja ya viwanja vyake kwa ajili ya mechi yao ya kufuzu
michuano ya Mataifa ya Afrika. Sierra Leone ilikuwa imeomba ruhusa
kucheza baadhi ya mechi zake za kufuzu michuano hiyo nchini Ghana
kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola nyumbani kwao. Katika
taarifa ya Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF iliyotolewa jana imedai
kuwa Sierra Leone walielekeza mechizao za nyumbani katika mzunguko wa
mwisho wa kufuzu zichezewe Ghana. Baada ya CAF kutuma maombi hayo ya
Sierra Leone kwenda kwenye mamlaka husika Ghana, GFA walijibu kwa
kuwataka majirani zao hao kushughulikia suala hilo kiserikali. GFA
limelitaka Shirikisho la Soka la nchini hiyo kutuma maombi yao
serikalini kwani suala hilo linahusisha mambo ya afya hivyo wao watakuwa
hawana kauli kwenye hilo.