VAN GAAL AWATAKA SHABIKI WA MAN UNITED KUWA NA SUBIRA

BOSI mpya wa Manchester United Louis van Gaal
anadhani atahitaji muda zaidi ili kuibadilisha timu hiyo pamoja na
kukamilisha mechi sitaza kujipia nguvu kabla ya kuanza kwa msimu kwa
ushindi. United ilimaliza ratiba yao ya mechi zao kujipima nguvu kwa
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Valencia jana usiku na kumpa Mholanzi huyo
ambaye alichukua mikoba baada ya kuingoza nchi yake kushika nafasi ya
tatu katika Kombe la Dunia, ushindi wa kwanza katika Uwanja wa Old
Trafford. Sasa United wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Swansea City
katika ufunguzi wa Ligi Kuu nyumbani Jumamosi lakini Van Gaal hana
uhakika kama Jonny Evans, Luke Shaw
na Antonio Valencia ambao hawakucheza mechi ya jana kutokana na
majeruhi kama watakuwa fiti. Watatu hao wakiwa benchi, Van Gaal
alilazimika kuwatumia Phil Jones, Chris Smalling na Tyler Blackett
katika nafasi ya ulinzi wa kati huku Asley Young na Reece James
wakicheza kama katika wingi.Akiwa amefanikiwakufanya usajili wa
wachezaji wawili pekee ambao ni Shaw na Ander Herrera kiangazi hiki, Van
Gaal amesema bado anahitaji muda kwani timu wala wachezaji hawawezi
kubadilika katika kipindi cha wiki mbili au tatu.