Tuesday, July 16, 2013

KUTOA OFA PAUNI MILIONI 40 KUMNUNUA HULK--CHELSEA

Katika harakati za usajili baada ya kuikosa saini ya kumnasa Straika hatari wa Uruguay, Edinson Cavani, ambae sasa yuko njiani kukamilisha ku

hamia PSG kutoka Napoli, Chelsea sasa imemgeukia Straika wa Klabu ya Urusi Zenit St Petersburg, Hulk, anaetoka Brazil.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ana nia ya kuongeza safu yake ya Ushambuliaji na tayari ameshamnunua Mchezaji wa Germany Andre Schurrle huku kukiwa na tetesi Mastraika wa sasa, Fernando Torres na Demba Ba, huenda wakapigwa bei.
Katika Msimu wake wa kwanza na Zenit, Hulk alifunga Bao 11 katika Mechi 30 na kabla hajahamia huko Urusi, akiwa huko Portugal na FC Porto, Hulk aliifungia Klabu hiyo Bao 54 katika Mechi 99 za Primera Liga na Jumla ya Mabao yake kwa FC Porto ni 78.
Inadaiwa Chelsea imetoa Ofa ya kwanza ya Pauni Milioni 40 kwa Mchezaji alienunuliwa Septemba Mwaka Jana kwa Pauni Milioni 35.