Tuesday, May 21, 2013

PEREZ ATANABAISHA KUWA CLUB HIYO INAKAZI KUPATA KOCHA MPYA.

RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ametanabaisha kuwa klabu hiyo ina Kazi nzito mrefu wa makocha akiwemo kocha Carlo Ancelotti wa Paris Saint-Germain-PSG ili kuziba pengo la Jose Mourinho ambaye anaondoka. Klabu hiyo iliweka wazi Jumatatu kuwa Mourinho ambaye ni raia wa Ureno ataondoka Santiago Bernabeu katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi na kazi ya kutafuta mbadala wake tayari imeanza. Perez alithitisha kuwa tayari wameshazungumza na Ancelotti ambaye ameonyesha nia ya kuikacha PSG lakini klabu hiyo imeamua kumng’ang’ania kocha huyo Muitaliano. Mbali na kuzungumza na Ancelotti Perez pia amesema walizungumza na mkurugenzi mkuu wa PSG ili kuangalia uwezekano wa kumchukua Ancelotti lakini walikataa, hivyo wana siku chake za kufikiria suala hilo ingawa amedai kuwa wana orodha ya makocha wengi walioomba nafasi hiyo.

TOURE KOLO VS EBOUE WAKABILIWA NA KIFUNGO.

Wanandinga wa kimataifa wa Ivory Coast, Kolo Toure anayekipiga katika klabu ya Manchester City na Emmanuel Eboue wa klabu ya Galatasaray wanakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo kufuatia kauli walizozitoa katika vyombo vya habari kulishambulia Shirikisho la Soka la nchi hiyo. Wachezaji hao wawili wameenguliwa katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kitapambana na Gambia na Tanzania katika mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Hatua hiyo ya kuwaacha wachezaji hao ilifikiwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo kufuatia malalamiko yaliyofikishwa na kocha anayekinoa kikosi hicho Sabri Lamouchi. Ivory Coast inatarajia kuchuana Gambia Juni 8 mwaka huu kabla ya kupambana na Taifa Stars Juni 16 katika michezo ya kundi C ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia.

MICHO ATARAJI KUTAMBULISHWA TIMU YA TAIFA UGANA THE CRANES.

KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Milutin Sredojevic Micho anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya timu ya taifa Uganda inayojulikana kama The Cranes. Micho ambaye ni raia wa Serbia anatarajiwa kutangazwa mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya Shirikisho la Soka la Uganda-FUFA na kumaliza tetesi zilizozagaa karibu mwezi mzima baada ya kutimuliwa kwa Bobby Williamson mwezi uliopita. Micho mwenye umri wa miaka 43 alitimuliwa kuinoa Rwanda mwezi huohuo ambao Bobby naye alitimuliwa kuifundisha The Cranes na sababu za kutimuliwa kwao zinafanana kwani wote wawili timu zao zilikuwa zikifanya vibaya katika mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia. Changamoto ya kwanza atakayokutana nayo Micho ni kukirejesha kikosi hicho katika ari ya ushindani na kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zao za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia pamoja na ile ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani-CHAN.

14 RCL KUUMANA RAUNDI YA PILI WIKIENDI


LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao inaingia raundi ya pili wikiendi hii kwa kukutanisha timu 14 zilizofanikiwa kusonga mbele.

Timu zitakazocheza raundi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ni Abajalo ya Dar es Salaam itakayokuwa mwenyeji Kariakoo ya Lindi katika mechi itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Siku hiyo hiyo Uwanja wa Azam ulioko Chamazi utatumika kwa mechi kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga wakati Jumapili (Mei 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Machava FC ya Kilimanjaro na Mpwapwa Stars ya Dodoma itakayochezwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Stand United ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida katika mechi itakayochezwa Jumapili (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Polisi Jamii ya Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana siku hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Mjini Kigoma kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi. Nayo Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya Njombe katika mechi itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sabasaba.

Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu wakati timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI MECHI YA FIFA
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi (referee assessor) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.

