Wednesday, September 10, 2014

JE TUFIKA KUHUSU TAIFA STARS HII AMA NDIO MWISHO

Hakuna kitu kinawaumiza watanzania kuhusu kilio kikubwa cha wadau na wapenzi wa soka nchini Tanzania ni kuitaka serikali, TFF na vyama wanachama wake pamoja na klabu zote kuwekeza katika soka la vijana kwa manufaa ya Taifa.
Tatizo la soka la Tanzania ni la kimfumo. Hakujawa na njia sahihi ya kupata wachezaji na kusababisha kuborongo kwa muda mrefu.
Aina ya wachezaji wanaopatikana Tanzania ni wale wasiokuwa na misingi ya mpira tangu utotoni, kwasababu hakuna akademi za kisasa na hata za kawaida kwa maeneo mengi ya nchi hii, hivyo vijana wenye vipaji vya soka hujikuta hawana kwa kujiendeleza.
Soka la vijana ni muhimu na lazima Taifa kama Taifa liandae mpango mkakati wa kitaifa kwa malengo ya kuwa na falsafa ya Taifa na mfumo sahihi wa kuibua, kukuza na kulinda vipaji vya soka.
Marsh aliachishwa kazi ya kuinoa Stars sambamba na kocha Mdenish, Kim Poulsen kwa madai ya wawili hao kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa na Shirikisho la soka la Tanzania, TFF.
Hata hivyo wakati Kim anavunjiwa mkataba, Mashi alikuwa wodini akipata matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Usidhani huwa anakaa bure. Marsh ni moja ya watu wachache nchini wenye kiu ya kuona soka la nchi hii linapiga hatua.
Tangu mwaka 1991 anamiliki kituo chake cha kuibua, kulea na kukuza vipaji mkoani mwanza.

WADHAMINI WA VPL WAGAWA JEZI KWA TIMU ZA VPL KWA AJILI YA SEPT 20 VPL

Ikiwa zimebaki siku 10 kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu msimu wa 2014-2015 wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom watoa jezi kwa vilabu vyote 14 vitakavyoshiriki ligi hiyo.
Katika hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu za Ligi Kuu msimu mpya leo, Vodacom wamekabidhi jezi za rangi ya kijani na njano kwa Yanga na nyekundu na nyeupe kwa Simba, lakini muundo ni mmoja kila kitu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwakilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye alihakikisha timu zote 14 za Ligi Kuu zinapatiwa vifaa hivyo.
Timu zote 14 zilituma wawakilishi wao katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam.  
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu, mabingwa watetezi, Azam FC wakifungua dimba na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo, wakati washindi wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 20.
Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC wataanza kampeni ya kutwaa tena taji hilo Septemba 21 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumapili wiki hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Yanga SC.

MAJIMAJI YAWEKA HADHARANI KIKOSI CHAKE KWA AJILI YA LIGI DARAJA LA KWANZA

 ya zamani Tanzania, Majimaji FC WANALIZOMBE ya Songea mkoani Ruvuma imetaja kikosi cha wachezaji 26 iliyowasajili kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara msimu wa 2014-2015.
Ofisa Habari wa Majimaji ya Songea, Nathan Mtega ametaja kikosi cha msimu ujaoAmesema katika kikosi hicho, wachezaji 12 ni wapya ambao ni Oswald Issa, Samir Said, Emmanuel Maganga, Ally Mohamed, Kudra Omary, Said Fundikira, Mrisho Said, Idd Kipagule, Mohamed Omary, Yohana Kimburu na Msafiri Abdallah.
Amewataja wachezaji wa zamani 14 watakaoendelea kuitumikia klabu hiyo kuwa ni pamoja na Anthony Mwingira, Eliuta Ndunguru, Bahati Yussuf, Gerarrd Mbena, Abdallah Aus, Ditram Nchimbi, Filoteus Mahundi, Mpoki Mwakinyuke, Alex Zegega, Sadiq Gawaza, Odo Nombo, Frank Sekule, Marcel Boniventure na Freddy Mbuna.