Tuesday, July 16, 2013

KUTOA OFA PAUNI MILIONI 40 KUMNUNUA HULK--CHELSEA

Katika harakati za usajili baada ya kuikosa saini ya kumnasa Straika hatari wa Uruguay, Edinson Cavani, ambae sasa yuko njiani kukamilisha ku

hamia PSG kutoka Napoli, Chelsea sasa imemgeukia Straika wa Klabu ya Urusi Zenit St Petersburg, Hulk, anaetoka Brazil.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ana nia ya kuongeza safu yake ya Ushambuliaji na tayari ameshamnunua Mchezaji wa Germany Andre Schurrle huku kukiwa na tetesi Mastraika wa sasa, Fernando Torres na Demba Ba, huenda wakapigwa bei.
Katika Msimu wake wa kwanza na Zenit, Hulk alifunga Bao 11 katika Mechi 30 na kabla hajahamia huko Urusi, akiwa huko Portugal na FC Porto, Hulk aliifungia Klabu hiyo Bao 54 katika Mechi 99 za Primera Liga na Jumla ya Mabao yake kwa FC Porto ni 78.
Inadaiwa Chelsea imetoa Ofa ya kwanza ya Pauni Milioni 40 kwa Mchezaji alienunuliwa Septemba Mwaka Jana kwa Pauni Milioni 35.

SIMBA YAJA NA MKUTANO MKUU JALAI 20 MWAKA HUU VS TBL"

Club ya soka ya Simba, inatarajia kufanya wake Mkutano Mkuu Jumamosi Julai 20 na Mdhamini wao, TBL, Tanzania Breweries Limited ambapo mdhamini huyo ametoa Shilingi Milioni 20 ili kuendesha Mkutano huo.
Mkutanno Mkuu huo ni fursa safi kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, kuwasilisha Ripoti ya shughuli za Klabu hiyo.
TBL, ambayo ina Mikataba ya Miaka mitano mitano ya kuzidhamini Yanga na Simba kuanzia Miaka miwili iliyopita, inawajibika kuzipa Klabu hizo Shilingi Milioni 20 kila mmoja ili kuendesha Mikutano Mikuu ya Vilabu vyao.
Akiongea wakati akikabidhi Cheki ya Shilingi Milioni 20 kwa Simba, George Kavishe, Meneja wa Bia ya aina ya Kilimanjaro Premium Lager, alisema: "Kama Wadhamini wakuu, tunatoa Fedha hizi kama jukumu letu kwa Klabu ili iwajibike, ipate mafanikio nje na ndani ya Uwanja. Tunaamini Mkutano huu utaimarisha uhusiano kati ya Simba na Wanachama wake kwa kuwapa nafasi kupitia masuala ya Klabu yao waipendayo."
Nae Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, aliishukuru TBL kwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa Mkataba na akaahidi Fedha hizo zitatumika kama ilivyokusudiwa.
Kwa baadhi ya Wadau wa Simba Mkutano Mkuu huu unasubiriwa kwa hamu kubwa hasa baada ya Klabu hiyo kugubikwa na mfarakano na Mwezi Machi Kikundi kimoja cha waliodaiwa kuwa Wanachama kujaribu kumpindua Rage kwa madai ya kushindwa kuongoza lakini jaribio hilo halikufua dafu.
Pia, inasemekana ipo Kambi ya Wanachama itakayoshika bango waelezwe kinagaubaga nini kimetokea kuhusu kuuzwa kwa Straika wao kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, kwa Klabu ya Tunisia Etoile Sportive Du Sahel Mwezi Januari kwa Dau linalodaiwa kuwa Dola Laki 3 na Klabu kutolipwa Fedha hizo hadi sasa.
Wengine watapenda wajue nini kiliwasibu Msimu uliopita na kumalizika Mwezi Mei huku Simba ikinyang’anywa Taji lao la Ubingwa na Mahasimu wao wakubwa, Yanga, na pia kujikuta wakibwagwa hadi Nafasi ya 3 nyuma ya Yanga na Azam na hivyo kutopata fursa ya kucheza Mashindano ya Klabu Barani Afrika Mwakani.

FABREGAS ASEMA AMWAMBIA VILANOVA NATAKA KUBAKI HAPA"

Meneja wa Manchester United,  David Moyes huenda akapata pigo lingine baada ya kiungo wa FC Barcelona, Cesc Fabregas kumweleza kocha wake  Tito Vilanova kuwa anataka kubakia ndani ya club ya Barcelona wazee wa Katalunya.

Ambapo Jana julai 15 Man united walithibitisha kutuma ofa ya pauni milioni 26 ili kumsajili Febregas,  nahodha wa zamani wa washika bunduki wa kaskazini mwa London, klabu ya Asernal.

Dili la kumhitaji Febregas limekuja baada ya  Thiago Alcantara kujiunga na kocha wake wa zamani Pep Guardiola  
Wachezaji wa Barcelona wakiwa mazoezini kwa ajili ya msimu mpya wa La Liga
katika klabu ya Bayern Munich badala ya kujiunga ma mabingwa wa ligi kuu soka nchini England, Manchester United.

Mambo yamekuwa magumu kwa United baada ya kocha wa Barca Tito Vilanova kuweka wazi kuwa amezungumza na Febregas ambaye amesema anataka kubakia Camp Nou.

Vilanova alisema: ‘Cesc amepokea ofa kutoka klabu nyingine. Nilizungumza naye na ameniambia anataka kubakia hapa. Ndoto yake ni kutwaa makombe hapa”

“Tunafurahi kuwa na Cesc. Nafahamu amepata ofa nyingi, lakini ameniambia kuwa, ana furaja ya kuwepo Barca, hakuna haja ya kuondoka.’