Mechi hiyo ya Kundi B, Kanda ya Afrika kati ya Cape Verde na Equatorial Guinea itafanyika Juni 8 mwaka huu saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Verzea mjini Praia.

Waamuzi wa mechi hiyo ambao watatoka Angola ni Martins De Carvalho Helder, Dos Santos Jerson Emiliano, Da Silva Lemos Julio na Muachihuissa Caxala Antonio. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Diarra Massa Momoye wa Mauritania.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MTU SPECHOO MOURINHO KWA HERI REAL MADRID".

RAIS wa Real Madrid Florentino Perez leo usiku ametangaza kuondoka kwa Kocha wao Mkuu Jose Mourinho kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.
Akihutubia Wanahabari walioshuhudia Perez amesema Tumeamua kumaliza uhusiano wet na mtu spechu. Hakuna Mtu aliemfukuzwa kazi bali ni makubaliano ya pande mbili.
Real madrid ikiwa imebakisha Mechi 2 za La Liga, Real Madrid wako Nafasi ya Pili na Pointi 13 nyuma ya Mabingwa FC Barcelona na Ijumaa iliyopita walitwangwa 2-1 kwenye Fainali ya Copa del Rey na Mahasimu wao Atletico Madrid.
MOURINHO NA MATAJI YAKE:
UCL: 2004 (Porto), 2010 (Inter Milan)
UEFA CUP: 2003 (Porto)
BPL: 2005, 2006 (Chelsea)
FA CUP: 2007 (Chelsea)
LEAGUE CUP: 2005, 2007 (Chelsea)
LA LIGA: 2012 (Real Madrid)
COPA DEL REY: 2011 (Real Madrid)
SERIE A: 2009, 2010 (Inter Milan)
COPPA ITALIA: 2010 (Inter Milan)
PRIMEIRA LIGA: 2003, 2004 (Porto)
TACA DE PORTUGAL: 2003 (Porto)
Aidha Katika Miaka mitatu aliyoifundisha  Real, Mourinho ameshindwa kuivusha Real katika Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kutolewa katika hatua hiyo katika Misimu yote hiyo na Msimu huu ikichalazwa na Borussia Dortmund kwa kuchapwa Bao 4-1 huko Germany na  nyumbani wakijiongeza kwa kushinda 2-0.
ikumbukwe kabla Mourinho kutua Real Madrid, Klabu hiyo ilikaa Miaka miwili bila Taji lolote n baada ya kufika yeye walitwaa Copa del Rey Mwaka 2011 na kufuatia Ubingwa wa Spain wa La Liga Mwaka 2012 lakini Msimu huu ametoka mikono mitupu ukiachia Super Cup.
katika tetesi zilizopo kwa taarifa mbalimbali inaaminika kuwa Mourinho anarejea katika Klabu yake ya zamani ya jijini london club ya Chelsea, na  kwa Real  inaaminika akatatua Carlo Ancelotti kutoka PSG ingawa bado uthibitisho rasmi  haukutolewa mbali ya PSG kumkatalia Ancelotti kuhama.

VILLA -BOAS ASEMA BALE NI MUHIMU KUBAKI CLUBUNI"

BOSI wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Andre Villas-Boas ametanabaisha kuwa ni jambo la muhimu kwa klabu hiyo kumbakisha mshambuliaji wake nyota Gareth Bale kama wanataka kufanya vizuri zaidi msimu ujao. Spurs wamekosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika siku ya mwisho baada ya kuzidiwa kwa alama moja na mahasimu wao wa jiji la London Arsenal ambao walimaliza msimu katika nafasi ya nne. Kukosa huko nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya kumeleta mjadala kuhusu mustabali wa winga huyo mwenye umri wa miaka 23 raia wa Wales. sambamba na hayo Villas-Boas amesema kama wanahitaji kufanya vyema msimu ujao ni lazima wawabakize wachezaji nyota na hilo ndio aliloambia na viongozi wa juu wa klabu hiyo. Bale amekuwa akifukuziwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya ambavyo vitashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa ikiwemo Real Madrid.