Timu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kukichalaza kikosi cha pili cha Azam fc mabao 2-0 dhidi ya katika mechi
maalumu ya kirafiki ya Tamasha la Usiku wa Matumaini usiku huu uwanja wa Taifa,
uliopo maeneo ya Chang’ombe, jijini Dar es salaam.
Kwa
ushindi huo, wakata miwa wa mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro
wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Matumaini.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa kocha mkuu wa Mtibwa, Mecky Mexime
kuonesha wachezaji wake jinsi walivyoiva, wachezaji wawili wakongwe, Musa
Hassan Mgosi na Vicent Barnabas walionesha kandanda l
a kuvutia na kudhihirisha kuwa utu uzima dawa.
Baada
ya mechi ya leo , kikosi hicho cha Azam kitasafiri muda wowote kuelekea mjini Kigali
nchini Rwanda kikifuata kikosi cha kwanza kinachoshiriki kombe la Kagame.
a kuvutia na kudhihirisha kuwa utu uzima dawa.