FIFA YASEMA CLUB YA FENERBAHCE NA BASIKTAS ZIMESHINDA RUFANI YAO

Shirikisho la kandanda barani Ulaya-UEFA, limesema kuwa klabu za Fenerbahce na Besiktas za Uturuki zimeshindwa rufani zao za kupinga adhabu ya kushiriki michuano inayoandaliwa na shirikisho hilo. Fernabahce ambao ilikuwa washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu walifungiwa kushiriki michuano yoyote ya Ulaya kwa misimu miwili huku Besiktas ambao walifuzu kushiriki michuano ya Europa League wao wamefungiwa msimu mmoja. Klabu zote mbili zinatuhumiwa na kashfa ya upangaji matokeo katika baadhi ya mechi za Ligi ya Kuu ya Soka nchini Uturuki mwaka 2011. Baada ya kugonga mwamba UEFA, klabu hizo bado zina haki ya kukata rufani katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS.

FIFA BADO USO KWA USO NA CAMEROON KATIKA MICHEZO

Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limedai kuwa klabu ya Coton Sport ya Cameroon haitaruhusiwa kucheza mechi yao ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika mwishoni mwa wiki hii kwasababu ya adhabu iliyopewa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot na FIFA. Hatua ya kuzuiwa kwa klabu hiyo kunazidi kuleta utata katika michuano hiyo mikubwa kabisa ya vilabu barani Afrika huku mahasimu wa soka nchini Misri klabu ya Zamalek na Al Ahly ambao ndio mabingwa watetezi nao wakiwa hawajui hatma ya mechi baina yao kwasababu ya vrugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo. Timu nane zilizofanikiwa kuvuka hatua ya makundi, ndio zinatarajiwa kuchuana kutafuta washindi watakaocheza nusu fainali ya michuano hiyo katika mechi zao za kwanza mwishoni mwa wiki hii. FIFA imesema kuwa tayari wameshaanza mazungumzo kujaribu kutatua mgogoro wa Cameroon lakini mpaka sasa hakuna lolote lililofikiwa mpaka kuwashawishi kuondoa adhabu ya kuifungia nchi hiyo kushiriki michuano yoyote ya kimataifa waliyoitoa Julai 4 mwaka huu. Kufungiwa kwa Cameroon kumekuja kufuatia uchaguzi wa Juni 19 ambao Mohammed Iya alichaguliwa tena kuongoza Fecafoot pamoja na kukamatwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha wakati akiongoza kampuni ya Cotton Development Corporation inayomiliki timu ya Cotton Sport.

REAL MADRID YATAJWA KUWA CLUB YENYE THAMANI ZAIDI DUNIANI

CLUB ya Real Madrid ya Hispania imetajwa kuwa klabu yenye thamani zaidi katika orodha ya timu za michezo 50 zenye thamani zaidi duniani iliyotolewa na jarida Forbes la nchini Marekani. Katika orodha hizo timu za Ligi Kuu ya Mpira wa Kimarekani-NFL ndizo zilizoonekana kutawala kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida hilo Madrid ambao ni mabingwa mara tisa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wana utajiri unaofikia dola bilioni 3.3, utajiri huo ukiwa umeongezeka kwa dola bilioni 1.88 kulinganisha na mwaka uliopita baada ya kuongeza mapato yao kwa kuingia mikataba na kampuni za Adidas na Shirika la Ndege la Emirates. Manchester United wamepigwa kikumbo na Madrid na kushuka mpaka nafasi ya pili wakiwa na utajiri wa dola bilioni 3.17 wakati mabingwa wa Hispania Barcelona wao wamekwea kutoka nafasi ya tano mpaka ya tatu wakiwa na utajiri unaofikia dola bilioni 2.6. Nafasi ya nne inashikiliwa na timu ya Baseball ya Marekani ya New York Yankees ambao wana dola bilioni 2.3, wakifuatiwa na Dallas Cowboys ya NFL dola bilioni 2.1 na New England Patriots dola bilioni 1.6. Nyingine ni Los Angeles Dodgers ya baseball dola bilioni 1.6, timu za NFL Washington Redskins na New York Giant pamoja na klabu ya soka ya Arsenal ya Uingereza ambazo zote hizo zina utajiri wa dola bilioni 1.3.

KAMPUNI YA VIFAA VYA MICHEZO ADIDAS YA SIMAMISHA MKATABA WA TYSON GAY

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas imesimamisha mkataba wake wa udhamini na mwanariadha nyota wa mbio fupi Tyson Gay wa Marekani baada ya kukutwa na chembechembe za dawa za kuongeza nguvu. Msemaji wa kampuni alidai kuwa awameshtushwa na tuhuma hizo kwa Gay na hata kama bado hajakutwa na hatia ya kosa hilo moja kwa moja kampuni itasimamisha udhamini wake mpaka hapo hukumu itakapotolewa. Gay mwenye umri wa miaka 30, ndio mwanariadha wa pili mwenye kasi zaidi duniani katika mbio za mita 100 akiwa sambamba na Yohan Blake wa Jamaica na pia ndiye mwanariadha aliyeweka rekodi ya kasi zaidi kwa mwaka huu. Nyota huyo ambaye aliwahi kuwa bingwa wa dunia katika mbio za mita 100, 200 na mita 400 kupokezana vijiti mwaka 2007 alishindwa kukata tuhuma hizo na kudai kuwa alimwamini mtu ambaye alimwangusha na hivyo atapokea adhabu yoyote atakayopewa.