Friday, March 21, 2014

MAN UNITED YAPANGWA NA BAYERN MUNICH ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE


Mechi za Robo Fainali kuchezwa Apirili 1 & 2, Marudiano Aprili 8 & 9
Droo ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iimefanyika huko Nyon, Uswisi na Mabingwa Watetezi Bayern Munich watakutana na Mabingwa wa England, Manchester United, na Mechi ya Kwanza kuchezwa Old Trafford Aprili 1 au 2.
Chelsea watakuwa Ugenin kucheza na Paris Saint-Germain.
Barcelona wataanza kwao Nou Camp kwa kucheza na wenzao wa Spain Atletico Madrid.
Real Madrid wataanza Nyumbani Santiago Bernabeu kwa kucheza na Klabu ya Germany Borussia Dortmund.
Mechi za Marudiano zitachezwa Wiki moja baadae.
Barcelona v Atletico Madrid
Real Madrid v Borussia Dortmund
Paris St Germain v Chelsea
Manchester United v Bayern Munich
Mechi kuchezwa April 1/2 and April 8/9

VPL, LIGI KUU VODACOM YANGA KUIKABILI RHINO YA TABORA


YANGA, RHINO KUCHEZA TABORA VPL
Yanga inaumana na Rhino Rangers katika moja kati ya mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa wikiendi hii katika miji miwili tofauti.
Mechi hiyo itafanyika kesho (Machi 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora ambapo kiingilio kitakuwa sh. 5,000 kwa jukwaa kuu na sh. 3,000 mzunguko.
Nayo JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbeya City katika mechi itakayochezwa kesho Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Jumapili) kwa mechi nne ambapo Simba itacheza na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex. Mechi hizo mbili zitakuwa ‘live’ kupitia Azam Tv.
Mechi nyingine za Jumapili ni Mgambo Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Ruvu Shooting na Ashanti United zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
20
12
8
0
27
44
2
Yanga SC
19
11
7
1
29
40
3
Mbeya City
21
10
9
2
10
39
4
Simba SC
21
9
9
3
17
36
5
Kagera Sugar
21
8
8
5
3
32
6
Ruvu Shooting
20
7
7
6
-4
28
7
Coastal Union
21
5
11
5
1
26
8
Mtibwa Sugar
21
6
8
7
-1
26
9
JKT Ruvu
21
8
1
12
-13
25
10
Prisons FC
20
3
10
7
-4
19
11
Mgambo JKT
20
4
6
10
-17
18
12
Ashanti United
21
4
6
11
-18
18
13
JKT Oljoro
21
2
9
10
-16
15
14
Rhino Rangers
21
2
7
12
-14
13
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Machi 26
Mgambo JKT v Azam FC
Yanga v Tanzania Prisons
Jumamosi Machi 29
Ashanti United v JKT Oljoro
Jumapili Machi 30
Mbeya City v Tanzania Prisons
Kagera Sugar v Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar v Coastal Union
JKT Ruvu v Rhino Rangers
Azam FC v Simba
Mgambo JKT v Yanga
KIKOSI KAZI KUSHUGHULIKIA TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB zimeunda kikosi kazi (task force) kwa ajili ya kushughulikia matumizi ya tiketi za elektroniki ambayo yalisimamishwa kutoka na changamoto mbalimbali zilizokuwa zimejitokeza.
TFF na CRDB zimefanya kikao cha pamoja jana (Machi 20 mwaka huu) kuhusu masuala ya tiketi za elektroniki na kukubaliana kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya uboreshaji matumizi ya mfumo huo.
Kikosi kazi hicho kitakuwa na wajumbe kutoka TFF na CRDB. Kwa upande wa TFF wajumbe wake ni Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama, Evodius Mtawala, Ofisa Habari na Mawasiliano, Boniface Wambura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa shukrani za kipekee kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei ambaye alihudhuria binafsi kwenye kikao akiongoza timu yake.
Malinzi amesema ni imani ya TFF kuwa mfumo wa tiketi za elektroniki ndiyo mkombozi wa ulinzi wa mapato milangoni, na anaamini kwa pamoja TFF na CRDB zitafanikisha matumizi hayo ya tiketi za elektroniki.