Hawa ni washindi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara tangu mwaka 1965. Katika rekodi hii klabu ya Yanga
imetwaa taji hilo mara 24, Simba mara 18 na mtibwa mara 2, nyingine zote
zilizopoa hapa zimetwaa mara moja. Tarehe 20 ligi itaanza tena ya msimu
wa 2014/15, Je Unadhani timu gani ipo katika nafasi ya kushinda taji
hilo msimu huu?
Thursday, September 11, 2014
WEKUNDU WA MSIMBAZI KUTIFUANA NA URA YA UGANDA
Simba Wekundu wa msimbazi SC kesho wanatarajia kushuka dimbani kuonyeshana kazi katika Mechi ya pili ya kimataifa ya kirafiki chini ya kocha Patrick Phiri
dhidi ya timu ya mamlaka ya ukusanyaji wa mapato nchini Uganda, URA katika uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam katika mtanange utakao anza majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki.
Wakati huo huo jumamosi jioni,
Simba itakuwa na mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Ndanda fc katika
uwanja wa Nangwanda Sijaona mk
oani Mtwara katika maadhimisho ya ‘Ndanda
fc Day’.
TAREHE NDONI YA TAIFA 2014 2014 YAPIGWA KALENDA
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT)
limesogeza tarehe ya kufanyika kwa mashindano ya ngumi ya Taifa na sasa
yatafanyika kuanzia tarehe 03-08/11/2014.Dar es salaam.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika tarehe 08-14/10/2014 Dar es salaam.
Sababu za kusogeza mashindano hayo
ni kuyapisha mashindano ya ngumi ya kimataifa yaliyoandaliwa na chama
cha ngumi wilaya ya Temeke yanayotarajia kuanza kufanyika mwishoni mwa
mwezi huu, lakini pia ni kutoa nafasi zaidi kwa mikoa ili kujiandaa
vizuri na kufanya mashindano ya kuwapata wawakilishi wa mikoa yao katika
mashindano ya taifa.
BFT tunawataki maandalizi mema na tunatoa wito kwa maafisa michezo
wa mikoa yote ya Tanzania bara kuhakikisha wanaleta wachezaji kutoka
katika mikoa yao ili kuleta upinzani utakaopelekea kupata timu ya taifa
iliyo bora kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara.
Aidha BFT inawapongeza kampuni ya
simu za mkononi ya Z antel kwa udhamini wa mashindano hayo kwa
kutoa kiasi cha Tsh. 10,000,000/=ambazo zitasaidia baadhi ya mahitaji ya
msingi ya kufanikisha mashindano hayo.
MWAMBUSI ASEMA PHIRI, MAXIMO, ASEMA NGOMA DAKIKA 90.

Akizungumza na mtandao huu,
Mwambusi amesema kocha Phiri ana historia ya kufundisha soka la Tanzania
kwa ngazi ya klabu wakati Maximo amefundisha timu ya Taifa, lakini wote
wataleta changamoto nzuri kwake.
Subscribe to:
Posts (Atom)